Kwa 'Uchawi' unaofanyika ambao ni wa 'Kufuru' Wajukuu wa Hayati Mandela watajuta kuwafahamu Wajukuu wa Hayati Nyerere kwa Mkapa Kesho

Kama huyo mganga ni hatari kiasi hicho,TP mazembe wangekuwa wanachukua hilo kombe la CAF kila msimu,Simba Safari imeisha subiri msimu ujao
 
Huu uzi utakuwa na wachangiaji wengi sana baada ya mechi. Wengine watakuja kumponda mleta uzi na wengine watakuja kumpongeza mleta uzi kwamba kapita mle mle. Binafsi hili swala sipingani nalo, nilitegemea Simba watafanya kila mbinu ili ipindue meza, kwenye mpira uchawi upo. Nikikumbuka mechi ya juzi juzi hapa kati ya Simba na timu za nje ya nchi ndani ya uwanja wa Mkapa unaona kabisa wapinzani wanavyozidiwa maana mpira wanautafuta kwa tochi na magoli pia hawayaoni. Al Ahly ilipata shida sana utadhani anacheza na Bayer Munich jinsi walivyozidiwa.
 
Kamati ya Ufundi isha fanya yao !
 
Al ahly hawapo vizuri wanashindia bahat. Kama uliangalia game lake na mamelod utakubaliana nami.
 
Walianza wao SSC wanamaliza...
 
Wanaweza wakawa wamekuja nao, ila mazingira ya kuutega yanaweza yakawa changamoto kwao. Si umesikia Kwa Mkapa kunalindwa na 'makomandoo' siku ya tatu mfululizo leo!
Hawa makomandoo ni wanajeshi wa south afrika au
 
Mkuu huyu Mtaalam ( Mganga ) wa Congo DR wa TP Mazembe ' Vitu ' anavyovifanya eneo la Siri Mikocheni lililo Jirani pia na Bahari ya Hindi kuna Watu Kesho watafungwa Goli 6 au 7 kwani ni ' Kufuru ' tupu tu
Kwa msisitizo wako Mkuu Sina shaka kesho itakuwa patashika nguo kuchanika....
 
SIMBA KESHO AKISHINDA NA KUFUZU NITAWEKA HAPA REAL NAME, VYETI VYANGU, KITAMBULISHO CHA KAZI, MAHALI NINAPOISHI, NITATOA MSHAHARA WANGU WA MWEZI HUU NA KUWANUNULIA TIMU YA SIMBA KWA WIKI NZIMA.

MATOKEO RASMI YA GAME YA KESHO
SIMBA 2 - 3 KAIZER CHIEFS
Kwa nilivyoiangalia hii mechi kwa jicho la kiufundi (maana uchawi haupo ktk soka)
SIMBA ITAANZA KWA MPIRA WA KASI SANA DK 10 ZA MWANZO NA NDANI YA DK HZO kutokana na presha yao KAIZER CHIEFS WATAPATA BAO LA KUONGOZA hali itakayopelekea Simba kuchanganyikiwa na kupigwa la pili dk chache mbele. Lkn matokeo ya mwisho simba atafungwa 3 - 2
 
Hawa makomandoo ni wanajeshi wa south afrika au
'makomandoo' kama 'makomandoo'. Serikali ipo na Simba, funguo za mageti ya Kwa Mkapa zilisakabidhiwa muda mrefu kwa Simba, wao washindwe wenyewe! Ukisikia AC za vyumba vya kubadilishia nguo zinafanyiwa ukarabati, wala usidhani kwamba zilizopo zimechakaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…