Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
- Thread starter
- #41
Tunapendelea vita viishe haraka na vyakula na mafuta vishuke bei.
Zelensky naye kasema atafanya kama hivyo kwa meli za Urusi zitakazokatiza eneo hilo. tuangalie kitisho cha nani kitakuwa na nguvu na athari kwa mwenzake. Suala la Ukraine kusafirisha ngano yake kwa njia ya bandari tatu zilizobaki mikononi mwake ni la muhimu ili abaki kuwa hai na kuwa na pesa ya kuendelea na vita.
Njia atakayobaki nayo ni matumizi ya vyombo vya ardhini kama garimoshi kupitia Poland na nchi nyengine inazopakana nazo ukiondoa Belarus. Matumizi haya ni ya gharama sana na mzunguko mkubwa kuyafikia masoko kama ya mashariki ya kati na Afrika na hata kwa nchi za Ulaya nazo pia zitazipata bidhaa hizo kwa shida.Na zaidi ni kuwa nchi marafiki na Ukraine wameamua kutokubali kupitisha bidhaa za kilimo za Ukraine kuelekea kwenye masoko yake kwa vile bidhaa hizo huwa zinabaki nchini mwao kwa muda mrefu kutokana na mdororo wa usafiri na hilo hupelekea kwa namna moja au nyengine kushuka bei sana kwa mazoo yake ya kilimo jambo lililollalamikiwa na wakulima wake tayari.
Hakuna njia ya uhakika ya kusafirisha kiwango kikubwa cha bidhaa za Ukraine kuliko bahari.Kwa upande wa Urusi matumizi ya bahari nyeusi ni mepesi kwake lakini ana nafasi ya kutumia bandari nyengine zilizokuwa za Ukraine kutoa na kuingiza bidhaa zake ILI kukwepa kuwa karibu na shabaha za drones za Ukraine.
Kuonesha kuwa Urusi imeona madhara ya kuruhusu meli kuingia na kutoka Odessa siku tatu za mwanzo tu ya kujitoa mkataba huo imeshambulia bandari hizo na kuharibu miundo mbinu muhimu ya kupakilia na kushushia bidhaa hizo.