Kwa story za kuchangamsha genge tunaikaribia Kenya lakini kiuhalisia tumepigwa kanzu, Tulichowazidi labda ni muziki na mpira

Mtoa mada angefanya research ya kutembelea border zetu tulizopakana na kenya ili ajionee bidhaa za TZ zinazoenda kenya na za kenya zinazokuja TZ,bidhaa za TZ unaweza kukuta zaidi ya trucks 50 zinaingiza mahindi,vitunguu n.k kenya,halafu kivan ki1 toka kenya kinaleta cofta na panadol TZ,shida ipo kwa serikali na tbs yake wapo local sana kwenye masuala ya takwimu
Achana na bidhaa za macho, tu ataka data😁😁😁
 
Balance of trade - Thamani ya pesa ya bidhaa zinazonunuliwa kutoka Kenya ni kubwa kuliko bidhaa za Tanzania zinazouzwa Kenya, Kwa upeo mdogo wa kielimu watanzania wengi tumekomalia kwenye kuwauzia Mahindi lakini ukichunguza vizuri hapa kwetu kuna bidhaa nyingi sana za Kenya kuanzia kiwi, Viberiti, sabuni, mafuta ya mwilini, Blueband, pipi na mahitaji mengi sana.

View attachment 3179900

Uwekezaji - Wakenya wengi wamefanya uwekezaji Tanzania wanakula mema ya rasilimali zetu, misituni wamejaa wanachanja mbao wanauza ulaya, Soko la maparachichi Kenya ni kinara kwa kuuza China na ulaya lakini ukichunguza ni wakenya wenye mashamba hapa Tanzania pamoja na madalali wanaonunua kwa bei chee sana wanaenda kuuza kwabeighali masoko ya kimataifa, Benki za Kenya zina share nzuri kwenye banking industry ya Tanzania mfano Equity Bank, ukija kwenye madini mengi yanasafirishwa Kenya kuuzwa, Kinara wa kuuza Tanzanite amewahi kuwa Kenya.

View attachment 3179901
View attachment 3179902

Diaspora - Kuna wakenya wengi sana Marekani, Ulaya, Asia, n.k. Lugha huwarahisishia kwenda majuu, ukiongeza na kupenda elimu kumesaidia wengi kupata kazi nzuri kama madaktari, wanasheria, maprofesa, n.k. Nyuma ya wanigeria na waghana, wanaofuatia kwenye black diaspora waliofanikiwa zaidi ni wakenya, Kuna wakenya kibao mitandao ya kijamii wana fundisha wenzao jinsi ya kwenda nje, Hapa bongo ukiingia tiktok ni comedy

View attachment 3179913

Uwekezaji kutoka makampuni ya Nje - Kampuni kibao za nje zimeweka vianda Kenya kwa kuzingatia factors nyingi ikiwemo population kubwa iliyo elimika kwenye taaluma kibao, kitu kingine ni wepesi wa kuelewana kwa Lugha , Mazingira rafiki ya uwekezaji, n.k. kuna kampuni nyingi sana za ulaya zime invest Kenya.

View attachment 3179924

Elimu - Wapo mbali mno, Ukiangalia hata mahojiano kwenye maandamano ya Gen Z ungeweza kuona jinsi walivyoelimika, Kwenye mashindano kadhaa mfano kulikuwa na Airtel University Challenge wakenya walitukimbiza mpaka unatamani kuzima TV, , Ukienda mitandao ya kijamii wanaweka comments zilizoshiba points tofauti na sisi watu wanagombania likes, Hizi shule za english medium ambazo wenye uwezo hulipia watoto kusoma waasisi wakuu ni walimu kutoka Kenya.

View attachment 3179919

Lugha - Hapa tumepitwa mbali sana, Watanzania wengi mpaka Phd za Udsm lugha ni Tatizo, Lugha unayosomea kuanzia sekondari mpaka Phd inakupiga chenga utaishia kukariri vingi darasani ndio sababu ya elimu yetu kuwa poor, Watanzania wakifika ulaya au Marekani huwa ni wa kuonewa huruma vile lugha huwapa shida, Lugha inakufungulia ulimwengu kwa kiasi kikubwa sana, huwezi kuchukulia poa Language which is a means of communication.

