HOJA Kwa ufaulu huu wa 99.9% mamlaka husika zitazame upya kozi za afya na uhitaji wake

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

GUZMAN CHAPO

Member
Joined
Jun 16, 2026
Posts
22
Reaction score
56
Kulingana na ufaulu wa kidato cha sita kuendelea kupanda na kuwa juu kadri miaka inavyozidi.Ni muda muafaka sasa mamlaka husika zikafanya jitihada za kimakusudi kutanua wigo wa masomo ya kozi za afya nchini.

Katika nchi ya Tanzania bado wahitimu wengi wa kidato cha sita tahasusi ya PCB wanamawazo ya kozi zilezile miaka nenda rudi huku soko la kozi hizo likiendelea kushukua kila mwaka.

Kozi kama Degree ya udaktari wa binadamu, ufamasia na unesi ndio ndoto ya kila mwanafunzi wa tahasusi ya PCB.Lakini mahitaji katika mazingira ya kila siku vituo vya afya na mahospitali ni zaidi ya UDAKTARI,UFAMASIA NA UNESI.

Kuna wataalamu kama OPTIOMETRY(WATAALAMU WA MIWANI NA MACHO), PHYSIOTHERAPY, DIAGNOSTIC RADIOLOGY,ANAESTHESIA, EMERGENCY AND CRITICAL CARE,N.K. Hawa wataalamu wanahitajika kwa wingi lakini kwa kiasi kikubwa bado tunategemea wale wa SHORT COURSE.

Nchi kama India wanatoa degree ya hizi kozi.Kwanini sisi bado tunaendelea kutoa vishort course vya mwaka mmoja.

Nchi kama India wamepiga hatua kubwa sana katika matibabu kwakuwa wataalamu ni wengi na wabobevu.Kwamfano mtaalamu wa kutoa ganzi na dawa za usingizi (ANAESTHESIA).Aliyesoma short course ya mwaka mmoja huwezi kumfananisha na aliyesoma kozi hiyo hiyo kwa miaka mitatu level ya degree.Huduma ya mtaalamu huyu wa miaka mitatu au minne ni ya hali ya juu kutokana na muda aliotumia kusoma na kujifunza kwa vitendo.

Pia baadhi ya kozi zifutwe ili kutoa nafasi kwa kozi mama kuweza kustawi vizuri.Diploma in Clinical medicine imeshakuwa SUPER SATURATED wahitimu ni wengi lakini lengo lake hasa la kuanzishwa ilikuwa kufidia gap la upungufu wa madaktari kwa miaka hiyo.Kwa sasa wahitimu wa shahada ya udaktari ni wengi sana kiasi kwamba wengine wako mtaani hawana ajira.Ukiachilia mbali wingi wa wahitimu wa shahada ya udaktari pia kufuta kozi hii ya diploma ya udaktari kutaboresha huduma zaidi katika level zote za kutolea huduma za afya.

Kurudisha kozi ya cheti cha wahudumu wa afya.Hii kozi ilifutwa miaka michache nyuma angali inaumuhimu wake mkubwa katika kutoa huduma za kila siku mahospitalini.Mhudumu wa afya alikuwa anafundishwa mambo yote ya usafi maeneo ya hospitali na jinsi ya kujilinda na taka za hospitali.Pia walifundishwa kusaidia baadhi ya kazi kama.Kupeleka wagonjwa mahodini na kwenye vipimo kwa wagonjwa wasiojiweza wanaohitaji usaidizi mdogo.Hii iliboresha sana mazingira ya kazi na usalama katika sehemu za kutolea huduma.

Kwa kumalizia, muundo wa kada za afya ubadilishwe ili kuvutia zaidi wahitimu wengi kuweza kujigawa katika kozi mbalimbali kuliko hii ya sasa kila mhitimu anakimbilia UDAKTARI NA UFAMASIA AU BIOMEDICAL ENGINERING kwakuwa muundo wa hizi kozi unaanzia ngazi ya juu ya mshahara kuliko kozi nyingine.

Kozi ya unesi japo wengi wanaikimbilia ila wakifika makazini morale ya kazi inapungua sana maana hakuna uwiyano wa majukumu na ngazi ya mshahara.Nesi anasoma degree miaka minne sawa na mfamasia ila nesi yupo ngazi ya chini TGHS C huku mfamasia akiwa ngazi ya TGHS D na daktari TGHS E.

Wataalamu wa maabara wanapiga kazi nyingi na vile wako wachache lakini ngazi ya mshahara kwa DEGREE ni TGHS C,vivyo hivyo na CLINICAL NUTRITION na DIAGNOSTIC RADIOLOGY.Hii inapunguza ushawishi kwa wahitimu kwenda kwenye hizi kozi kwakuwa maslahi yanatofautiana kidogo sana na wa DIPLOMA.Pia hawa wataalamu kwenda kujiendeleza imekuwa mtihani kwakua NGAZI ZA MSHAHARA hazishawishi.

