Imewahi kunitokea, nakumbuka vizuri sana nilikuwa natoka kwenye mishe mishe zangu, nilifika mahali ambapo zinapita bodaboda nyingi na watu wachache tu wanaotembea kwa miguu. Nilikuwa nina simu 2; moja ya touch nyingine ya Nokia ilikuwa ndogo na kiasi cha Tsh 7000 mfukoni pamoja na chaji ya smartphone.
Nakumbuka wakati natembea taratibu kwa maringo kama Twiga, simu yangu ya touch ikaingia massage ya WhatsApp, nikaiotoa ili kuisoma aisee ile message na ule mwanga wa simu viliniponza kabla hata sijafika mbali nilishtuka nimepigwa roba moja kali sana mpaka nikahisi pumzi inataka, nikajua enhe hapa tayari nimekabwa na wahuni. Usiombe kukutana na hao wajinga hawaoni shida kutoa uhai wako. Ile distance ya kutoka zinapopita bodaboda na tulipokuwa sisi ilikuwa ni hatua chache sana ingawa kiza kilikuwa kikubwa. Nashukuru hawakunichana hata na kiwembe japo nilijitahidi kuwazuia walinishinda power nilichezea tu ngumi za uso wakaondoka na simu yangu ya touch.