Kwa 'Uchawi' unaofanyika ambao ni wa 'Kufuru' Wajukuu wa Hayati Mandela watajuta kuwafahamu Wajukuu wa Hayati Nyerere kwa Mkapa Kesho

Sawa bhana haya wape na hiyo
 
He!. Makubwa haya. Haji si tayari ameshampoteza Bibi yake jana, inatosha- Goli la nne hilo. Tuishie hapo ili twende kwenye penart
 
Nachojua Simba atashinda. Lakini kwa Magoli zaidi ya manne? Inahitaji mshipa.
 
Wapi Shomari Kapombe?
Tunafurahishana tu mkuu, Hizi ndio burudani unazoweza kuzipata Tanzania tu. Ndio maana kuna watu huwa wanazimia au kufa kwa presha maana vifua vyetu vinajazwa sana hizi imani, ukija uwanjani ngoma inakuwa tofauti.

Kiuhalisia leo unaweza kukuta Wawa akimpisha Kened Juma. Nyoni hana kasi sio rahisi kucheza nafasi ya Kapombe. Kumbuka ile forwadi ya Kaizer inakimbia kama imefungwa Mota labda hizi ndumba zifanye kazi ya kuwapiga misumari.
 
Dah, kweli kaka! Nimejiskia sana! Yaani Bibi yake kamtoa kafara ili timu ipate matokeo!
Hiyo mizimu ya Congo Ingemchagua Mo au Badra au Haji halafu timu itaenda kutolewa nusu fainali nayo si ingekuwa hasara juu ya hasara?

Maamuzi mazuri ni kukubaliana na matokeo yoyote hata timu ikitolewa hapa robo fainali panatosha tu. Timu mnaipigania iende nusu fainali halafu napo mtaanza tena kufikiria mtoe damu ya nani? Au tutoe kiganja cha kiongozi wetu wa zamani yule Senzo?.. Maana huko mbele wababe waliosalia ni wagumu zaidi ya Kaiza.

Ufanyike usajili bora kwa msimu ujao - Hongereni Simba na Namungo hapo mlipofikia panatosha wala sina cha kuwadai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…