Ikiwezekana kuwe na flat rate kwa ngazi ya degree kama ilivyo kuwa flate rate ngazi ya mishahara kwa ngazi ya Diploma wote TGHS B.

#Kazi na utu.
 
Kwa ufaulu huo wa 99.9% wachache wenye division 2 watapata kozi za afya wengine watatawanyika almradi degree na the rest watarudi kusoma DIPLOMA kama kifuta jasho kwa kazi yote waliyoifanya kwa miaka miwili A-level.

Ni ukweli mchungu,na ndo uhalisia.
 
Umeandika vizuri ila ungeweza kufupisha kwani hapo maelezo mengi yamejirudia rudia
Always hit the nail on the head hakuna haja ya kujieleza saaana.

Hivi hii mitihani ya PCB ya kizazi hiki ni ile ile tulikuwa tunafanya miaka ya 2010?
Enzi zetu tulikuwa tunasoma usiku mzima ILA siku hizi kjana yupo yupo tu, ana kula beats na game bado anapata Div one au 2?
 
Issue ni uhitaji mkuu.

Kwa nchi za dunia ya 3 wanaona ni hasara kuajiri mtu aliyesoma Midwifery tu au Critical Care tu, wakati wakimuajiri mtu aliyesoma General Courses ataweza kuwa Multipurpose.

Nakumbuka waliwahi kuanzisha Bachelor Degree ya Midwifery baadaye wakaifuta maana ilionekana haina maslahi kwa waajiri.
 
ila huu ufaulu badae utaleta shida sana, sijui wanafaulu kweli ama wanatufurahisha wazazi
Ukiangalia GUIDE BOOK ya NACTE 2026/2027 ni hatari tupu.

Projection yangu by 2030 hakuta kuwa tena na kozi zinaitwa hot cake!!!

Nacte wamefungulia mbwa😀😀😀.Kila chuo inaudahili capacity ya 100 na kuendelea hii ni hatari sana. Najiuliza tu huko juu wanaotoa vibali vya kuanzisha hizi kozi wanaangalia na ubora wa elimu,miundombinu na mazingira ya kujifunzia???!!!.

Chuo hakina hata hospitali ila kina kozi nne mpaka sita na kozi hizo zote zinahitaji practical🤔🤔🤔

Walezi na wazazi waangalie san hivi vyuo.Mwisho wa siku watoto wao hawatakuwa na ufaulu bali ufaulu alimradi na ndo itakuwa habari imeishia hapo.
 
Issue ni uhitaji mkuu.

Kwa nchi za dunia ya 3 wanaona ni hasara kuajiri mtu aliyesoma Midwifery tu au Critical Care tu, wakati wakimuajiri mtu aliyesoma General Courses ataweza kuwa Multipurpose.

Nakumbuka waliwahi kuanzisha Bachelor Degree ya Midwifery baadaye wakaifuta maana ilionekana haina maslahi kwa waajiri.
Huu utitiri wa vicollege vinafunguliwa kila uchochoro inaomesha hii ni lucrative bussiness.

Uhitaji upo wakutosha sana, ni vile uelewa ni mdogo.Watu wengi wanapewa rufaa unecessary wakati kama kungekuwa na wataalamu wa kutosha rufaa zingekuwa chache.

Wengine wanachelewa kugundulika magonjwa yao kisha kupata huduma stahiki.Hii inapelekea mgonjwa kuchelewa kupata matibabu na kuishia na hasara,kupoteza kiungo au kifo.

Kuachive huduma bora pia kuangalie ratio ya staff to client.Mambo ya bora liende alimradi mzigo ufike punda afe katika karne hii umepitwa na wakati.
 
Priority ya serikali ni "Cheap Labors".

Ndiyo maana kwenye posts zote za ajira Diploma wanapewa kipaumbele wakati wenye Bachelor Degree wamejaa telee mitaani.
 
Umeandika vizuri ila ungeweza kufupisha kwani hapo maelezo mengi yamejirudia rudia
Watu wengi hupenda kusoma mada fupi...always hit the nail on the head hakuna haja ya kujieleza saaana.

Hivi hii mitihani ya PCB ya kizazi hiki ni ile ile tulikuwa tunafanya miaka ya 2010?
Shukrani kwa ushiriki wako,

Ni vile hujui vizuri hao unaoita watu wengi.Hao watu wengi ambao ni wavivu na wazembe wanapenda vitu soft na vyenye msisimko wapo radhi wasome kurasa tatu za mada inayoelezea ngono na upuuzi upuuzi.

Hii mada ipo kucreate aweareness haipo kutafuta wasomaji wengi.

Wewe soma ambulia kitu kisha kama upo kwenye position ya kiamamuzi chukua hatua.
 
U
Kulingana na ufaulu wa kidato cha sita kuendelea kupanda na kuwa juu kadri miaka inavyozidi.Ni muda muafaka sasa mamlaka husika zikafanya jitihada za kimakusudi kutanua wigo wa masomo ya kozi za afya nchini.

