Kwa Taarifa Tu: ICC hawaingii hadi majibu ya maswali 5 yafuatayo yatolewe...

Kwa Taarifa Tu: ICC hawaingii hadi majibu ya maswali 5 yafuatayo yatolewe...

Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa wanaokumbuka nilitoa taarifa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana hapa kuwa nilipata nafasi ya kufanya "utalii" pale The Hague Uholanzi. Sikuwahi kufikiria naweza kufika mahali hapo kiutalii na kuweza kujifunza mambo mbalimbali. Matukio ya Oktoba 29-Nov. 4, 2025 yalinifanya nitafute kujipendekeza hapo kidogo. Nilijifunza kidogo jinsi ICC (Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu) inavyofanya kazi hasa kuzingatia kile kilichotokea nchini kwetu wiki chache kabla ya utalii wangu.

Nilileta taarifa hapa kuwa ICC inafanya kazi kwa kuongozwa na Mkataba wa Roma ambao uliunda taasisi hiyo. Tanzania ni mtiaji sahii wa mkataba huo. Baada ya miezi kadhaa kupita watu wamekuwa wakiuliza mbona ICC hawaji, mbona kama wamepuuzia, mbona wako kimya. Kwa uelewa wangu mdogo naomba kupendekeza majibu yafuatayo ili kuwatoa wasiwasi wahanga na waathirika wa vitendo vya umwagikaji damu vilivyotokea kufuatia jaribio la Uchaguzi Mkuu wa 2025.

ICC wameshapata taarifa zote za awali za matukio ya Oktoba 29. Wanazo picha za video, picha mgando, maandishi na ushahidi mwingine wa kidigitali. Picha na video nyingi tulizoziona na ambazo hazikurushwa hadharani zimekusanywa na taasisi hiyo. Hata hivyo hawaji isipokuwa mambo yafuatayo yawe yamekamilika. Mara zote ICC inaingia kwenye nchi na kutoa mashtaka (Indictments) baada tu ya mazingira fulani kukamilika. Kwa Tanzania jambo moja linasubiriwa kwanza kabisa.

Taarifa ya Tume ya Jaji Chande
Ikumbukwe kuwa kwa Tanzania hakuna chombo kingine chochote kilichoundwa na serikali au mamlaka yoyote ya kisheria (ikiwemo Ofisi ya DPP au AG) ambao imeanzisha uchunguzi huru wa matukio yale. Chombo kilichoundwa ni Tume ya Jaji Othman Chande ambayo kama wengi mnavyojua imekuja ikiwa imejaa shuku za kila namna. Baadhi ya mambo ambayo yameulizwa kuhusu Tume hiyo ni pamoja na uhuru wake, wajumbe wake, mamlaka yake na upeo wa mamlaka hayo.

Ili ICC iingie ni lazima ionekane kuwa vyombo vya ndani havijakidhi utaratibu wa kimataifa wa uchunguzi na hivyo kuonekana kuwepo kwa dosari katika uchunguzi wa ndani. Ili ICC ije Tume ya Jaji Chande lazima ishindwe kufanya mambo yafuatayo:

1. Ishindwe Kumtaja/Kuwataja waliohusika na kufanyika mauaji ya Watanzania siku ile. Tume ishindwe kuwataja kwa majina watu hao au kwa nyadhifa zao au vikundi vilivyohusika. Kwa mfano, kule DRC wahusika mbalimbali walitajwa na baadaye kushtakiwa (wapo waliokutwa na hatia na wale waliochaliwa au kufutiwa mashtaka kwenye rufaa). Miiongoni ni watu kama Bosco Ntaganda na Thomas Lubanga.

2. Ishindwe kuwatambua watendaji wa serikali au taasisi nyingine walioagiza au kusimamia matukio yale na kufuata mnyororo wa amri (chain of command) ya utekelezaji wa amri zile. Ni wazi kuwa kuna suala zima la kutumika kwa vyombo vya dola kuzima maandamano yale ya vijana. Tume ya Chande ni lazima ioneshe ni nanni alitoa amri ya kuvunja maandamano kwa risasi badala ya kutumia vyombo vya kawaida vya kuzuia vurugu (kama FFU).

