Kirikou Wa Kwanza
JF-Expert Member
- May 24, 2013
- 3,564
- 1,991
Sio mbali, jana tena tukio kama hilo kidogo linitokee kama sio kuwa makini ingekula kwangu. Nilikuwa natoka Kunduchi nakwenda nyumbani Salasala; mapema tu saa 2 usiku nikasema leo sipandi bodaboda wala bajaji -- leo natembea taratibu kwa miguu mpaka nyumbani.
Safari ikaanza, nikatembea ikabaki kipande kidogo tu niingie mitaa ya home ila kuna mtaa mmoja ndio huwa njia yangu ya miguu siku zote japo mazingira yake sio mazuri kuna miti na vichaka vingi. Nilipofika hapo nikawaona watu watatu wamesimama katikati ya njia kama walikuwa wanajadili kitu hivi, nikawasoma nikajua kabisa hawa sio watu wazuri nikasita kuendelea na safari, pembeni yangu kulikuwa na nyumba ina duka nikaona yes ngoja nipoteze lengo nikaulizie vocha... Nimekwenda mpaka dukani kujifanya nataka vocha, nikajibiwa zipo za Halotel na Tigo... Nikasema basi mimi nilikuwa nahitaji ya Vodacom...
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] dawa yao ni kutembea na bastola tuuImewahi kunitokea, nakumbuka vizuri sana nilikuwa natoka kwenye mishe mishe zangu, nilifika mahali ambapo zinapita bodaboda nyingi na watu wachache tu wanaotembea kwa miguu. Nilikuwa nina simu 2; moja ya touch nyingine ya Nokia ilikuwa ndogo na kiasi cha Tsh 7000 mfukoni pamoja na chaji ya smartphone.
Nakumbuka wakati natembea taratibu kwa maringo kama Twiga, simu yangu ya touch ikaingia massage ya WhatsApp, nikaiotoa ili kuisoma aisee ile message na ule mwanga wa simu viliniponza kabla hata sijafika mbali nilishtuka nimepigwa roba moja kali sana mpaka nikahisi pumzi inataka, nikajua enhe hapa tayari nimekabwa na wahuni. Usiombe kukutana na hao wajinga hawaoni shida kutoa uhai wako. Ile distance ya kutoka zinapopita bodaboda na tulipokuwa sisi ilikuwa ni hatua chache sana ingawa kiza kilikuwa kikubwa. Nashukuru hawakunichana hata na kiwembe japo nilijitahidi kuwazuia walinishinda power nilichezea tu ngumi za uso wakaondoka na simu yangu ya touch.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Nikaondoka dukani, lakini nilipowaangalia wale jamaa nikawaona bado wamesimama pale njiani, nikasema sipiti tena hapo ilikuwa njia panda nikabadili njia nikaona bora nizunguke tu. Taratibu nikiwa natembea kwa tahadhali kabla sijafika hata mbali nikageuka nyuma nikamuona mtu ananifuata, nikamuangalia kama sek. 5 hivi nikaangalia upande wa juu nikaona jamaa wawili wanakimbia kuniwahi kama wanataka kuni over take, nikajua enhe kazi imeanza ila leo hawanipati... Mzee nikala kona kwenye kichaka kikatoka nduki mpaka yalipo makazi ya watu nikarudi mpaka barabara kuu nikasema hapa nipo salama, nikamshukuru sana Mungu.
Kuna mjeshi alikabwa mpaka akavunjwa bega siku ya mechi ya simba uwanja wa taifa wakaja wajeda watu walikula kichapo sanaNatamani hao wajinga waingie ktk mikono ya polisi/mjeshi alie valia kiraia.
imesomeka!!
Buguruni sehemu gani?Ilinitokea siku moja kipindi nipo form six maendo ya buguruni. Jamaa walinibanisha mida ya saa nane usiku wakanichomoa kama 12000 hivi.
