GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Lakini ujue kabla ya kuwasha indicator yeye alishakuonesha ishara ya kukusimamisha. Ukikata kona hatadai kuwa umefanya hivyo kumkwepa?Mimi sijasoma sheria za barabarani hata kidogo mkuu! Ila kwa maelezo yako na askari wetu wa nchi hii kazi unayo!
Mimi ningesimama hapo hapo pointi B na kuwasha indicator ya kuingia pointi B, wala nisingeenda pointi C mpaka aniite
Ndiyo maana nimesema nitasimama hapo hapo huku nimewasha indicator ya kuingia pointi B!Lakini ujue kabla ya kuwasha indicator yeye alishakuonesha ishara ya kukusimamisha. Ukikata kona hatadai kuwa umefanya hivyo kumkwepa?
Acha uongo mkuu😃Ndiyo maana nimesema nitasimama hapo hapo huku nimewasha indicator ya kuingia pointi B!
Ngoja waje mkuu mimi sina chochote ninachokijua kuhusu sheria za barabarani
Kwakuwa ulikuwa unaenda Point B itabidi uende point B kwa hatua chache halafu tia Gari Pembeni kumsubiri atakuja..Unaendesha gari kutoka point A kwenda point B.
Point B ipo hatua chache kutoka iliko point C ambako kuna kizuizi cha Polisi.
Ulipokaribia point B, ambapo utapaswa kukata kulia kwa kuwa ndiko unakoelekea hivyo hulazimiki kufika point C, na kabla hujaindicate kuwa unataka kukata kona kwenda point B, askari akakuonesha ishara ya kusimama kwa ajili ya ukaguzi.
Kwa mujibu wa Sheria, unapaswa kufanyeje?
1. Uende hadi point C ukaguliwe kwanza kisha ugeuze kwa ajili ya kwenda point B?
2. Utaonesha ishara ya kuelekea point B bila kujali kuwa askari alishakuashiria kusimama?
Kujua umuhimu wa kuwasha indicator imetokana na mimi kuona vyombo vya moto vikiwasha indicator vinapo katiza upande fulani!Acha uongo mkuu😃
Hujui chochote wakati unajua mpaka umuhimu wa indicator unapotaka kukata kona😀
Inawezekana hujui Sheria zote, lakini inawezekana ukawa umeniacha mbali sana kwenye uelewa wa Sheria za usalama barabarani.