Stori yangu ni tofauti kidogo. Kipindi nimeenda kuwatembelea wazazi Mwanza (2011).....kuna jamaa wa kitaa waliniona jioni nazunguka na wengine walionifahamu wakanisalimia na kutaka kujuwa nilifika lini mjini. Usiku wazazi wamelala nasikia mbwa wanabwaka, ile kuchungulia dirishani naona kuna jamaa anakimbia uwani na mkuki akifukuza mbwa na mmoja wao kafa kwa kulishwa sumu. Nikamwamsha Mze taratibu huku tukimuambia Mama na ndugu wengine wanyamaze. Mze akachukua bunduki yake nami yangu, Mze akapanda juu nami nikawa chini maeneo ya jikoni waliko majambazi (4) na kutaka kubomoa mlango wa nyuma. Wale jamaa walikuja na mtungi wa gesi kuchoma geti la mlango, mbwa wakawa bize kuwakalipia na hii ndiyo ilikuwa hukumu yao. Huku wakipigana na mbwa mimi na Mze tulipanga strategy ya kuwaua. Mze akamlipua mmoja wao nami nikamlipua mwingine huku nikimjeruhi yule aliyebeba mtungi wa gesi ila mbwa ndiyo walimla vibaya sana, yaani walimchana nyama za usoni na kuirarua **** yake. Matokeo yake, tuliua majambazi wawili pae Ilemela, Zoo. Sina huruma na kibaka hata jambazi.....Kaba, tukabane au ua ukiniwahi, nikuue.