3. Ishindwe kuwahoji viongozi wa juu wa serikali na vyombo vya dola. Hadi hivi sasa (kwa jinsi ninavyojua) hatujaona mahojiano yoyote ya Tume ya Chande na viongozi wajuu wa majeshi, vyombo vya usalama n.k. Lakini pia hatujaona Rais Samia, aliyekuwa Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) na Mawaziri waliosimamia vyombo vya dola (Polisi, Jeshi, na Usalama) wakihojiwa. Mmoja wa waliokuwa mawaziri wakati wa matukio yale (Stergomena Tax) ni mjumbe wa Tume ya Chande. Kushindwa kuhojiwa kwa hawa ni alama ambayo inazua maswali kwa ICC.

4. Ishindwe kupendekeza mashtaka ya jinai kwa wote waliohusika (1-3) hapo juu. Ikumbukwe kuwa tume hii haikupewa madaraka yoyote ya kuleta mashtaka kwa mtu yeyote; yenyewe ni ya uchunguzi tu na baadaye kumpa taarifa Rais (mtu ambaye anaweza kuwa amehusika na mambo ya 1-3). Ikumbukwe kuwa taarifa mbalimbali ambazo zilitolewa na serikali (akiwemo na Rais mwenyewe) baada ya matukio yale zilileta lawama kwa watu mbalimbali na taasisi mbalimbali kuwa zilihusika. Kama hili ni kweli, tutarajie Tume ya Chande kuweka wazi wahusika na hatua gazi zichukuliwe dhidi yao.

5. Ishindwe kujibu baadhi ya maswali ambayo yamekuwepo kabla na baada ya matukio yale ya kutisha yaliyoacha majeraha kwenye fikra na hisia za Watanzania. Baadhi ya maswali hayo ni haya:
- Ni kweli kuna silaha ziliingizwa nchini kabla ya uchaguzi mkuu
- Ni kweli mtoto wa Rais Samia Bw. Abdul anahusika au alihusikaje na matukio ya Oktoba 29
  • Ni kweli vikosi vya mamluki kutoka nje ya nchi (hasa Uganda) viliingia nchini kupitia ziwa Victoria na kuhusika na mauaji au udhibiti wa waandamanaji sehemu yoyote nchini?
  • Je, vikosi vya KMKM kutoka Zanzibar viliingia Tanzania bara na kama vilifanya hivyo, viliingizwa kwa utaratibu gani wa kikatiba au sheria, vilipokuwa bara (kama vilikuwa huko) vilikuwa chini ya mamlaka ya nani?
  • Je, ni watu wangapi waliuawa na kujeruhiwa; miili mingapi imepatikana na mingapi haijapatikana hadi sasa na ile ambao haijapatikana ipo wapi au ilikuwa disposed(kuzikwa) vipi na wapi na kwa utaratibu gani?
  • Je, ni familia ngapi hadi hivi sasa hazijui ndugu zao wako wapi
  • Je, kuna watu wangapi wanashikiliwa mikononi mwa serikali hadi hivi sasa kufuatia matukio yale ya Oktoba 29 na baadaye na wangapi ya hao wamefunguliwa mashtaka mahakamani.

Kwa hiyo mambo haya matano majibu yake ndiyo yataamua ICC ina nafasi gani. Kama majibu yatakayotolewa na Chande na timu yake hayataridhisha mfumo wa ICC ni wazi itaonekana na itafungua ukurasa kwa ICC kuamua kuanzisha mashtaka yake ili watu hao wote waje kutoa majibu mbele ya jamii ya kimataifa. Kutopatikana kwa majibu yoyote ya kuridhisha itakuwa ni ishara ya kutojitosheleza kwa utaratibu wetu wa ndani wa kufanya uchunguzi na hivyo kuhitaji msaada wa Mahakama hii ya Kimataifa.

Kama baada ya ripoti ya Chande tutakachoambiwa ni kuwa "yaliyopita si ndwele tugange yajayo" na kama baada ya ripoti hiyo hakuna mtu yeyote atakayepigwa pingu basi tujue kuwa ICC wataingia kati na kuamua kushughuulikia kilichotushindwa sisi. Suala la muda lisiwatishe au kuwakatisha tamaa watu. Kesi za ICC zinaweza kuchukua muda kidogo na mara nyingi miaka ikibidi. Kwa hiyo, kama alivyosema Komredi Kipepe - Tusubiri Vitu!!
Screenshot_20260516-003803~2.png
 
Nilimaanisha, nini kitafuata baada ya kiroja cha Chande kwa mtazamo wa bandiko lako la kwanza
ICC wanafanya kazi meticulously...sioni namna gani CCM na serikali yake watakudhi matakwabya Rome Statue na hivyo kukwepa pingu. Ninachoona hii tume mpya itajaribu kwenda mbali kuliko ya Chande kwa kuleta indictments...

