Kwa tabia hizi chafu za Viongozi na Mashabiki wa Yanga, TFF wakizinduka tutaadhibiwa

Aliyelalamika ni nani? Hao mashabiki wachache walio jitokeza hapo uwanjani ndiyo ionekane mashabiki wote wa Yanga tunalalimika na kufanya fujo?...
Umeongea kwa hoja. Jinsi ambavyo kila mwanamichezo anapaswa awaze. Mimi kutoa maoni yangu kuhusu wachezaji na benchi la ufundi ni haki yangu. Na haya hayawezi badilisha lolote ambalo team inapanga. Natimiza tu haki yangu ya kikatiba. Kama ambavyo ningesifia ni sawa pia.
 
Nmekutana sana na hizo changamoto admins wengi wa magroup huwa hawana akili, uelewa. Hawawezi hoja wanataka tusifuna kuabudu tu. Ukikosoa unaitwa mamluki.
 
Ni wachezaji wazuri tunawapa muda. Wapo alina Saido (Majeruhi) akina Kisinda ,Mukoko Tonombe, Deusi Kaseke n.k
Ao wachezaji majeruhi awawezi. washatumika sana ndo maana mkapewa kwa bei rahisi,viongozi wenu wamewapa mikataba ya wiki 24 kila mchezaji kwasabau washatumuka sana.

Alafu embu nijuze mkuu,Ntibayonkiza kapata majeraha kwenye mechi ipi?
 
Ao wachezaji majeruhi awawezi. washatumika sana ndo maana mkapewa kwa bei rahisi,viongozi wenu wamewapa mikataba ya wiki 24 kila mchezaji kwasabau washatumuka sana.

Alafu embu nijuze mkuu,Ntibayonkiza kapata majeraha kwenye mechi ipi?


Simba vs Yanga. Au unadhani alipatia majeraha akiwa kitandani?😁
 
Tumeletewa mchezaji kwenye briefcase hatukuruhusiwa kuhoji wala kumfanyia majaribio, tuliambiwa kwa huyu Fiston Messi anamsubiri ....yangu macho...nasubiri miujiza
 
Simba akifungwa au sare mashabiki wa simba wanawalaumu wachezaji wao au benchi la ufundi. Manula, Sven wamelaumiwa sana humu timu inapovurunda. Hii ni faida sana kwa timu.

Ila Yanga mkifungwa au sare mashabiki mnawarushia marefa makopo na kulaumu TFF mkijitahidi sana analaumiwa sarpong ila kocha kwenu mnamuona kama Gurdiola.
 
Ule ndio mpira wenu, pira gwaride makuruta fc, pili kwanini kocha na baadhi ya wachezaji wamfanyie fujo refa kama hamkwenda na matokeo yenu
 
Viongoz yanga acheni kutubadilishia makocha Kama mboga ipo siku mtaingia choo kike,kaze yupo vizuri sana.
 
Timu inayoongozalig yanga
Timu inayoongoza kulalamika yanga
Timu yenye kelel bongo yanga

Kama mtoto wa kambo
 
Bila shaka utakuwa hauna muda mrefu kwenye football mkuu

Last season EPL Liverpool akiwa form alipigwa na Watford ambayo ilikuwa inashuka daraja
 
Kuhusu hilo nenda moja kwa moja kuwa Yanga ndo wanaogomea Nembo ya Mdhamini

Ujinga huo wauko Msimbazi, angalia CAF nembo yao ni kijani na njano mbona Simba wanabandika kwenye mabega ya jezi yao na haibadilishi uhalisia wa timu.

Ukisema mafumbo hawawezi kubadilika waambie wazi wazi kuwa viongozi wa Yanga ni mataahira waache ujima.
 
Bila shaka utakuwa hauna muda mrefu kwenye football mkuu

Last season EPL Liverpool akiwa form alipigwa na Watford ambayo ilikuwa inashuka daraja
Mkuu hayo mamo ya last season ndo unayowezamueleza mtu hakuwepo kwenye soka! nimewashududia mpaka akia Zamoyoi Mogella(Golden Boy), Gagario, Idd Pazy, Suday Juma(Pikipiki), Mambosasa, Said Zimbwe, Kenny Mkapa, Fredy felix Minziro, huko nje kwa EPL na nyinginezo, nikikutajia hata majina ya wachezaji wa enzi hizo hapa Tanzania tulikuwa tunasikiliza mpira kupitia Redio Tanzania (RTD) na kutoka huko majuu tulipata haari za michezo kutoka idhaa ya kiswahili ya Ujerumai Magharibi, hata nikikutajia watangazaji wa mpira maarufu wa enzi hizo sidhani kama unamfahamu hata mmoja!..........Kwa ufupi Yanga punguzeni malalamiko, pale mnaposhindwa jitazameni zaidi katika uthaifu weu a msiwe wepesi wa kutafta visigizio! Ni aibu kwa timu iliyosheheni wachezaji wa kimataifa tena wanaotisha kama akina Kisinda, Tonombe, Surpong, Fiston na wengine lakini mnashindwa kupata matokeo mbele ya timu isiyo na mchezaji wa kulipwa hata mmoja! Alafu mnakimbilia kulaum refa!
 
Kwa hiyo mkuu, Yanga anatakiwa Adroo/kufungwa na team gani VPL?

Au anatakiwa kushinda game 32 kasoro mbili za Simba SC?

Nikukumbushe tu msimu huu mwaka huu huu, United ikiwa na (pogba, Bruno, cavan, rashford etc) alifungwa na Sheffied United ambayo yuko last postion na mpaka anakutana na United alikuwa kashinda game 2 tu
 
Mkuu kuna timu ambazo mkipoteza au kutoa nayo sare unasema hapa tulistahili matokeo haya na kuna timu ambayo ukipata matokeo hayo kwao inabidi wewe mwenyewe ujitathmini upya! Hapo juu nimekupeni ushauri wa bure si kama shabiki wa Simba bali mdau wa soka, Sasa msipoufanyia kazi ushauri wa bure kama huo mkang'ang'ana kutolea mifano ya Ligi za majuu ni sawa na kuhalalisha Yanga ifungwe na timu yoyote hata ya mchangani na bado watu waone ni sawa tuu!
Wazungu wanasema "Two wrongs do not make it wright!".
 
Unadhani aliyekuwa Kocha Wao Luc Eymael ( Mbelgiji ) aliposema kuwa Mashabiki wa Yanga SC ni Nyani, Mbwa na Sokwe alikosea Ndugu? Unachokiona / Kukisikia ndiyo Uthibitisho wake Kamili. Mtu akikuambia Wewe ni Yanga kama uko nae karibu mzabe hata Kofi kwani hapo ni sawa amekutukana na Kukudhalilisha mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…