Kwa uhalifu wa demokrasia unaofanywa na CCM, bado kinastahili kuitwa chama cha siasa?

Kwa uhalifu wa demokrasia unaofanywa na CCM, bado kinastahili kuitwa chama cha siasa?

ngusillo

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2019
Posts
1,064
Reaction score
2,017
Sote tumeshuhudia uvuruga wa demokrasia unaoendelea nchini chini ya usimamizi wa CCM. CCM imesimika sheria za kiimla na za kidikteta ambazo hata wakoloni hawakutunga sheria za kihalifu za kiwango kikubwa kiasi hiki.

Sote tumeona kwa macho na tumesikia kwa masikio katibu mkuu wa CCM akiikana misingi ya demokrasia kinyume na katiba huku akikitangaza chama chake cha CCM kuwa cha kidikteta. Ametangaza kuwa CCM itawatawala watanzania mithili ya mifugo yao.

Tunashuhudia CCM ikibariki matendo yote ya kujimilikisha nchi, kujitwalia mamlaka kwa njia za kihalifu kabisa, kuwanyima wananchi haki yao ya kuchagua viongozi, kuwabambika mataahira ya CCM kama viongozi kidikteta nk.

Kutokana na matendo hayo yaliyojaa uhalifu wa wazi na nia mbaya kabisa dhidi ya wananchi, napendekeza yafuatayo.

1. CCM litangazwe kundi la kihalifu, kidikteta na la kigaidi linalopaswa kuondolewa madarakani kwa njia zozote, kisha shughuli zake zote kupigwa marufuku.

2. Wanaoendelea kukaa na kuishabikia CCM watengwe rasmi na jamii ya watanzania. Waambiwe wachague moja, sauti za wananchi au matendo ya kihalifu ya CCM.

3. Mali zote za CCM zitangazwe kuwa mali zilizopatikana kihalifu. Hivyo yeyote atakayeendelea kuzitumia na kunufaika nazo, aandaliwe mashtaka ambayo atashtakiwa nayo tutakapoiondosha CCM madarakani hapo mwakani 2020.

Karibuni kwa mawazo huru.
 
Hiko chama kwa sasa inabidi kijibadilishe na kiitwe Chama Cha Majambazi
 
Back
Top Bottom