Kwa sasa, kuokota simu si bahati tena bali ni balaa

Kuna mwingine kauziwa simu ya mchungaji ambaye alivamiwa akauliwa… jamaa anasota jela aliacha mkewe mjamzito mpk kajifungua yeye hajatoka..!!

Aliyemuuzia hamjui na hajapatikana mpk sasa.!! Hizi tamaa zingine sio nzuri.!
Jamooniii....
 
Binafsi nikiona hela naokota, sijisumbui, wala kuhangaika na kitu ninachokiona njiani. Siokoti na hata polisi sijisumbui kupeleka. Polisi sio waaminifu
 
Kuna simu zina feature ya kurekodi sura ya mtumiaji kwa siri
Simu zote tuu zinaturekodi kwa siri, we unajua hiyo camera ya mbele hapo ina kazi gani?

Kwa kweli wametuweza, mpaka sura zetu wanazijua vema.

Unafikiri umenunua simu, kumbe umejiwekea TRACKING DEVICE.

Cc: Extrovert
 
Kwa polisi wetu hawa, kuliko kuiokota na kuipeleka kwao, bora usiokote kabisaaa achana nayo
 
Kuna Kijana huku aliletewa simu auziwe wakakubaliana elfu sabini, Smartphone. Jamaa akainunua kwakuwa ana uhitaji na hakuwa na kiasi cha kutosha kumudu kuchukua dukani.

Aliyemuuzia ni mpitaji tu, na haikuwa hata na password. Kizaazaa kikaja aada kama wiki, siku moja katulia tu anashangaa askari hawa hapa. Wakamdaka. Kilichotokea asikwambie mtu. Mashtaka aliyosomewa yanaogofya. Akaambiwa mara ya mwisho simu kuibiwa walivunja mlango wa nyumba ya mhusika na kuchukua simu na vitu vingine pamoja na pesa shilingi laki tano.

Mwanzo aliona ni rahisi tu akitoa maelezo kuwa naye aliuziwa tu itaeleweka. Badala yake issue ikawa serious. Alijikuta anapoteza zaidi ya milioni na nusu hadi msala kuisha na hayo yote walifanya wazazi wake kumnusuru.

Ashukuru Mungu hakukuwa na tukio la mtu kuumizwa au kuuwawa siku ya upotevu huo, vinginevyo hili balaa lingemtafuna hadi mifupa.

Kwa hiyo, mbali tu na kuokota, pia kununua hizi Devices used sio salama sana sababu wanaotuletea tunakuwa hatuna uhakika na uhalali wa umiliki wao. Unaweza kuta hata mtu hakuibiwa na fedha, ila kwakuwa wewe ndio unakutwa na mali, mtu anaamua kukuungia tu
 
Inauma sana mtoto mchanga wa miezi saba anachukuliwa na hao wavamizi
 
Kitu chochote kilichotumika ni hatari sana! Hata kuoa mke aliyezaa ni kuoa mke na mali ya mtu! Potelea mbali binti asiye na bikra ndo umoumo labda kwa msaada wa Mungu!
 
Ushauri mzuri sana!
 
Muhimu ni kuiacha kama ulivyoikuta. Hata usiiguse.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…