Kwa ufupi Hayati Magufuli aliwachukia watumishi wa umma

Kwa ufupi Hayati Magufuli aliwachukia watumishi wa umma

Sijui ni watumishi gani unawazungumzia.
Sie wengine tulidharaulika sana wakati wa shetani lile.
Mana ulikuwa unaitwa unafokewa jadharani mbele ya wananchi, refer mikutano ya Makonda, Ali Hapi na Ngosha mwenyewe.
Tulikuwa tunawekwa ndani na maDC kiholela tu. Halafu we unasema eti tuliheshimiwa
Kama ulikuwa mwizi na unadhulumu wananchi hiyo ilikuwa ni haki yako.
 
Ukiwa mwizi na kudhulumu wananchi unakufa mapema tena kifo cha hovyo kama lilivyokufa lile shetani lenu la Chato.
Limetuacha sasa hv tuna amani na furaha kama yote
Uwizi sio sifa nzuri mkuu acha hiyo tabia. Mwamba hajafa bado anaishi ndio maana haipiti siku bila uzi wa kumuhusu yeye kuletwa humu, sasa kama kikundi cha watu wachache tu wa jf kila siku wanamuwaza jiulize huko nje hali ikoje. Hata wezi na mafisadi wakitaka kufanya yao lazima wahisi sauti ya mwamba ikiwakemea ila wanashupaza shingo.
 
Kwani unadhani watu wengine wote tunawapenda watumishi wa umma?
Tuwapende kwa lipi la maana?
Kwa productivity yenu ndogo?
Kwa ulaji wenu wa rushwa?
Kwa kuzungusha watu maofisini bila kuwahudumia?
Kwa kutumia muda mwingi kupiga soga badala ya kufanya kazi?
Kwa uzembe na ubabaishaji uliojaa makazini mwenu ndiyo unataka tuwapendee?
Yani tuwapende kwa lipi haswa?
Kwa kupokea mishahara na marupurupu msioyafanyia kazi?
Kwa kuwa kwenye nafasi za kazi bila kufanya kazi? Mnakula pesa zetu za kodi bila kuzifanyia kazi. Kwa hiyo ndo unataka tuwapende kwa hayo?
Fikiri vizuri.
Pole weee!!!!
 
Hata yeye alikuwa mtumishi wa umma kabla ya kuwa mbunge na rais
Ndiyo maana akawashuhulikia, maana alikua anazijiua tabia zenu chafu za ufisadi! Na JPM ulikua ni mpango wa deep State kuwashuhulikia Watumishi wala Rushwa! Na bado msizani kufa kwa JPM huo mpango nao umekufa,bado atakuja another JPM very soon!!
 
Ha

Halafu huwa wajinga kweli!!! Huwa wanaamini kuwa mtu yeyote ambaye hakubaliani na baadhi ya mambo ya JPM basi huwa ni vyeti fake au mpiga dili!!!
Sasa Kama wwe siyo vyeti feki au mpiga deal,ni sababu ipi ilikufanya umchukie JPM!? Basi lazima wwe utakua na ndg au Jamaa walionyooshwa na Magu kwa ufisadi,na wwe ulikua unanufaika na huo uchafu ndiyo maana ukamchukia JPM!! Bishaa!!?
 
Sijui ni watumishi gani unawazungumzia.
Sie wengine tulidharaulika sana wakati wa shetani lile.
Mana ulikuwa unaitwa unafokewa jadharani mbele ya wananchi, refer mikutano ya Makonda, Ali Hapi na Ngosha mwenyewe.
Tulikuwa tunawekwa ndani na maDC kiholela tu. Halafu we unasema eti tuliheshimiwa
Si mlikua wazembe ndiyo maana mlikua mnashuhulikiwa kikamilifu,mbona Watumishi wengine walikua hawafanyiwi hivyo!? Nyinyi ndiyo wale Watumishi mliona office za Umma ni Kama Mali zenu binafsi mnafanya mnavyotaka huku mkitesa wananchi wa kawaida wanaokuja kufuata huduma kwenye office za Umma!!
 
Ukiwa mwizi na kudhulumu wananchi unakufa mapema tena kifo cha hovyo kama lilivyokufa lile shetani lenu la Chato.
Limetuacha sasa hv tuna amani na furaha kama yote
Hata Yesu alikufa mapema,nalo hilo unalizungumziaje bro!!?
 
Rais Mama Samia ashukuriwe sana, amedhamiria kuwaheshimisha watumishi. Kutoka kwenye dhalala.

Hata hivyo ushauri wangu kwa Serikali iweke utaratibu maalum wa kuwakopesha fedha watumishi kwa riba nafuu ili wajikwamue kiuchumi kuliko kuwaacha Wana dhalilishwa kwenye MIKOPO umiza.
 
Wwe Kama ni Mtumishi wa Umma kua mkweli na Mungu anakuona, "hizo Mali ulizo nazo je ni kweli zinaendana na mshahara wako"!? Tukikuchunguza utaona Kama unaonewa kumbe wwe ni mpiga deal tu huko kwenye office za Umma!!
Mimi ni muuza duka.Mali zote ni halali.Kuhisi kila aliyepata ni mwizi nao ni uchawi.Ndiyo maana kila mti una bango la mganga wa jadi.
 
Ulikwisha fanya kazi kwa wahindi or wachina. ..hawapendi watu wavivu utafanya cku moja tu kesho hurudi. ...
 
Back
Top Bottom