Kwa Tanzania/Dunia ya leo Katiba kuruhusu Darasa la Saba kuwa Mbunge ni aibu kwa Taifa

Kwa maana ya usomi ni nini????? Mbona watanzania tunataka kuhalalisha ujinga kwa kiasi hiki?????

Usomi wa mtu unatakiwa kuwa nyakati zote na kwenye mazingira yote anayokuwa. Kusema nimuangalie akiwa nje ya siasa hapo sikubaliani na wewe!!! Ifike kipindi watanzania tuwe wakweli ili tuisadie kweli nchi yetu. Haiwezekani mtu akawa msomi wa madegree mengi alafu akawa haonyeshi huo usomi wake kwenye nafasi anazopata alafu tunachukulia poa tu!

Amini maneno yangu, class ya wasomi ya Tanzania ndo watu wajinga zaidi kuliko class ya watu ambao hawajasoma sana
 
Mbunge anayeongoza Jimbo lenye kata 30 anakuwa na elimu ya darasa la Saba, ila afisa mtendaji wa kata anayeongoza kata moja anatakiwa angalau awe na Diploma/
Mtendaji ameajiriwa na halmashauri,mbunge anachaguliwa na wananchi
Hujalazimishwa kumchagua wa Darasa la 7,pigia kura tu mwenye PhD
Kumbuka Mbunge ana uwezo wa kuajiri karibu mwenye Masters akawa na jukumu la kuchambua na kushauri juu ya nyaraka na Mambo mbali mbali
Mwakyembe amenisikitisha sana!
 
Hao maprof wame fanya nini??
 
Ubunge mtu anabidi kuwa na Masters angalau kama walivyo wabunge wengi wa chadema
 
Kitu cha ajabu ni kwamba kigezo moja wapo cha kuwa mbunge ni uwe umemaliza darasa la saba, lakini kwa upande mwingine kigezo cha kuweza kuajiriwa kuwa mfanyakazi wa bunge eg. Janitor lazima uwe umehitimu kidato cha 4.
 
Wasomi wepi hao wanaofaa kuwa wabunge? Wanaokariri mambo ya wazungu kichwani wanaoshindwa hata kuandika vitabu? Wasomi ambao hata utamaduni wetu hawaujui? Wanaohonga walimu chuo kikuu ili wafaulu mitihani? Wasomi gani hao? Walioshindwa hata kutengeneza mfumo mzuri wa elimu, kila mwaka ni kubahatisha tu.

Hawa wasomi ambao wanaotunga sheria eti kijana aliyesomea udaktari kwa miaka saba haruhusiwi kufungua huduma hata sebuleni kwa baba yake, na kumfanya kuwa mzururaji, ila mganga wa kienyeji anaruhusuwa kuendesha huduma na kulaza wagonjwa hata kwenye banda la nyasi. Tena mtuache la saba wala msituchokoze.

Ninyi wasomi ambao mnasema mwalimu wa shule ya msingi awe na digrii wakati hakuna digrii ya shule ya msingi hapa Tanzania inayomuandaa mwalimu kwa shule ya msingi, diploma zenyewe pia ni za sekondari.

Nyinyi mnaoandaa digrii ya sheria lakini mtu akifuzu harusiwi kuwa mwanasheria, yaani anakuwa mtaalamu hewa bila kwenda Tanga. Tena msituchokoze la saba.

Ninyi wasomi ambao hata Hamna faida, jitu linakaa vijiweni miaka nenda rudi linasubiri ajira hata kufuga kuku haliwezi, hΓ ta kuchoma mishkaki hawezi, hata kufanya kazi ya kubrashi viatu hawezi, mnaamini hizi kazi ni za darasa la saba, hawa la saba ndio wakulima, ndiyo wafanya biashara hawa ndiyo awanaokuza mapato ya nchi hawa, sisi la saba ndio tunaoendesha nchi.

Nyinyi wasomi muda faida gani zaidi ya kulamba viatu vya mabosi wenu. Ha ha ha nisameheni la saba na nimeandika ki la saba, nieleweni hivyo hivyo.
 
kudos kaka. nimependa hiyo hoja. ubunge ni kazi kama kazi zingine tena yenyewe ni kazi nyeti ya kutunga sheria na kusimamia serikali. sasa iweje kazi zingine zihitaji wasomi halafu kazi nyeti isihitaji usomi?
 
