Kirikou Wa Kwanza
JF-Expert Member
- May 24, 2013
- 3,564
- 1,991
Nikaondoka dukani, lakini nilipowaangalia wale jamaa nikawaona bado wamesimama pale njiani, nikasema sipiti tena hapo ilikuwa njia panda nikabadili njia nikaona bora nizunguke tu. Taratibu nikiwa natembea kwa tahadhali kabla sijafika hata mbali nikageuka nyuma nikamuona mtu ananifuata, nikamuangalia kama sek. 5 hivi nikaangalia upande wa juu nikaona jamaa wawili wanakimbia kuniwahi kama wanataka kuni over take, nikajua enhe kazi imeanza ila leo hawanipati... Mzee nikala kona kwenye kichaka kikatoka nduki mpaka yalipo makazi ya watu nikarudi mpaka barabara kuu nikasema hapa nipo salama, nikamshukuru sana Mungu.