Kwa takwimu hizi za sensa ya 2022 maisha lazima kilio cha ugumu wa maisha ni jambo lisilo epukika

Kwa takwimu hizi za sensa ya 2022 maisha lazima kilio cha ugumu wa maisha ni jambo lisilo epukika

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
FuJQSxiXgAEZASS

Ukiziangalia takwimu za tume ya takwimu zinatotokana na sensa ya 2022 karibu watanzania 55M ama ni watoto, wako shule, wanatafuta kazi au wamepoteza uwezo wa kufanya kazi wakitegemea nguvu kazi ya 6M. Kwa kuzingatia ufanisi wetu wa uzalishaji uwiano huu matokeo yake ni ugumu wa maisha
 
Hii inchi kutoboa tusahau upumbavu ni mwingi sana itachukua miaka 200 kuanza kuwa serious. Kwasasa ni upumbavu mwingi sana sababu wapumbavu ni wengi kuliko wenye hekima.
 
Hii inchi kutoboa tusahau upumbavu ni mwingi sana itachukua miaka 200 kuanza kuwa serious. Kwasasa ni upumbavu mwingi sana sababu wapumbavu ni wengi kuliko wenye hekima.
Mkuu umechangia au umetukana- please come again
 
Kwa ufupi

Kuanzia miaka 0-35 ni watu Milioni 48, ambao wengi ni wanafunzi, watoto, wasio na kazi etc.

Kuna kundi la kuanzia miaka 60-80
Ni watu Milioni 3.5, ambao ni wastaafu, wazee etc
Hivyo jumla tuna watu Milioni 51.5 ambao hawazalishi

Hawa wengi ni tegemezi.

Jumla ya tegemezi ni Asilimia 84

Hivyo twabakia na watu Milioni 10 pekee ambao wako kwenye kazi

Asilimia 16 pekee ndo yalipa kodi, yafanya kazi kulisha Asilimia 84
 
Ni haki tujiiete taifa changa na tegemezi
 
Yaani 18 -35 hawazalishi??
 
Yaani 18 -35 hawazalishi??
wanazalisha wapi mkuu- wanacheza pool na kutoa huduma kama vile kushiriki kwenye maandamano- lakini kuzalisha kitu wakakiweka sehemu tukione hakuna
 
Yet watu wanaongoza Nchi bila kuwa na Mipango serious
Imagine vyuo vya kati na vya Juu private na puplic vyote Kwa pamoja Kwa kada Moja tuu ya walimu wanadahili Watoto zaidi ya 131,000 na kazi zinazotolewa haziziti 12,000 Kwa mwaka..

Hii ni hatari
 
wanazalisha wapi mkuu- wanacheza pool na kutoa huduma kama vile kushiriki kwenye maandamano- lakini kuzalisha kitu wakakiweka sehemu tukione hakuna

Generalization hii....
Mmeongeza chumvi Sana...
Kwahiyo bodaboda wote ni tegemezi??

Kuna kitu mnaongea lakini chumvi imeizidi uhalisia
 
Hii ni dalili ya Taifa linalokua yaani si la wazee. Hoja ya msingi si makundi hayo, bali walio juu wanaadaa mipango gani kwa makundi hayo ili yanapofikia umri wa kufanya kazi wawe kweli kazini? Utakuta katika kundi la 36 - 64, labda nusu wako kazini lakini asiliomia kubwa ya hiyo nusu ni ufisadi tu. Wengi walio madarakani wanajiangalia wao tu. Sikiliza mjadala wa ajira huko bungeni. Soma ripoti ya CAG
 
Generalization hii....
Mmeongeza chumvi Sana...
Kwahiyo bodaboda wote ni tegemezi??

Kuna kitu mnaongea lakini chumvi imeizidi uhalisia
Mkuu si tegemezi ila hawako kwenye actual physical production- hawa ndio wanataka wali na maharage uuzwe 500 wakiabiwa 1,500 wanasema maisha yamepanda. Hawajui wali unaanzia kwenye jaruba, unakuwa mpunga, halafu mchele. Hawajui ndizi zinalimwa. Hawajui nyama inatopkana na ng'ombe anayechungwa na kutafutiwa maji
 
Mimi sijasema ni tegemezi na mtoa mada asipotoshe asubirie uchambuzi unaendelea wahusika watatoa labour force patterns yetu.
Mkuu kwa kutumia takwimu hizo za wenyewe ninao uwezo wa kuchambua na kukwambia taifa letu ni la watu tegemezi na sipotoshi
 
Back
Top Bottom