KWA TULIOWAHI KUTAITIWA NA VIBAKA NA MAJAMBAZI TUKUTANE HAPA.

hii ishu isikie tu kwa mtu ila hisikutokee me nilishasemaga kabisa siwezi kutemeshwa na vibaka sasa majuzi sikukuu naenda zangu beach flani nikakutana na jamaa kisura ni kuwa namfaham but sikumbuki nilimuona wap akanichangamkia akaniuliza namkumbuka? nikajibu yah kama nakupata niaje akajibu flesh tukapiga story kama sekunde kumi uku tumesimama nikamuuliza nikumbushe tulikutana wapi akachomrkea mada eti niazime sim yako nimrafute jamaa yangu amesema nimsubili apo beach sasa hatokei

mmh nikashtuka chini nimepiga pensi na earphone zangu sim inaonekana nikamwambia sim haina salio akasema nipe kwa sauti uku kakaza sura mda huohuo wakatokea majaa wengine nikaona huu msala sasa afu jamaa kama anachomoa kisu kiunoni
bila uwoga wala kitete nikamwambia kuwa mshkaji wangu icho kisu hakitakusaidia chochote hii sim siwezi kuwapa labda niwape nauli iliobaki tu mfukoni na elfu tano wakasema lete nikawàpa due ile wameshapokea yu mshaji mwingine kaja kwenye mfuko wa simu anataka simu nikakaza mkono kajamaa hakakua ata na nguvu nikawaza pale nikajua hapa demokrasia haitumiki tena kama noma naiwe noma ile nataka kulianzisha wapitanjia wakatokezea wakaniaga poa brother safari njema nikatoka zangu uyoo lakini nilikuwa nimeshaapa moyoni siwezi kutemeshwa simu vinginevyo mpaka watumie nguvu za ziada kama wakiweza
 
Mimi siku hiyo natoka zangu kwenye mishe kama saa 5 usiku sasa kuna njia ya shortcut ya makabulini, nikasema nipite. Sasa ile kufika kwa mbali nikaanza kusikia harufu ya bangi na nikawaona jamaa kwa mbali wanavuta ile kitu wamekaa jirani na kaburi. Nikataka kukikmbia nirudi lakini akili ikanijia nivue nguo zote na nikazivilingisha nyuma yangu mgongoni halafu nikaanza kutembea taratibu kuwafauta pale walipokaa. Ile jamaa kuniona wakastuana na kuanza kunisogelea, ile kufika karibu na mimi na ile mbalamwezi walikakauta niko uchi kabisa. Jamaa walistuka kichizi kunuion vile na bangi zikaisha ghafla, kuna moja alianguka vibaya wakati anakimbia.

Ile ndiyo ilikuwaga ponapona yangu aisee, sikurudia kupita njia ile tena.....
 
MKUU NDIYO ZILE ZA MILIONI NINI? MIMI MWENYEWE NINGEKAZA
 
Bro...nadhani umeona advertise ya timu ya wananchi....haya hebu funguka hapo ikulu walikufanyaje?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaah nimeona bro....
Pale aisee siku hiyo najivinjari mitaa ya ule ufukwe kuanzia kule ocean road hospital, nikawa nakuja mdogo mdogo pale kivukoni nipande gari kurudi mbezi. Basi nafika usawa wa pale geti la ikulu nikavamiwa na kundi la vibaka kama 5 hivi. Wakachukua simu na pesa kama elfu 50. Tangu hapo mitaa ile naiogopa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We ndio funga kazi!je wangekuingilia kimwili ingekuwaje?!!siku ingine usivue nguo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaa.. [emoji3][emoji3][emoji3]

Hii ni nyoko aiseee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kigogo hiyo.Nilienda kwa mjomba sasa hapo nilikuwa nimejifunza kurusharusha ngumi hewani nipo fit halafu nimepiga push up za ngumi za kutosha nina nakozi ngumu hatari,mwili una nyege ya ugomvi htr.Kumbe huo mtaa una vibaka mi sijui natoka zangu saa 3 hivi kwenda kununua vocha nakutana na mtoto tu wa km miaka 15 hivi kanitokea kwa nyuma ananiambia nimetumwa kuchukua 10000 na ma bro wale pale, nacheki mbele nakuta watu km wa 3 au 4 hivi.Niligeuka nilipiga ngumi ya chembe yule mtoto,nzito,ya uhakika,ya kujiamini.Yule dogo alienda chini kama alivyo bila kelele na hapo hapo nikarudi nilipotoka na speed ya htr,jamaa wakaunga wapiiii hapo nina pumzi zangu za kuruka kichura chura.Mwezi ukaisha nikarudi kwetu ila yule dogo alipata cha kusimulia manake nilipiga ngumi na nikajisikia kabisa hii imezama..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka flan hiv maeneo ya sinza napeleka chakula kwa mgonjwa mida ya usiku,,nimebeba kapu lina mahotpot na chupa ya chai,,kufika kwenye giza nakutana na wajinga wametega mara nasikia sauti,,oya we simama" mm nikawaangalia huku naendelea na safar yangu,,nikasikia tena oya ww lete kapu hilo huku wanakuja na mapanga yao,,,yan hiyo siku ndio nikajua kuwa hata binadamu wanazo turbo kama zinazofungwa kwenye magar ila hatujijui tu,,maana nilikimbia mpaka nikawa najishangaa,,,na ingine ilikuwa mida ya saa sita ucku nipo ndani njaa inauma nikasema nitoke nikatafute hata chips nijitulize,,sasa nafungua geti natoka nje nasogea kama hatua tano nikakuta wajinga wametega wapita njia ila wao hawakuniona,,nikajua tu hawa sio watu wema maana mtaa wangu naujua mim kuanzia saa tatu huwa hakuna mtu mazingira yale,,basi wakati nawachora mmoja wao akaniona,,akawatonya wenzie,,mara nikaona wanajitawanya nikajua hawa wananilia timing nikajibana kwenye giza alafu nikarudi mdogo mdgo nikafungua geti nikajibanza kwa ndan,,nikawa nawasikilizia,,mara nasikia wamefika nilipokua nimesimama kwa nje alafu wanalaumiana,,"dah tumezubaa jamaa atakua kaingia kwenye hili get hapa"maana get limejificha kidogo kwahiyo mtu kujua kama hapa kuna mlango sio rahisi,,tangu siku hiyo sitoki tena usiku kizembe lazima niweke tagi bavuni alafu natoka kibabe,,wakiniona unasikia bro niaje maana mwendo na mkwara wangu wenyewe wanaona huyu jamaa ni mwamba kumbe mm mzee turbo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…