Ukawalipua ki- black American kama wanugu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Stori yangu ni tofauti kidogo. Kipindi nimeenda kuwatembelea wazazi Mwanza (2011).....kuna jamaa wa kitaa waliniona jioni nazunguka na wengine walionifahamu wakanisalimia na kutaka kujuwa nilifika lini mjini. Usiku wazazi wamelala nasikia mbwa wanabwaka, ile kuchungulia dirishani naona kuna jamaa anakimbia uwani na mkuki akifukuza mbwa na mmoja wao kafa kwa kulishwa sumu. Nikamwamsha Mze taratibu huku tukimuambia Mama na ndugu wengine wanyamaze. Mze akachukua bunduki yake nami yangu, Mze akapanda juu nami nikawa chini maeneo ya jikoni waliko majambazi (4) na kutaka kubomoa mlango wa nyuma. Wale jamaa walikuja na mtungi wa gesi kuchoma geti la mlango, mbwa wakawa bize kuwakalipia na hii ndiyo ilikuwa hukumu yao. Huku wakipigana na mbwa mimi na Mze tulipanga strategy ya kuwaua. Mze akamlipua mmoja wao nami nikamlipua mwingine huku nikimjeruhi yule aliyebeba mtungi wa gesi ila mbwa ndiyo walimla vibaya sana, yaani walimchana nyama za usoni na kuirarua **** yake. Matokeo yake, tuliua majambazi wawili pae Ilemela, Zoo. Sina huruma na kibaka hata jambazi.....Kaba, tukabane au ua ukiniwahi, nikuue.
Hunters ya ubungo au?mwaka gani huo?Tuko watatu tuna kross bich to bich ilikua sikukuu flani hivi. Tumetembea kandokando ya bahari toka chadibwa tunaelekea hunters. Katikati wakaibuka vibaka na mavisu mkononi "oyaa tusalimianeni basii". Dooh nikajua on target. Kwakua mi nilishika kamera wakanianza mimi wenzangu wakafungukaa. Dooh nikawa sina jinsi mepigwa sana mabapa ya panga wakanipukutisha kila kitu. Nilikua mgumu kutoa waleti, nikaonja panga la mgongo, nikajua no jock wakanipulula asee. Walivomaliza wakawaunganishia na wenzangu. Asee siwezi sahau siku hiyo. Nilitembea kwa mguu mpaka kivukoni usiku saa mbili. Damu zinanitoka nikamwomba msamaria buku akanipa nikapata nauli nafika home nawakuta washkaji wanapanga jinsi ya kwenda kunitafuta. Walijua nishauwawa tayari
Ndomboro ya soro haha[emoji23] [emoji23]Pablo Blanco hao jamaa wakikuwahi huna tena ujanja hata kama unayo silaha ya kujihami. Wana kawaida moja, wakitega sehemu huwa wanakuwa group si chini ya watu hata wa 4 au zaidi; jaribu kufikiri watu wa 4 wote wakikuweka kati lazima ucheze ndomboro ya soro.
Waliwahi kunifanyia "ambush" walikuwa kama sita hivi sasa kwa kuwa sikuwa nimejianda na sikujua hili wala lile walifanikisha azma yao!
But nilitafakari sana lile tukio hivyo nikaamua kutafuta mbinu ya kupambana nao wakati mwingine, hivyo nilipata mbinu ya kupambana nao kulingana na mazingira tofauti tofauti, aina ya vibaka, idadi ya vibaka na aina ya silaha wanazotumia!
Siku wakaingia katika mtego, kwa kweli nadhani huko waliko kama wanakumbuka hilo tukio nahisi watakuwa wanadhani walipambana na jini!
Anamaanisha ungesimulia tukio,maana we tukio hujaelezea lilikuajeSiyo mkwara boss, kama wewe ni kibaka ingia kwenye anga zangu utapandisha uzi hapa!
Waliwahi kunifanyia "ambush" walikuwa kama sita hivi sasa kwa kuwa sikuwa nimejianda na sikujua hili wala lile walifanikisha azma yao!