Na kila mtu anahaki ya kusoma . Standard kuwepo ni muhimu , Kuwa na Mbunge darasa la Saba ni kuendeleza wimbo wa ndio Bungeni,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesema kwa Tanzania. Kwa Tanzania wasomi ni wajinga kuliko watu wasiosoma. Mie kila nikimwangalia na kumsikiliza Kabudi huwa najiuliza hivi nisome PhD ili iweje sasa kama kabudi ana PhD na kajaa ujinga vile????
Mfananishe Kalamaganda Kabugi wa Katiba ya Warioba na huyu mteule, utagundua tatizo ni njaa, sio ujinga.
 
Itakuwa katiba ya kijinga mtu na inayokiuka haki za binadamu mtu ana haki ya kupiga kura nakupigiwa kura pia akitaka .Huwezi tengeneza katiba inayomnyima mtu haki zote mbili
Kila haki ina mipaka na wajibu wake. Hata sheria ya sasa inamnyima mtu asiye na akili timamu kuchagua/kuchaguliwa, inamnyima mtu aliyewahi kufungwa kwa baadhi ya jinai kugombea, inamnyima mtoto (under 18) kugombea/kupiga kura, inamnyima aliye chini ya miaka 41 kugombea urais nk nk.

Kuna tatizo gani tukiweka kigezo cha elimu kwenye ubunge, udiwani na urais ili kuendana na wakati? Kwa miaka ile kama taifa ilikuwa sawa kwa kuwa hatukuwa na wasomi wengi wa kutosha.

Mbona hii ya sasa inamnyima kugombea asiyejua kusoma na kuandika na huoni ni tatizo?
 
Kitendo tu cha yeye kutokuwa na msimamo kuhusu elimu na uelewa wake na kutaka hadi kuaminisha wengine ujinga ili ampendeze aliye mteua, kinatosha kumuondoa kwenye kundi la watu walioelimika na kuwa na maarifa.
 
Je kua na mpiga kura darasa la saba?
Kazi ya mpiga kura ni kuchagua tu, na wagombea wanapewa siku 60 kuongea na wapiga kura kuwaeleza ni kwa nini wawachague. Haihitaji elimu kubwa sana kujua huyu ataniwakilisha vyema kama mambo mengine ya rushwa nk yakidhibitiwa.

Kinyume chake, mbunge anatunga sheria, anaishauri serikali, anajadili na kupitisha miradi mbalimbali, anajadili taarifa za kifedha na kuwasilisha kero za wananchi wake. Haya yote yanahitaji mtu makini na mwenye elimu na maarifa ya kiwango fulani.
 
Usichanganye majukumu tafadhali. Kuwa mwalimu ni zaidi ya kuwa mbunge, mwalimu kazi yake ni kupandikiza kitu kwenye ubongo wa mwanafunzi wake, lazima ajue ni mbinu gani atayotumia kufanikisha hilo na hili hutofautiana kati ya mwanafunzi mmoja na mwingine, wakati mbunge kazi yake ni simple tu, kusikiliza matatizo ya wapiga kura wake na kwenda kuyawasilisha bungeni kwa utatuzi.
 
'Amalinze' wa Bariadi amenisikitisha (au kwa kizungu 'AMENISATYA') sana bajameni!
πŸ˜…
πŸ‘Š ✌✌✌πŸ’₯
 
Mbunge anatekeleza ilani ya chama chake. Hivyo serikali itatekeleza ilani na miongozo ya chama kilichoshika dola.
Mbunge ni msimamizi tu wa serikali ili mambo yaende.
 
Hivi hizo Sheria zinatungwa kwa lugha ya malkia alafu mbunge darasa la Saba hajui ht kutamka 1100 kwa kiswahili... Je hiyo Sheria ataijuaje zaidi tu ya kupitisha pasipo kupinga ili asiulizwe kasoro zilizomo...
Lugha haihitaji madegree.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…