-- wataleta mashtaka dhidi ya Mange, Maria Sarungi, Twaha Mwaipaya na wale waliokuwa wakihamaisha mitandaoni...wanaweza kutakwa wawe extradited

_ wataleta mashtaka kwa baadhi ya maafisa wa polisi ea ngazi za chini..katika hili nakudokeza juu ya "askari 16" waliouwa wakati wa kuzima maandamano kwa nguvu...

Ila hawatoguswa wanasiasa na kwa hakika hawataleta mashtaka dhidi ya Samia na hapa ndio mlango wa ICC ulipo...bila Samia na viongozi wa juu wa serikali kushtakiwa ICC lazima waingie.
 
Unadhani indictment itakuwa katika ''basis' zipi
_ wataleta mashtaka kwa baadhi ya maafisa wa polisi ea ngazi za chini..katika hili nakudokeza juu ya "askari 16" waliouwa wakati wa kuzima maandamano kwa nguvu...
Polisi kwa modus operandi wanafanya kazi kwa chain of command ! Je itatosha tu kushtaki askari wa kawaida peke yao? Wakubwa katika ''chain'' watakuwa witness dhidi ya hawa wadogo?
Ila hawatoguswa wanasiasa na kwa hakika hawataleta mashtaka dhidi ya Samia na hapa ndio mlango wa ICC ulipo...bila Samia na viongozi wa juu wa serikali kushtakiwa ICC lazima waingie.
Tume hii inawezaje kuwaita Wanasiasa ikiwa inafanya kazi kwa 'blue print' ya Chande!
 
Inachosha sana na mizungushano ya maneno meeengiii; lakini ndiyo hivyo tena!

Huyo mtu wa ICC (mSenegali), aliyekutana na hao waovu; ziara yake ilihusu nini?

Niliishia katikati ya andiko.

Kenya walifanya nini hadi wakaja mapema; pamoja na kwamba hata huko kazi ya hiyo mahakama ilikuwa ya kipuuzi kabisa!

Hawa siyo watu wa kuwategemea kwa lolote. Sasa hivi hata Samia akiitwa hatakwenda. Atawapuuza tu na kuendelea na kazi zake za kuhujumu taifa hili.

Huenda nikarud tena baadaei kuchambua zaidi baadhi ya yaliyoandikwa humu..
Matukio ya Kenya hayafanani na TZ..

Kenya, ilikuwa ni MAKABILA yanapigana yenyewe na kuuana baada ya kuhamasishwa na wanasiasa.

TZ ni vyombo vya Dola ndio vimeua watu.
 
Matukio ya Kenya hayafanani na TZ..

Kenya, ilikuwa ni MAKABILA yanapigana yenyewe na kuuana baada ya kuhamasishwa na wanasiasa.

TZ ni vyombo vya Dola ndio vimeua watu.
Sijaelewa unalenga nini hapa.

Kenya waliuliwa watu. Tanzania wameuliwa watu. Tofauti yake ni huyo aliyehusika katika mauaji?

Wale ma-'warlords' wa DRC waliofikishwa kwenye mahakama hiyo; na wao tofauti yao ni nini?

Kule Liberia, Charles Taylor, alikuwa hatumii dola kuua wa-Liberia?

Au unamaanisha nini hapa?

Huko Kenya, walioitwa na mahakama hiyo; Uhuru Kenyatta na William Ruto waliitwa kama wawakilishi wa makabila yao?
 
Polisi kwa modus operandi wanafanya kazi kwa chain of command ! Je itatosha tu kushtaki askari wa kawaida peke yao? Wakubwa katika ''chain'' watakuwa witness dhidi ya hawa wadogo?
Hii ni 'assumption' au ndiyo kweli; kwamba polisi walihusika katika mauaji.
Kuna ushahidi wowote unaoonyesha uhusika wa polisi kwenye mauaji?