View attachment 3179920

Ajira -Tatizo la ajira ndani ya nchi wameanza kutumia advantage walizonazo, Waziri wa ajira Kenya, Mr Alfred Mutua anapambana kila kukicha kuwatafutia wakenya ajira nhe ya nchi, Account yake ya Facebook imejaa post za nafasi za Kazi kwa Wakenya, Kenya imeweza kutengeneza mazingira mazuri kwa wawekezaji kutoka Ulaya, Marekani, n.k, kufungua makampuni huku wakenye wakifaidika na ajira, Mwaka huu Ujerumani imeingia makubaliano ya kuchukau wakenya laki 2 na nusu kwenye kazi za kitaaluma na zisizo za kitaaluma, Ukienda nchi za nje walimu wengi wa Kiswahili ni wakenya.

View attachment 3179926
Sasa kaitembelee Kenya yenyewe
 
Na huo ndo ukweli wenyewe
 
mtanzania mpe chakula ashibe simba na yanga zishinde hakuna kitu kingine atawaza. zaid ya ngono

Tanzania kuna utegemezi ambao upo above expected line yani kwenye familia pakiwa na mtu mmoja mwenye ajira au uwezo kiuchumi bas atabebeshwa mzigo wa kusaidia ndugu ,na wazazi wote

reflection yake ni aliyesawa kiuchum anaijoin kweny chain ya ufukara indirectly
Inasikitisha sana
 
Mtoa mada angefanya research ya kutembelea border zetu tulizopakana na kenya ili ajionee bidhaa za TZ zinazoenda kenya na za kenya zinazokuja TZ,bidhaa za TZ unaweza kukuta zaidi ya trucks 50 zinaingiza mahindi,vitunguu n.k kenya,halafu kivan ki1 toka kenya kinaleta cofta na panadol TZ,shida ipo kwa serikali na tbs yake wapo local sana kwenye masuala ya takwimu
Kenya wanasafirisha bidhaa zao na ndege zaidi kupeleka Ulaya.
 
Achana na bidhaa za macho, tu ataka data😁😁😁
Tbs wapo kijima,awatoi data while wenzao uwa mpaka wanapika data,TZ waajiriwa wengi awatimizi majukumu ya kikubwa tu mwisho wa mwezi anapokea mshahara wake,mimi si mtaalam wa masuala ya uchumi ila nikiangalia gape la deni la taifa la kwetu na kenya na miradi yetu kama nyerere dam,sgr,brt phase 2,3 na 4 GDP yetu aitakiwi iwepo ilipo sasa
 
Sasa hili kosa la wakenya?
 
Wakenya hawalali usiku kucha wanatafuta fursa sisi usiku kucha tuna bet, miziki, uzinzi, ushirikina, kunywa pombe mbaya zaidi tunaongozwa na watu wajinga haswa
 
Tanzania kuna ujinga mwingi kila mtu ni comedy kila mtu anaimba mziki.upumbavu mtupu

Sasa hivi kila radio ni mipira tu na kubet

Imefikia wakati tuna kampui za kubet nyingi kuliko kuliko vyuo vikuu

Watu wanapenda maisha flani rahisi
Hawataki kuumiza kichwa.
Wabongo tuna roho za kukunja sana
Mtu hata kama ana mchongo ulaya hawezi kukupa details za kueleweka anataka kupata yeye tu

UJinga ni mkubwa sana tanzania na kuna hawa watu ambao hawana faida yoyote hapa nchini lakin bado wanakumbatiwa na wana haribu generation

Kwa mfano hawa wakina MWIJAKU, BABA LEVO NA DOTO MAGARI PAMOJA NA HUYU CHIFU GODLOVE SIJUI KWA NN WAPO URAIANI MPAKA SASA HAWA NI WAPUMBAVU WA MWISHO AMBAO JAMII INAWACHEKEA.

