Kwa ufupi Hayati Magufuli aliwachukia watumishi wa umma

Jamaa anakumbukwa kweli kila siku lazma tred mpya kumhusu ije
 
hahaahaaaa vyeti feki wewe
 
Magufuli hakuwachukia watumishi Ila aliamini kwamba ili kufanya mtumimishi aweze kuishi Maisha nafuu Ni lazima Kuna mambo yakae Sawa na suluhu si kuongeza mshahara.

Kwa mfano aliamini kuwa kupunguza gharama za Maisha kunasaidia kumpa unafuu ,ndio maana yeye alikuwa anataka kuwezesha vitu vinavyoonekana gharama za Maisha.

Mfano aliamini umeme ukipatikana Kwa urahisi bhasi wazalishaji watapunguza bei ya vitu,aliamini ukisafirisha vitu Kwa kutumia train bhasi bei ya vitu itapungua,ukiweka mazingira mazuri bandarini bhasi gharama za vitu vitokavyo ughaibuni vitapungua gharama.
 
Alikuchukia wewe kwa kuwa ulikuwa na cheti fake lakini sisi watumishi wa vyeti original hatukuwa na shida naye kabisa.
Acha ujinga wewe. Kama wewe hukuwa na tatizo ndo unataka wote tunyamaze tusiseme alivyotunyanyasa?
Binafsi nilipandishwa 2016 nikalamba mshahara wa April pekee. From there alinishusha kwa kisingizio cha uhakiki na sikupanda tena mpaka lilipokufa shenzi lile
 
You are wrong very wrong. Kupenda au kutopenda Wafanyakazi haiko kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi, kilichomo ni kutetea na kuboresha maslahi yao. Katika muda wa Urais wake Magufuli. Wafanyakazi wamefaidika marudufu mara 4. Kwanza, kima cha chini kilipanda, maana yake TAKE HOME PAY ya kila mtu ilipanda by 26% across the board. Hiyo wewe unaita kupandisha mshahara. Pili, elimu bure. Gharama ya Private schooling Kindergarten ni milioni 3 na darasa la kwanza 1.5m/=. Hii ina maana Mfanyakazi kaokoa shilingi milioni 4.5 kwa kila mtoto, wastani wa Tanzania sensa iliyopita ni watoto wanne. Tatu, huduma zimekuwa bora. Ukienda shule mwalimu yupo, hospital nurse yupo, idara ya pensheni mtumishi yupo wanakuhudumia. Kabla ya Magufuli hapakuwa na discipline kama hiyo. Mwisho, nne, Magufuli kaokoa makanikia yetu na mikataba mibovu ya TTCL tuliyokuwa tupunjwe, tunaibiwa. Yote hii imeongeza huduma.
 
Ngoja Sukumagang na Mataga waje huku wakiwa wamejawa na jazba, kukutukana na kukuita mpiga dili na mwenye vyeti feki.
Hii je?

Uhttps://www.facebook.com/reel/1416575512418799?s=yWDuG2&fs=e&mibextid=Nif5oz
 
Ila enzi za JPM watumishi waliheshimika sana mitaani sijui ni kwanini.
 
Kwamba Magufuli aliongeza mishahara?
Labda huko aliko sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…