Kwa uchafu unaoendelea nchi nzima ni vema Waziri wa Tamisemi akajiuzulu au atimuliwe

Kwa uchafu unaoendelea nchi nzima ni vema Waziri wa Tamisemi akajiuzulu au atimuliwe

Naona umetafuta mbuzi wa kafara. Hivi kwa akili zako inamaanisha kweli hujui hayo yanayofanyika yana baraka za nani?
Huu ujinga unaotendwa na watendaji wa vijiji na kata nchi nzima wa kuhakikisha fomu za wagombea wa upinzani hazipokelewi kwa udi na uvumba, haujawahi kuwepo kwa kiwango kama hiki tangu nipate akili, sijawahi kuona serikali ya ccm isiyojiamini kama hii tangu nchi hii iachwe na wakoloni, ni aibu kubwa sana.

CCM imeishiwa pumzi kabisa ! bila watendaji hakuna kitu.

Natoa wito kwa Waziri Jaffo kujiuzulu mara moja kwa vile ameshindwa kusimamia mchakato wa haki wa uchaguzi wa serikali za mitaa, fomu za wagombea zinachanwa, zinakataliwa, wengine wanakimbiwa na watendaji hadi kufikia baadhi ya watendaji kuvunjika miguu baada ya kuanguka kwenye korongo, huku Waziri akinyamaza tu.

Aibu iliyoletwa awamu hii haijawahi kuletwa kwenye nchi hii tangu mfumo wa vyama vingi uanze.
 
Huo uchafuzi una baraka zote kutoka kando kando ya bahari.
 
Wajinga wa ccm wanasema upinzani hautapata mitaa hata 20 nchi nzima, sasa uoga wa nini?
 
Mngekuwa ni watu wa kupongeza pale mazuri yanapofanyika bila shaka hata malalamiko yenu yangesikilizwa. Ila sasa hivi mnaonekana vituko tu kwa sababu hakuna jambo mmewahi kupongeza.
Unataka wapongeze ujinga wenu!
 
Mwacheni Jafo atimize majukumu yake!
Hahaha, kwani huyo waziri ni wa chama gani?!

Kwanini afukuzwe ikiwa yanayofanyika yanalenga kukisaidia chama chake?

Nani amfukuze ikiwa chama kinacho nufaika na haya ni ccm?!
 
Matokeo ya semina elekezi iliyofanywa jumba jeupe hivyo karibuni.
Ni matukio coordinated very strange
 
Siungi mkono yanayofanywa na ccm ila km pana viongozi bora utawala huu wa magufuli basi jaffo huwezi mueka pembeni kinachomponza yupo ccm mfano suala LA majuzi wanafunzi kupigwa akakemea lkn Mzee kaenda kuunga mkono
 
Back
Top Bottom