Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kwa heka heka za uchaguzi wa chadema iliyogawanyika ngazi ya taifa zinazoendelea, wasomi vijana na wadau wa siasa nchini, wanapata fursa na nafasi muhimu sana ya kujifunza, kuelewa na kufahamu umuhimu wa kua na subra na kutathmini mambo kwa kina na umakini mkubwa kabla ya kufanya maamuzi na kuchukua hatua kuelekea mbele katika utekelezaji wa maamuzi yako, vinginevyo maamuzi yako yanaweza kua ni kujifungia fursa na kuzika ndoto zako mwenyewe.
Lakini pia,
wanasiasa vijana wasomi na wadau wa siasa humu nchini, wanapata fursa ya kipekee sana, kujionea kinagaubaga, mchana kweupe athari za maamuzi ya pupa, tamaa, makelele na mdomo, kwenye mambo muhimu ambayo yanahitaji mahesabu na tathmini ya kina kabla ya kufanya uamuzi.
Uchaguzi huu wa chadema Taifa, ni shule na darasa muhimu sana kwa watu wenye ndoto, matarajio na mipango, mathalani ya kua viongozi wakubwa wa kitaifa na kimataifa. Pamoja na mambo mengine, athari zitakazowakumba baadhi ya wagombea uongozi, zinafaa kutufundisha kuwa watulivu, kutumia hekima na busara kuamua, lakini pia kua sharp sana, katika kuasses faida, matokeo na hasara za uamuzi utakachukua.
Kujinyima fursa kwa uamuzi wa pupa ni sawa na kujidhulumu mwenyewe kwa kujidhuru.
Epuka tamaa na uchu wa madaraka. Usifanye maamuzi kwa hasira. Jihadhari na washauri wabaya.
Chadema inakwenda kupata fursa ya kumpendekeza na kumchagua mgombea urasi na mpeperusha bendera wake urais 2025, ikiwa na umoja wa kiwango cha juu sana licha ya kwamba hatashinda nafasi hiyo ya ukuu wa nchi. Hapatakua na makelele wala mdomo tena chadema 🐒
Mungu Ibariki Tanzania