Kwa sasa shahada si kitu tena, tutafuta namna nyingine ya kuokoa vijana

Forex nayo hata mimi ilinitisha baada ya kusoma malalamiko ya watu waliopigwa mkwanja mrefu wakabakia fukara
Hapo ndio tunapokosea mkuu,

Hata kilimo utakutana na watu wanaolia kwamba kimewapiga lakini hapo hapo kuna watu wanatajirika kwa kilimo hicho hicho. Hakuna fursa isiyo na chamgamoto.

Forex matapeli wapo sana ila ni ni wewe tu, uzuri forex elimu yake iko online. Yani kila kitu unakipata kiganjani mwako.
 
Umeandika ukweli, tatizo ni Serikali ukifanya Biashara ili uzalishe ajira wanakufilisi, wabunge wanatunga sheria mbovu za kufilisi watu, alafu watoto na Ndugu zao ndio wanatembea na bahasha mkononi, Ni laana tupu.
 
Nimeliona hili bandiko Instagram je ni wewe uliyeliweka or copy and paste
 
Wakati haya yakitokea, Rihana ametoka kununua nyumba ya jirani yake kwa Bilioni 23;fedha ya Kitanzania! Kweli Dunia haina usawa.
 
Hata VETA kusha saturate. Tuwafundishe watoto jinsi ya kujitegemea bika kujali ni VETA, chuo kikuu, la7 nk.
Wazazi tufanye uwekezaji usio kufa mapema, kama viwanda vidogo, kilimo cha mazao ya kudumu, uvuvi, ufugaji nk.
Wazazi wengi ni chanzo cha umasikini wa watoto wao.
Mzazi ukijikwamua watoto watajikwamua.
Mtu ana mashamba kijijini kwao heka hata 100 ametayelekeza yupo mjini Dar, anashindwa hata kupanda miti pori watoto waje wachome mikaa wapate mitaji.
Chanzo ni wazazi serikali inafuatia jamii inamalizia.
 
Umeandika vizuri sana
 
Point tupu
 
Ccm imewatengezea watz maisha mabovu sana sana watoto wa viongozi ni wabunge,madc,na madasi,
Tatizo kubwa ni sisi watazania wenyewe tuna viongozi wasio na mission wala vision kila uchaguzi tunachagua tena hao hao kwa kupewa kofia na fulana !!!!
 
Mimi huwa siwaonei huruma watz !!! Suburi uchaguzi uje utaona watakavyo vaa nguo za kijani na kukebehi wenye Sera mbadala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…