KWA TULIOWAHI KUTAITIWA NA VIBAKA NA MAJAMBAZI TUKUTANE HAPA.

KWA TULIOWAHI KUTAITIWA NA VIBAKA NA MAJAMBAZI TUKUTANE HAPA.

Mwaka 2005 nakumbuka kombe la dunia lilitembelea tanzania pale diamond jubilee wakat huo nipo chuo mwaka wa kwanza nikaenda na demu wangu Irene tulipotoka pale tukaenda beach maeneo ya aga khan basi giza linaanza kuzama hivi nashtuka tumezungukwa na watu kama 8 wana mapanga wakachukua simu pochi cheni...nilichezea kichapo maana nlitaka kujifanya mm komando joni nipambane kama sio mpenzi wangu kuwaomba wanisamehe wangenitoa jicho.


Tokea mwaka huo ile beach naichukia sn
pole mkuu,kule kigiza kikiingia tu ndio zao.
 
Stori yangu ni tofauti kidogo. Kipindi nimeenda kuwatembelea wazazi Mwanza (2011).....kuna jamaa wa kitaa waliniona jioni nazunguka na wengine walionifahamu wakanisalimia na kutaka kujuwa nilifika lini mjini. Usiku wazazi wamelala nasikia mbwa wanabwaka, ile kuchungulia dirishani naona kuna jamaa anakimbia uwani na mkuki akifukuza mbwa na mmoja wao kafa kwa kulishwa sumu. Nikamwamsha Mze taratibu huku tukimuambia Mama na ndugu wengine wanyamaze. Mze akachukua bunduki yake nami yangu, Mze akapanda juu nami nikawa chini maeneo ya jikoni waliko majambazi (4) na kutaka kubomoa mlango wa nyuma. Wale jamaa walikuja na mtungi wa gesi kuchoma geti la mlango, mbwa wakawa bize kuwakalipia na hii ndiyo ilikuwa hukumu yao. Huku wakipigana na mbwa mimi na Mze tulipanga strategy ya kuwaua. Mze akamlipua mmoja wao nami nikamlipua mwingine huku nikimjeruhi yule aliyebeba mtungi wa gesi ila mbwa ndiyo walimla vibaya sana, yaani walimchana nyama za usoni na kuirarua mboo yake. Matokeo yake, tuliua majambazi wawili pae Ilemela, Zoo. Sina huruma na kibaka hata jambazi.....Kaba, tukabane au ua ukiniwahi, nikuue.
 
Ilinitokea siku moja kipindi nipo form six maendo ya buguruni. Jamaa walinibanisha mida ya saa nane usiku wakanichomoa kama 12000 hivi.
 
Waliwahi kunifanyia "ambush" walikuwa kama sita hivi sasa kwa kuwa sikuwa nimejianda na sikujua hili wala lile walifanikisha azma yao!
But nilitafakari sana lile tukio hivyo nikaamua kutafuta mbinu ya kupambana nao wakati mwingine, hivyo nilipata mbinu ya kupambana nao kulingana na mazingira tofauti tofauti, aina ya vibaka, idadi ya vibaka na aina ya silaha wanazotumia!
Siku wakaingia katika mtego, kwa kweli nadhani huko waliko kama wanakumbuka hilo tukio nahisi watakuwa wanadhani walipambana na jini!
Kaka naomba unitonye mbinu ulio tumia wakanasa mtegoni..!!
 
Uzi mtamu sana huu[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Stori yangu ni tofauti kidogo. Kipindi nimeenda kuwatembelea wazazi Mwanza (2011).....kuna jamaa wa kitaa waliniona jioni nazunguka na wengine walionifahamu wakanisalimia na kutaka kujuwa nilifika lini mjini. Usiku wazazi wamelala nasikia mbwa wanabwaka, ile kuchungulia dirishani naona kuna jamaa anakimbia uwani na mkuki akifukuza mbwa na mmoja wao kafa kwa kulishwa sumu. Nikamwamsha Mze taratibu huku tukimuambia Mama na ndugu wengine wanyamaze. Mze akachukua bunduki yake nami yangu, Mze akapanda juu nami nikawa chini maeneo ya jikoni waliko majambazi (4) na kutaka kubomoa mlango wa nyuma. Wale jamaa walikuja na mtungi wa gesi kuchoma geti la mlango, mbwa wakawa bize kuwakalipia na hii ndiyo ilikuwa hukumu yao. Huku wakipigana na mbwa mimi na Mze tulipanga strategy ya kuwaua. Mze akamlipua mmoja wao nami nikamlipua mwingine huku nikimjeruhi yule aliyebeba mtungi wa gesi ila mbwa ndiyo walimla vibaya sana, yaani walimchana nyama za usoni na kuirarua **** yake. Matokeo yake, tuliua majambazi wawili pae Ilemela, Zoo. Sina huruma na kibaka hata jambazi.....Kaba, tukabane au ua ukiniwahi, nikuue.
Nimekuelewa sana mkuu Mbishi, hongera sana
 
Mwaka 2005 nakumbuka kombe la dunia lilitembelea tanzania pale diamond jubilee wakat huo nipo chuo mwaka wa kwanza nikaenda na demu wangu Irene tulipotoka pale tukaenda beach maeneo ya aga khan basi giza linaanza kuzama hivi nashtuka tumezungukwa na watu kama 8 wana mapanga wakachukua simu pochi cheni...nilichezea kichapo maana nlitaka kujifanya mm komando joni nipambane kama sio mpenzi wangu kuwaomba wanisamehe wangenitoa jicho.