Mara nyingi polisi wanapoamriwa kukabili vurugu, huwa haijifichi kuwa wahusika kweli ni polisi; kwa sababu huonekana rasmi katika mavazi yao na alama mbalimbali kuonyesha kuwa ni polisi; na mara zote huwa kuna taratibu zinazofuatwa katika kutuliza vurugu.

Katika uchunguzi usio rasmi, sijaona dalili zozote zinazoonyesha polisi kuwa sehemu ya wauaji.

Hivi haiwezekani kukawa na kundi lisilo rasmi lililoandaliwa maalum kufanya kazi hii ya mauaji?

Nimeuliza swali hili mara kadhaa humu JF, lakini sijapata jibu la kuniondoa mashaka kwamba Samia hakuwa amejiandaa kivyake kutimiza kazi hii.

Hata kama ni polisi walioamriwa kutokuwa kwenye yunifomu siku hizo ili watimize kazi hiyo; hao bado siyo polisi. Aliyewaandaa alinuia kufanya uovu.
 
Sijaelewa unalenga nini hapa.

Kenya waliuliwa watu. Tanzania wameuliwa watu. Tofauti yake ni huyo aliyehusika katika mauaji?

Wale ma-'warlords' wa DRC waliofikishwa kwenye mahakama hiyo; na wao tofauti yao ni nini?

Kule Liberia, Charles Taylor, alikuwa hatumii dola kuua wa-Liberia?

Au unamaanisha nini hapa?

Huko Kenya, walioitwa na mahakama hiyo; Uhuru Kenyatta na William Ruto waliitwa kama wawakilishi wa makabila yao?
Kama unatumia visungura, punguza au acha kabisa
 
Hii ni 'assumption' au ndiyo kweli; kwamba polisi walihusika katika mauaji.
Kuna ushahidi wowote unaoonyesha uhusika wa polisi kwenye mauaji?

Mara nyingi polisi wanapoamriwa kukabili vurugu, huwa haijifichi kuwa wahusika kweli ni polisi; kwa sababu huonekana rasmi katika mavazi yao na alama mbalimbali kuonyesha kuwa ni polisi; na mara zote huwa kuna taratibu zinazofuatwa katika kutuliza vurugu.

Katika uchunguzi usio rasmi, sijaona dalili zozote zinazoonyesha polisi kuwa sehemu ya wauaji.

Hivi haiwezekani kukawa na kundi lisilo rasmi lililoandaliwa maalum kufanya kazi hii ya mauaji?

Nimeuliza swali hili mara kadhaa humu JF, lakini sijapata jibu la kuniondoa mashaka kwamba Samia hakuwa amejiandaa kivyake kutimiza kazi hii.

Hata kama ni polisi walioamriwa kutokuwa kwenye yunifomu siku hizo ili watimize kazi hiyo; hao bado siyo polisi. Aliyewaandaa alinuia kufanya uovu.
Chombo chenye mamlaka ya Usalama na Mali za Raia ni Jeshi la Polisi chini ya Waziri wa mambo ya ndani

Polisi hawajakanusha tuhuma za Uhusika. Chande haijatambua kundi jingine lililofanya mauaji

Polisi hawajafanya uchunguzi wa nani alitenda hayo.Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilipongezwa kwa kazi nzuri
Hakuna kiongozi kutoka vyombo vya Ulinzi, Usalama, Chama Tawala na Serikali vilivyotaja uwepo wa kundi jingine

Kwavile Usalama wa Raia na mali zao ni jukumu la Polisi, wao wanadhima ya kukanusha kuhusika, pili kutueleza wahusika ni nani. Ikiwa hawafanyi hivyo, dhima ya Usalama wa Raia ipo mikononi mwao na haya mauaji watakwepa vipi?
 
Hakuna hata moja nisilokubaliana nalo hapa.
Kwamba "haijulikani" ni kundi lipi lilihusika katika mauaji. "Chande hajatambua kundi (jingine/lolote) lililofanya mauaji.

Polisi kutolitolea taarifa haimaanishi wao ni wahusika.
Na kama nilivyoeleza hapo juu, kama baadae watabainika kuwa sehemu ya wahusika wa mauaji; tendo lao la kutokuwa katika mavazi rasmi ni njama za kufanya uhalifu.
Aliyepanga iwe hivyo itabidi ajibu tuhuma kwa nini aliandaa kundi la uhalifu nje ya taratibu za kulinda usalama.
 
Back
Top Bottom