Kwa Stand Up Comedy Joti ni Bora 1000 times Mc Pilipili ambaye analazimisha fani

Aisee... Tumeumbwa tofauti... Mimi binafsi huwa namwona anafanya tu mambo ya kipuuzi na kitoto... Nmeshindwa mara zote kuchekeshwa naye namwona tu kwa kuwa ndo ajira yake anajilazimisha aimudu.

Kwa wewe sikulamu ndege wa rangi moja huruka pamoja.


 
Ungeelewa ningeshangaa na kuhisi sasa nami naanza kupoteza uwezo wangu mzuri wa kufikiri. Hili bandiko si level yako acha wengine wanaelewa. Wewe utapata wa akili yako

Ivi ulitaka kusemaje manake hata sijakuelewa!!!
 
Naunga mkono hoja aisee!Jot angefanya Stand Up Comedy angetisha sana Alf ana maneno hatari........Mc Pilipili analiazimisha tu...

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Joti stand up comedy hawezi yule yuko vizuri kwenye vichekesho vinavyoandaliwa kibongo bongo Mpoki ndio anaiwezea hiyo kitu.

-Ndumilakuwili-
 
Nakubaliana na wewe ila ukimfuatilia Mpoki ni zaid ya wote hao nakumbuka alimtoa machozi Rais mstaafu Jk kwa kucheka ktk kinondoni Talent show..
Ivi ulitaka kusemaje manake hata sijakuelewa!!!


Post sent using JamiiForums mobile app
 
Ghaaa. Jamani joti kiboko ya uchafu. Yaani huwa nacheka mpaka machozi yananitokaga
 
mwanaume anapaka wanja!!??? what a fool!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Joti hawezi standup. Angekua ashafanya zamaani. Maigizo si sawa na mubashara.

Pilipili hana kipaji kikubwa. Lakini nani mwingine? Kwahiyo watu wanakula kilichopo. Bora kikipatikana utaona tu mwenyewe.

Kwanza bongo uwanda wa wechekeshaji mubashara baaaaado sana kukua. Ndo umeanza. Kwahiyo watatoka tu shimoni wote.

Pilipili kaenda hadi marekani kuchekesha leo we ni nani useme hawezi standup comedy? Useme tu kipaji chake sio kikubwa sana na hayuko natural kwenye flow ya uchekeshaji. Mada zake zingine zinaboa hapohapo ila nae mjanja kubadili upepo anaweka kile mlichozoea kucheka nacho
 
Aisee... Tumeumbwa tofauti... Mimi binafsi huwa namwona anafanya tu mambo ya kipuuzi na kitoto... Nmeshindwa mara zote kuchekeshwa naye namwona tu kwa kuwa ndo ajira yake anajilazimisha aimudu.

Kwa wewe sikulamu ndege wa rangi moja huruka pamoja.
Una akili nyingi na kwahyo unataka uchkeshwe ki akili nyingi,Sawa genious subiri uchekeshwe na Dr magufuli,vichekesho vingi huwa vina mambo ambayo hayapo serious na Mara nyingi ni mambo ya kijingajinga tu na kwahyo akili yako lazma ihame kutoka ktk mambo serious Kuja ktk kupokea hata vitu vya kijinga ili ucheke na akili irelax na hyo ndio inaitwa sense of humour,hata hvyo sio lazma kila mchekeshaji akuchekeshe hata mm huwa sifurahishwi na mtu anaitwa mkali wenu hata afanye nn.
 
kuna mc pilipili na yule aliyeshindaga B.B.A wanalazimisha kuchekesha wakati vipaji hawana.....watafute vya kufanya
 
Na mimi nakushauri mzee jitahidi kupambana na hali yako

Post sent using JamiiForums mobile app
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kahhh....nimecheka sana

Post sent using JamiiForums mobile app
 
mtoa uzi unamwandama sana mc pilipili. amekuchukulia demu nn

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mtendee haki Joti angalau wachekeshaji tulionao Tz na yeye yumo!

Kwa viwango vyetu jamaa anachekesha ila akitoka nje ya Tz ajiona bado sana!

Sio kila mchekeshaji anaweza kufanya standup comedy mkuu. Standup comedy is an art withing an art.
 
Kuenda marekan kwa mwaliko ukaunganisha hko huko wala si issue. Mi nmeenda marekan zaidi ya mara 3 wala si issue. Pilpil ni mpuuzi mwenye mambo ya kitoto ambayo wa aina yake wanaona anachekesha but kiuhalisia hana anachochekesha analazimisha sana....kama siku ya eid ndo alidhirisha kuwa hamna kitu ni mpuuzi tu kuja kusimulia safar ya marekani. Hakuwa akichekesha...kama alivyokuwa mwenzie mau... Hovyo kabisa.

Mi siku mc pilpili akinichekesha ntatembea uchi au ntaomba mods wanipige ban ya week nzima


 
Umeshasema anachekesha wa aina yake. Pilipili usioila yakuwashia nini? Wewe sio wa aina yake. Ama pengine huna bandama. Ndo maana huwezi kuchekeshwa nae.

Binafsi Joti Pilipili na Mau wote hawanichekeshi. Hawako original. Lakini siwezi sema ni wabaya. Kuna watu wanachekeshwa na yule wa insta anaepaka mikorogo. Sabutoke sjui. Kila kitu na mahali pake na watu wake.

Huwezi amini kuna watu wanaamini Magu anafanya vizuri. Hao ndo wananichekeshaga kuliko Sabutoke na miwanja yake kama nya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…