Kwa sasa, kuokota simu si bahati tena bali ni balaa

Kwa sasa, kuokota simu si bahati tena bali ni balaa

Kuna mwingine kauziwa simu ya mchungaji ambaye alivamiwa akauliwa… jamaa anasota jela aliacha mkewe mjamzito mpk kajifungua yeye hajatoka..!!

Aliyemuuzia hamjui na hajapatikana mpk sasa.!! Hizi tamaa zingine sio nzuri.!
Jamooniii....
 
Binafsi nikiona hela naokota, sijisumbui, wala kuhangaika na kitu ninachokiona njiani. Siokoti na hata polisi sijisumbui kupeleka. Polisi sio waaminifu
 
Kuna simu zina feature ya kurekodi sura ya mtumiaji kwa siri
Simu zote tuu zinaturekodi kwa siri, we unajua hiyo camera ya mbele hapo ina kazi gani?

Kwa kweli wametuweza, mpaka sura zetu wanazijua vema.

Unafikiri umenunua simu, kumbe umejiwekea TRACKING DEVICE.

Cc: Extrovert
 
Kwa polisi wetu hawa, kuliko kuiokota na kuipeleka kwao, bora usiokote kabisaaa achana nayo
 
Upo sahihi mkuu, kuna jamaa huko migombani alijiokotea simu smartphone akajua amepata kumbe kapatikana. Ile simu kuna tukio la wizi lilitokea na mwenye simu alijeruhiwa vibaya hali iliyopelekea kupoteza maisha siku chache baadae.

Ile simu ikafuatiliwa baada ya miezi 6 ya tukio kutokea wakamkuta nayo alieiokota, kufupisha kwa sasa yupo jela.
Kuna Kijana huku aliletewa simu auziwe wakakubaliana elfu sabini, Smartphone. Jamaa akainunua kwakuwa ana uhitaji na hakuwa na kiasi cha kutosha kumudu kuchukua dukani.

Aliyemuuzia ni mpitaji tu, na haikuwa hata na password. Kizaazaa kikaja aada kama wiki, siku moja katulia tu anashangaa askari hawa hapa. Wakamdaka. Kilichotokea asikwambie mtu. Mashtaka aliyosomewa yanaogofya. Akaambiwa mara ya mwisho simu kuibiwa walivunja mlango wa nyumba ya mhusika na kuchukua simu na vitu vingine pamoja na pesa shilingi laki tano.

Mwanzo aliona ni rahisi tu akitoa maelezo kuwa naye aliuziwa tu itaeleweka. Badala yake issue ikawa serious. Alijikuta anapoteza zaidi ya milioni na nusu hadi msala kuisha na hayo yote walifanya wazazi wake kumnusuru.

Ashukuru Mungu hakukuwa na tukio la mtu kuumizwa au kuuwawa siku ya upotevu huo, vinginevyo hili balaa lingemtafuna hadi mifupa.

Kwa hiyo, mbali tu na kuokota, pia kununua hizi Devices used sio salama sana sababu wanaotuletea tunakuwa hatuna uhakika na uhalali wa umiliki wao. Unaweza kuta hata mtu hakuibiwa na fedha, ila kwakuwa wewe ndio unakutwa na mali, mtu anaamua kukuungia tu
 
Kuna tukio limetokea Kibaha, Kwa Mfipa, familia imevamiwa, wameibiwa vitu ndani ikiwemo na gari, wamechukua na simu za uwakala wamelazimisha wapewe na PIN, wamepewa.

Kama haitoshi wamewafunga kamba mke na mume, wakawaweka kwenye mashimo ya choo tofauti, mtoto wa miezi saba hajulikani yuko wapi. Labda wameondoka nae, au nae wamemuweka shimo tofauti haieleweki. Mungu amuweke salama huko aliko, pole kwa familia.

Sasa najiuliza kama wakiamua kutupa hizo simu kisha mtu akajichanganya kuokota, atakumbana na kesho mbaya sana.

Kwasasa ukiokota simu ni bora uipeleke kituo cha polisi, matukio yamekuwa mengi na simu ya mhusika ni moja ya trace. Unaweza kudhani umepata kumbe ndio mlango wa gereza unaufungua.

Ni hatari sana.
Inauma sana mtoto mchanga wa miezi saba anachukuliwa na hao wavamizi
 
Kitu chochote kilichotumika ni hatari sana! Hata kuoa mke aliyezaa ni kuoa mke na mali ya mtu! Potelea mbali binti asiye na bikra ndo umoumo labda kwa msaada wa Mungu!
 
Kuna tukio limetokea Kibaha, Kwa Mfipa, familia imevamiwa, wameibiwa vitu ndani ikiwemo na gari, wamechukua na simu za uwakala wamelazimisha wapewe na PIN, wamepewa.

Kama haitoshi wamewafunga kamba mke na mume, wakawaweka kwenye mashimo ya choo tofauti, mtoto wa miezi saba hajulikani yuko wapi. Labda wameondoka nae, au nae wamemuweka shimo tofauti haieleweki. Mungu amuweke salama huko aliko, pole kwa familia.

Sasa najiuliza kama wakiamua kutupa hizo simu kisha mtu akajichanganya kuokota, atakumbana na kesho mbaya sana.

Kwasasa ukiokota simu ni bora uipeleke kituo cha polisi, matukio yamekuwa mengi na simu ya mhusika ni moja ya trace. Unaweza kudhani umepata kumbe ndio mlango wa gereza unaufungua.

Ni hatari sana.
Ushauri mzuri sana!
 
Kwasasa ukiokota simu ni bora uipeleke kituo cha polisi, matukio yamekua mengi na simu ya mhusika ni moja ya trace. Unaweza kudhan umepata kumbe ndio mlango wa gereza unaufungua. Ni hatari sana....

Never ever usije ukajaribu hilo kosa..unaweza kuangushiwa jumba bovu
Muhimu ni kuiacha kama ulivyoikuta. Hata usiiguse.
 
Back
Top Bottom