TANZANIA HAKUNA WATU WELEDI KABISA SIMBA VS YANGA

CCM NA CHADEMA ZINATUMALIZA

miaka ijayo tutakuwa nchi ya hovyo kupita maelezo
 
Factors zako ni dhaifu. Ila Ni kweli kwamba uchumi wao ni mkubwa kuliko wa kwetu. Factor kubwa ni mentality au mind set tu. Wao wana mind set ya kibepari, sisi tuna mind set ya kijamaa. Mind set ya kibepari inawatuma wakenya kutafuta mitaji na kujikusanyia mali.

Umejibu tu kwa Sifa za Kihaya, yeye kaleta Ushahidi wa maeneo anayoona wametushinda, wewe umeleta dharau tu na kusema kila kile alichosema
 
Kenya walicho tuzdi..nikuibia rasmal zetu nakuzpachika lebo zao..lakn tukipata raisi mjanja Kenya hawatuwezi kwa chochote ,,labda uhuru wa Katiba yao..
Kunakipindi jiwe aliwavimbia kidogo kuzuia watalii. mbona walfyata mkia wakarudisha mpaka dhahabu na hela zilizoibiwa
 
Very poor perception,
Wakenya wanatuuzia bidhaa ndogo ndogo lakini export yetu nje na around East Africa ni kubwa mno, (Kenya is a small part) Tanzania ina supply in a whole East African countries + drc, mabati , ceiling board, plastic good, coal, cement, tiles na bidhaa zetu huko EA ni hot cake, hii volume huwezi iona endapo upo tu dar na nadharia, kaa boarder uone kazi jinsi tons of cargo zikiondoka, -,mapato ya kutegemeana diaspora haya lakini muhimu kwa kiasi chake!
Sio Perception ni Reality, hivyo vyote unavyovisifia vina kiwango chake ndio maana tumezidiwa kiuchumi,ingekuwa vinaufaidisha sana tungekuwa mbali kuwazidi
 
Urasimu ulikuwa kikwazo sana kwa uwekezaji Tanzania, stay tune, after 3 years!
 
Very poor perception,
Wakenya wanatuuzia bidhaa ndogo ndogo lakini export yetu nje na around East Africa ni kubwa mno, (Kenya is a small part) Tanzania ina supply in a whole East African countries + drc, mabati , ceiling board, plastic good, coal, cement, tiles na bidhaa zetu huko EA ni hot cake, hii volume huwezi iona endapo upo tu dar na nadharia, kaa boarder uone kazi jinsi tons of cargo zikiondoka, -,mapato ya kutegemeana diaspora haya lakini muhimu kwa kiasi chake!
hizo tons of cargo zinasaidia nn labda kama mpaka leo kuna mtu atakufa hospitali kwa kukosa 150k mwingine atazalia njiani kwa kukosa miundombinu ikiwemo barabara na magari ya wagonjwa...... hizo siment mabati yanamsaada gani kwa mwananchi wa kawaida kama kiwanda kitakua hapa kwetu na bado atauziwa mfuko wa simenti 17000
 
Tuna safari ndefu kuifikia Kenya kiuchumi, kitu kimoja tu tunahitaji ni kubadili teaching language kutoka kiswahili kuwa English kuanzia chekechea to university.

Tatizo kubwa lililopo ni akili mgando za watunga sera waliozaliwa kijijini wakati wa ukoloni wasiotaka hilo litokee wakiwa ofisini. Hawa wengi ni wazee na wakifa wote sera itachange na nchi itafunguka, kwasasa tunakosa fursa nyingi toka nje sababu hatuwezi kuwasiliana na mapebari kwa lugha ya malkia.

Otherwise ni kweli kuwa bongo inapiga hatua kwa kasi kimaendeleo kuliko Kenya na SGR ikifika Mwanza na Kigoma na kuanza kubeba mizigo ya nchi jirani itakuwa kiama kwa Kenya ambayo inaelemewa na ufisadi na madeni makubwa ya nje, pamoja na ukabila na fujo za kisiasa.
Sisi pia maden yanakua tup karibia trilioni 99.
 
Back
Top Bottom