Kwa tuhuma alizonazo Ole Sabaya, anaweza akakimbia nchi, awekwe chini ya ulinzi

Ni mtuhumiwa, lakini kwa usalama wake na haki kutendeka, awekwe chini ya ulinzi...

Mkuu sitegemei huyo mama achukue hati yoyote kwa huyo muhuni. Kumbuka mama ameshaunda tume kuchunguza hela za BOT za januari to March mpaka leo kimya. Kaunda tume ya Covid, mpaka leo kimya. Naona ni muunda tume fulani bila kuchukua hatua, na hofu kutoka kwa wahifidhina ni kuwa anakiumiza chama kama atakchukua hatua.
 
Big up!

Umenena vyema mno!
 
Unaongea kitu ambacho kinaendeshwa na mihemko,nchi kama nchi hua ina taratibu zake za kufuatwa pale mtu anapotuhumiwa jambo.
Yeye Sabaya mbona alikuwa hafuati hizo sheria?

Sometimes,majambazi ya kisiasa kama Sabaya yanatakiwa kushughulikiwa kwa utaratibu wa ' mob justice'
 
You are very correct, anaogpa reaction ya chama chake. Lakini anaweza ku gain courage akatenda haki. Kibaya ni kumuonea mtu! As long s CDF yuko upande wake, anaweza kuthubutu!
 
Yeye Sabaya mbona alikuwa hafuati hizo sheria?

Sometimes,majambazi ya kisiasa kama Sabaya yanatakiwa kushughulikiwa kwa utaratibu wa ' mob justice'
Kosa moja halihalalishi kosa lingine,kama alikua hafuati sheria kama unavyodai na kama upo sahihi basi vyombo vinavyohusika ndio vilaumiwe,

Mob justice unaiongea bila kujua uhatari wake,

Mfano wewe huenda kuna watu wanakuchukia bila wewe kujijua,wanaweza siku moja wakapanga na kukupigia kelele za "Mwiziii" kisha wakakumaliza na kwa vile utakua haupo hai tena hutoweza kujitetea na kila mtu atashangaa na kuamini kua kumbe ulikuaga Mwizi!

Ndio maana kesi huamuliwa na Court of law with vivid evidence.
 
Malipizi ya dhambi ya uchafuzi wa 28/10. Na bado; wengi watalipa. Kinara alishakwisha lipa.
 
why wakuchukie?
Nimetolea mfano jaribu kua muelewa,na ndio maana nikasema huenda kuna watu wanakuchukia bila wewe kujijua,

Halafu tambua kwamba kila binadamu lazima atakua na haters hata kama utaishi kama Malaika,hakuna Binadamu aliyependwa na wote na akachukiwa na wote,hata Mitume wa Mwenyezi Mungu na walichukiwa na wengine kuteswa,

Hapa Duniani ukiwa huna haters basi tambua kwamba you are doing nothing.
 
Ndio maana naona maridhiano yale ni ya pata potea.

Huyu mtu ushahidi wa matukio yake ulikuwepo kidijitali kabisa ila saa hizi mpo nae mtaani huko.

Na soon naye anarudishwa ofisini kama Daudi zero
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…