Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
KWA SISI WATIBELI MTOTO CHINI YA MIAKA SITA ANAFUNDISHIWA NYUMBANI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
1. Iko hivi Sisi watibeli foundation ya mtoto ni miaka 0(akiwa tumboni) mpaka akifikisha miaka 6/7.
2. Foundation hii mtoto wa Kitibeli atajengewa msingi wa
a) kiafya ya mwili kuanzia Lishe,
b) Afya ya Roho kumfundisha Imani na maadili.
c) Afya ya kihisia, kuunganisha bond baina ya mzazi na mtoto, mahusiano, kumfundisha upendo, mahusiano, lugha.n.k
3. Mtoto atashinda nyumbani na kucheza nyumbani. Aki programiwa kuhusu tamaduni, kanuni, Imani, falsafa za maisha. Utibeli.
4. Kwa Watibeli Mzazi ndiye Mwalimu wa Kwanza. Baba na Mama ndio waalimu wa basic education na iwe true education
5. Kama Mzazi wa kitibeli atakuwa busy na majukumu ya uzalishaji, kazi au uongozi, basi ataajiri mwalimu anayemuamini. Atakayekuja kumfundisha mtoto nyumbani kwake. Sio mtoto aende Kwa Mwalimu. Bali mwalimu ndiye Aje.
6. Mtoto wa chini ya miaka 6 wa kitibeli atafundishwa mambo ya kusoma, kuandika, banguabongo, utatuzi wa matatizo mepesi, stadi za maisha ya Kila Siku na hayatazidi masaa manne kwa Siku.
7. Mtoto wa kitibeli umri huo mara nyingi atakuwa na wazazi wake kuliko mtu mwingine yeyote . Kwa maana hiyo utaona Mtibeli itampasa ajiajiri zaidi kuliko kuajiriwa na hii sio kwaajili ya uchumi tuu bali kujenga familia.
8. Mtoto akifikisha kuanzia miaka 6 ndio ataanza kuchangamana kidogokidogo kwa uangalizi mkubwa wa wazazi wake.
9. Kama atapelekwa shule ataenda shule ya karibu ambapo Mzazi anauwezo wa kutembea kwa mguu pasipo kuchukua usafiri. Kumaanisha Mtibeli lazima aishi maeneo yenye huduma za msingi za kijamii.
10. Mtoto wa miaka kuanzia 10 -14 umri wa kubalehe na kupevuka. Atakuwa anaachiwa huru kidogokidogo bila usimamizi wa wazazi wake
11. Hapo tayari awe amefundishwa njia ya kuchagua marafiki Wazuri kulingana na umri wake, malengo yake, tabia, hadhi na heshima ya familia ya Kitibeli.
12. Umri 14- 20 mtoto wa kitibeli anafundishwa ujuzi na taaluma ya kile ambacho ataweza kukifanya akiwa mkubwa. Taaluma au ujuzi huo sharti uzingatie utu wa mtoto kulingana na jinsia yake, maadili ya Kitibeli, na uelekeo wa dunia.
13. Umri wa miaka 17-24 binti wa kike wa kitibeli anatakiwa awe ameolewa.
Wakati kijana WA miaka 24-30 anatakiwa awe ameshaoa.
14. Kijana wa miaka 30 na binti wa miaka 25 wanaruhusiwa kuchukua nyadhifa za serikalini kuongoza jamii zao iwe kwa kiwango cha kata, wilaya, mkoa au ukanda.
15. Binti au kijana wa Tibeli mwenye umri chini ya miaka 40 hatatakiwa kuwa final say katika maamuzi ya nchi au dunia.
Kumaanisha hata awe na sifa za malaika kama yupo below 40 yrs hatatakiwa kuongoza nchi au kufanya maamuzi makubwa ya kitaifa.
Kufikia hapo sina la ziada
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam