sanalii
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,639
- 5,767
Kuna tukio limetokea Kibaha, Kwa Mfipa, familia imevamiwa, wameibiwa vitu ndani ikiwemo na gari, wamechukua na simu za uwakala wamelazimisha wapewe na PIN, wamepewa.
Kama haitoshi wamewafunga kamba mke na mume, wakawaweka kwenye mashimo ya choo tofauti, mtoto wa miezi saba hajulikani yuko wapi. Labda wameondoka nae, au nae wamemuweka shimo tofauti haieleweki. Mungu amuweke salama huko aliko, pole kwa familia.
Sasa najiuliza kama wakiamua kutupa hizo simu kisha mtu akajichanganya kuokota, atakumbana na kesho mbaya sana.
Kwasasa ukiokota simu ni bora uipeleke kituo cha polisi, matukio yamekuwa mengi na simu ya mhusika ni moja ya trace. Unaweza kudhani umepata kumbe ndio mlango wa gereza unaufungua.
Ni hatari sana.