Tokea mwaka huo ile beach naichukia sn
Hahahaaaaa hapo in hatari
 
Tryin to imagine, huwa unawaambia "shikamoo kaka kibaka, naweza nikapita hapa?"...
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji23] [emoji23] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Mwaka jana nlikua natembea beach flan iv niko mtoto wa kike flan iv, ile beach kwa mbele kuna msitu mkubwa wa hifadh ya jeshi basi tukawa tunatembea ufukwen ktk ule msitu ghafla zilitoka njemba tatu zina njaa ajabu ndan ya ule msitu yan azielew kbsb somo jamaa walikomaa sana na mimi kwa kunitisha nikae chini kiukwel walishaona simu 2 na mifuko imetuna asa wanataka nikae wanivamie nikiwa nimekaa nkawasoma mbinu yao nikaanza kuwapiga siasa nyingi nilitumia mbinu haswa kucheza na hisia zao sio siri wakuu siku zote kwenye hatar busara na utulivu ni kitu chema yan nliongea nao kwa akili mwishowe nliwapa 5000 na wakajikuta wanapiga stor na kutusindikiza ad kwenye beach niliyokuwa.
 
Tryin to imagine, huwa unawaambia "shikamoo kaka kibaka, naweza nikapita hapa?"...
hahaha kuna salamu zao anga hizo unasema kaka vipi kwemaa?? akijibu kwema sista unawaambia naona mnakula upepo mi napitaa lol kwangu inafanyaga kazi ila kwa wanaume sijuii
long time no see.......
 
hahaha kuna salamu zao anga hizo unasema kaka vipi kwemaa?? akijibu kwema sista unawaambia naona mnakula upepo mi napitaa lol kwangu inafanyaga kazi ila kwa wanaume sijuii
long time no see.......
Hahah!!!

Long time no see dooh!!! btw nipo mzima rafiki bila shaka nawe pia...
 
Imewahi kunitokea, nakumbuka vizuri sana nilikuwa natoka kwenye mishe mishe zangu, nilifika mahali ambapo zinapita bodaboda nyingi na watu wachache tu wanaotembea kwa miguu. Nilikuwa nina simu 2; moja ya touch nyingine ya Nokia ilikuwa ndogo na kiasi cha Tsh 7000 mfukoni pamoja na chaji ya smartphone.

Nakumbuka wakati natembea taratibu kwa maringo kama Twiga, simu yangu ya touch ikaingia massage ya WhatsApp, nikaiotoa ili kuisoma aisee ile message na ule mwanga wa simu viliniponza kabla hata sijafika mbali nilishtuka nimepigwa roba moja kali sana mpaka nikahisi pumzi inataka, nikajua enhe hapa tayari nimekabwa na wahuni. Usiombe kukutana na hao wajinga hawaoni shida kutoa uhai wako. Ile distance ya kutoka zinapopita bodaboda na tulipokuwa sisi ilikuwa ni hatua chache sana ingawa kiza kilikuwa kikubwa. Nashukuru hawakunichana hata na kiwembe japo nilijitahidi kuwazuia walinishinda power nilichezea tu ngumi za uso wakaondoka na simu yangu ya touch.
 
Sio mbali, jana tena tukio kama hilo kidogo linitokee kama sio kuwa makini ingekula kwangu. Nilikuwa natoka Kunduchi nakwenda nyumbani Salasala; mapema tu saa 2 usiku nikasema leo sipandi bodaboda wala bajaji -- leo natembea taratibu kwa miguu mpaka nyumbani.

Safari ikaanza, nikatembea ikabaki kipande kidogo tu niingie mitaa ya home ila kuna mtaa mmoja ndio huwa njia yangu ya miguu siku zote japo mazingira yake sio mazuri kuna miti na vichaka vingi. Nilipofika hapo nikawaona watu watatu wamesimama katikati ya njia kama walikuwa wanajadili kitu hivi, nikawasoma nikajua kabisa hawa sio watu wazuri nikasita kuendelea na safari, pembeni yangu kulikuwa na nyumba ina duka nikaona yes ngoja nipoteze lengo nikaulizie vocha... Nimekwenda mpaka dukani kujifanya nataka vocha, nikajibiwa zipo za Halotel na Tigo... Nikasema basi mimi nilikuwa nahitaji ya Vodacom...
 
Back
Top Bottom