But nilitafakari sana lile tukio hivyo nikaamua kutafuta mbinu ya kupambana nao wakati mwingine, hivyo nilipata mbinu ya kupambana nao kulingana na mazingira tofauti tofauti, aina ya vibaka, idadi ya vibaka na aina ya silaha wanazotumia!
Siku wakaingia katika mtego, kwa kweli nadhani huko waliko kama wanakumbuka hilo tukio nahisi watakuwa wanadhani walipambana na jini!
Baada ya hapo?Sio mbali, jana tena tukio kama hilo kidogo linitokee kama sio kuwa makini ingekula kwangu. Nilikuwa natoka Kunduchi nakwenda nyumbani Salasala; mapema tu saa 2 usiku nikasema leo sipandi bodaboda wala bajaji -- leo natembea taratibu kwa miguu mpaka nyumbani.
Safari ikaanza, nikatembea ikabaki kipande kidogo tu niingie mitaa ya home ila kuna mtaa mmoja ndio huwa njia yangu ya miguu siku zote japo mazingira yake sio mazuri kuna miti na vichaka vingi. Nilipofika hapo nikawaona watu watatu wamesimama katikati ya njia kama walikuwa wanajadili kitu hivi, nikawasoma nikajua kabisa hawa sio watu wazuri nikasita kuendelea na safari, pembeni yangu kulikuwa na nyumba ina duka nikaona yes ngoja nipoteze lengo nikaulizie vocha... Nimekwenda mpaka dukani kujifanya nataka vocha, nikajibiwa zipo za Halotel na Tigo... Nikasema basi mimi nilikuwa nahitaji ya Vodacom...
Pole kiongoziWaungwana hii kitu isikie tu kwingine
usiombe yakukute!
mara ya kwanza kutaitiwa na vibaka ilikuwa 2010.
nimetika klabu bwaxx bwaxx!
nikajikaza mdomdo kuelekea homu nikazime huko!
navuka reli kumbe kuna jamaa wamelala pale na hivi vimbaumbau sikujua nikajua reli kidogo niwakanyage!
mara mmoja akaniita oyoo kamanda una fegi hapo??!!nikasimama tu nashangaashangaa!
mara paap mmoja akanirukia mgongoni tukaenda wote chini mwingine akaja akanikanyaga miguu!
mwingine akaja na kisu nikawaambia chukueni msiniumize.
yule jamaa wa kisu akashika mfuko wa akauchana na kisu yaani akaondoka na mfuko wa suruali na vitu vyote humo!yaani walikata kama wanachinja vile!
hao wakasepa na chenji chenji na simu mbili!
Sitasahau na hiyo nimepanda boda usiku kutokea klabu kufika njiani jamaa wa bodaboda akaruka akaniacha na pikipiki nikapiga nayo mzinga wa atari!
kumbe dili bana ila nainuka nashangaa jamaa wanakuja wakijifanya wanataka kutoa msaada kumbe ndo vibaka asee walinikwarua kila kitu!
ila nashkuru kwa hayo matukio yote sijawah tobolewa jicho!
Kwa waliwahi kukutana na hizi kasheshe tupashane!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Uliwafanyaje mkuu Freyzem:Waliwahi kunifanyia "ambush" walikuwa kama sita hivi sasa kwa kuwa sikuwa nimejianda na sikujua hili wala lile walifanikisha azma yao!
But nilitafakari sana lile tukio hivyo nikaamua kutafuta mbinu ya kupambana nao wakati mwingine, hivyo nilipata mbinu ya kupambana nao kulingana na mazingira tofauti tofauti, aina ya vibaka, idadi ya vibaka na aina ya silaha wanazotumia!
Siku wakaingia katika mtego, kwa kweli nadhani huko waliko kama wanakumbuka hilo tukio nahisi watakuwa wanadhani walipambana na jini!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125]Siyo mkwara boss, kama wewe ni kibaka ingia kwenye anga zangu utapandisha uzi hapa!