Katika nchi ya Tanzania bado wahitimu wengi wa kidato cha sita tahasusi ya PCB wanamawazo ya kozi zilezile miaka nenda rudi huku soko la kozi hizo likiendelea kushukua kila mwaka.

Kozi kama Degree ya udaktari wa binadamu, ufamasia na unesi ndio ndoto ya kila mwanafunzi wa tahasusi ya PCB.Lakini mahitaji katika mazingira ya kila siku vituo vya afya na mahospitali ni zaidi ya UDAKTARI,UFAMASIA NA UNESI.

Kuna wataalamu kama OPTIOMETRY(WATAALAMU WA MIWANI NA MACHO), PHYSIOTHERAPY, DIAGNOSTIC RADIOLOGY,ANAESTHESIA, EMERGENCY AND CRITICAL CARE,N.K. Hawa wataalamu wanahitajika kwa wingi lakini kwa kiasi kikubwa bado tunategemea wale wa SHORT COURSE.

Nchi kama India wanatoa degree ya hizi kozi.Kwanini sisi bado tunaendelea kutoa vishort course vya mwaka mmoja.

Nchi kama India wamepiga hatua kubwa sana katika matibabu kwakuwa wataalamu ni wengi na wabobevu.Kwamfano mtaalamu wa kutoa ganzi na dawa za usingizi (ANAESTHESIA).Aliyesoma short course ya mwaka mmoja huwezi kumfananisha na aliyesoma kozi hiyo hiyo kwa miaka mitatu level ya degree.Huduma ya mtaalamu huyu wa miaka mitatu au minne ni ya hali ya juu kutokana na muda aliotumia kusoma na kujifunza kwa vitendo.

Pia baadhi ya kozi zifutwe ili kutoa nafasi kwa kozi mama kuweza kustawi vizuri.Diploma in Clinical medicine imeshakuwa SUPER SATURATED wahitimu ni wengi lakini lengo lake hasa la kuanzishwa ilikuwa kufidia gap la upungufu wa madaktari kwa miaka hiyo.Kwa sasa wahitimu wa shahada ya udaktari ni wengi sana kiasi kwamba wengine wako mtaani hawana ajira.Ukiachilia mbali wingi wa wahitimu wa shahada ya udaktari pia kufuta kozi hii ya diploma ya udaktari kutaboresha huduma zaidi katika level zote za kutolea huduma za afya.

Kurudisha kozi ya cheti cha wahudumu wa afya.Hii kozi ilifutwa miaka michache nyuma angali inaumuhimu wake mkubwa katika kutoa huduma za kila siku mahospitalini.Mhudumu wa afya alikuwa anafundishwa mambo yote ya usafi maeneo ya hospitali na jinsi ya kujilinda na taka za hospitali.Pia walifundishwa kusaidia baadhi ya kazi kama.Kupeleka wagonjwa mahodini na kwenye vipimo kwa wagonjwa wasiojiweza wanaohitaji usaidizi mdogo.Hii iliboresha sana mazingira ya kazi na usalama katika sehemu za kutolea huduma.

Kwa kumalizia, muundo wa kada za afya ubadilishwe ili kuvutia zaidi wahitimu wengi kuweza kujigawa katika kozi mbalimbali kuliko hii ya sasa kila mhitimu anakimbilia UDAKTARI NA UFAMASIA AU BIOMEDICAL ENGINERING kwakuwa muundo wa hizi kozi unaanzia ngazi ya juu ya mshahara kuliko kozi nyingine.

Kozi ya unesi japo wengi wanaikimbilia ila wakifika makazini morale ya kazi inapungua sana maana hakuna uwiyano wa majukumu na ngazi ya mshahara.Nesi anasoma degree miaka minne sawa na mfamasia ila nesi yupo ngazi ya chini TGHS C huku mfamasia akiwa ngazi ya TGHS D na daktari TGHS E.

Wataalamu wa maabara wanapiga kazi nyingi na vile wako wachache lakini ngazi ya mshahara kwa DEGREE ni TGHS C,vivyo hivyo na CLINICAL NUTRITION na DIAGNOSTIC RADIOLOGY.Hii inapunguza ushawishi kwa wahitimu kwenda kwenye hizi kozi kwakuwa maslahi yanatofautiana kidogo sana na wa DIPLOMA.Pia hawa wataalamu kwenda kujiendeleza imekuwa mtihani kwakua NGAZI ZA MSHAHARA hazishawishi.

Ikiwezekana kuwe na flat rate kwa ngazi ya degree kama ilivyo kuwa flate rate ngazi ya mishahara kwa ngazi ya Diploma wote TGHS B.

#Kazi na utu.
Unataka ma-MD wafanye kazi dispensary vijijini?

Pia watu walingane mshahara, je wewe ukisoma miaka mitano, mwingine miaka mitatu, halafu wote mlipwe TGHS-E, utajisikiaje? Hebu kuwa na nidhamu na taaluma za hao jamaa.
 
Back
Top Bottom