Kwa uhuni huu wa Fastjet haukubaliki

Mchokozi

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2012
Posts
215
Reaction score
29

Wana JF leo nimefedheheshwa sana na majibu yaliyotolewa na office za FastJet mara baada ya kuamka asubuhi na mapema na kufanikiwa kufanya booking online kwaajiri ya kusafiri kesho kuelekea Kilimanjaro, nilifanikiwa kufanya process zote na kisha kuprint karatasi ya uthibitisho niliyotumiwa kwenye mtando kana inavyoonekana hapa chini. Cha ajabu nilipfika office za Fastjet mkabala na office za British Council kwaajili ya kulipia Total Price TZS 75,040/= nilijibiwa na mhudumu aliyepo kulia ukiwa unainigia mlangoni kuwa nanukuu " Kuanzia asubuhi hii bei ni Tsh 154,000/= kwa maana hiyo booking yako ni batili? na siwezi kukuuzia, je haki iko wapi? hawa ni Fastjet au Fastjockes? naomba mnifahamishe haki yangu nitaipataje siku nyingine?




We have made the following booking for you:





Itinerary
Booking Reference: FATT3B Date of Issue:


CONTACT INFORMATION PASSENGER INFORMATION FLIGHT TICKET NUMBERS
MR WILLIAM T.W
MR WILLIAM T.W

DEPARTING:
Date Thu 10 Jan 13 All Times Local Flight-Number Cabin (book class)
From: Dar es Salaam Departure 10:30 FN 0151 (HK) Y (x)
To: Kilimanjaro Arrive 11:50
Info Flight 1: Check in closes 40 minutes before departure.
Rules Flight 1:
-Tickets are non-refundable.
-No name changes are allowed for any reason after ticket is purchased.
-A passenger is considered a no-show after the flight has departed, they miss the check-in desk closure or fail to board the aircraft within the required time.
-The ticket is non-refundable if unused.
-An administration charge applies to recover government taxes.
- Check-in closes 40 minutes before departure - All flight changes must be made 24 hours before the flight orignally booked - No change will be allowed within 24 hours before the flight -All fees and charges will be made in the currency of the original booking.
- Payment of change fee and ancillary products must be immediate for products and changes to be affected -Baggage is subject to a fee of $5 per bag.
-Only one bag allowed per passenger.
-You can carry 20kgs for the $5 fee.
-The passenger can pay for excess weight at a rate of $5 per kg up to a maximum of 32kgs.
- Fare differences apply per passenger and flight.
-Your new fare will be at least the fare you originally booked or may be more.
-You cannot change to a lower fare.
-No refund will be applicable if a lower fare is available.
-Fare difference is the difference (if any) between the fare orignally booked and the new fare available.
-The fare difference maybe substantial.
- Flight date changes are permitted subject to a fee and the applicable difference in the fare available.
-Origin and destination changes are not permitted.
- The passenger must make all date and flight changes 24hours before departure.
-After which time the passenger is committed to the reservation.
**Unaccompanied minor** Children aged less than 14 years are not allowed to travel unaccompanied, they can only travel with an adult.
If in doubt please ask for ID .
- Check in closes 40 minutes before departure - No name changes or refunds.


PRICING PAYMENT
Please pay for this booking at the Airlines office or airport ticket office by 09Jan2013 14:21 (DAR) otherwise the booking may be cancelled.
Price TZS 64000
Tax/Charge HY TZS 960
Tax/Charge TZ TZS 10080
Total Price TZS 75040
Agent Name: Agent ID: Agent Office:
 
no comment wacha waje wenyewe
umeshajaribu kutuma hii katika facebook wall yao?
 
Huu ni uhuni sasa!!!! They need to learn to be serious but sometimes wahudumu wa ofisini wanajitungia mambo yao wenyewe!!!! Take this issue up with the management, achana na hao uliowakuta hapo counter. Pole kwa mkasa huu uliokupata!!!!

Tiba
 
Serious hawa jamaa ni kama walikuwa wanatafuta jinci ya kuingia kwenye soko.. Maana sasa hivi kila mteja anaetaka huduma toka FastJet analalamika na haswa kwenye masuala ya nauli..! Na ukiongea na wafanyakazi wao wanasema ticketi za bei ya chini zinakuwa c zaidi ya 10 kwa kila safari..! Huu ni utapeli mkubwa..
 
ilinibidi nirudi kwa basi maana waliniudhi sana hawa watu go an return hapo mwanza wananicharge 380,000/=AKATI YAANI NILIJUA NIKIIBWA SANA NI LAKI MBILI ? SIPANDI TENA HIYO FAST JET KWA KWELI KILA WANAOKUJA WANAWAAMBIA TIKETI ZA KUANZIA 32,000/-ZIMEISHA
 
Nilitaka kushangaa kweli kabisa kibongo bongo ndo tushaula usafiri bei chee bila chenga, yani kukose mbwembwe na madoido kweli??? bite me
 
bado tupo mbali sana tunadanganyika kirahisi sana maskini
 
This issue is getting serious now, Lat week nilikuwa nasafirisha Familia yangu irudi Mwanza na isitoshe mtoto awahi shule, walipoingia ndani Airport wakaambiwa muda wa check in umekwisha na ticket haiwezi kutumika tena kwa next flight, ilibidi niwahi Ubungo wawahi kuondoka alfajili na mabasi ya Mwanza. hili swala linaniuma sana ila nashindwa kulifuatilia najuwa nitapoteza muda wangu bure.

Nilikata Go and Return ticket kutoka Mwanza kuja Dar na Dar to Mwanza halafu wao wananiambia aliyekosea kuandika muda wa reporting time ni Agent wa Mwanza na ninapaswa nikamlalamikie yeye, na yeye hajui kama mimi naishi Dar es salaam majibu ya kipuuzi kama haya unaweza kumtandika mtu nakozi ikawa kesi nyingine ndio maana nimeamuwa kujikalia kimya, mjinga mimi.
 

Nilitaka kushangaa kweli kabisa kibongo bongo ndo tushaula usafiri bei chee bila chenga, yani kukose mbwembwe na madoido kweli??? bite me
Ndio maana nina mgomo wa kununuwa king'amuzi mpaka mwezi upite ndio nitajuwa ukweli uko wapi, mtu ananunuwa king'amuzi halafu unaandikiwa no signal, yaani sisi ni mapoyoyo kuliko nchi yoyote, ukitaka kufanikiwa basi Tanzania ndio sehemu ya kuvuna ingawa wakweli ndio hawaaminiki.
 
Rudini Precision Air mpate huduma ya uhakika pasipo bugudha
 
Pole mkuu,

Wasiliana na management achana na huyo uliyemkuta counter.
Hiyo itinerary yako ni contract inayolibana shirika, una haki ya kuwashitaki wasipokupa ticket yako kwa bei waliyokupatia awali.

Record ya Easyjet shirika mama la Fastjet ni nzuri mkuu, sasa kama hawa Fastjet kwa kuwa wako Africa wanataka kufanya mambo kinyemela itakula kwao!
 

Duuh nivea.. Yaani walikuwambia ulipe kiaci hicho 380,000/=..?? Yaani mie nilikuwa na imani nao lakini toka nishuhudie mwenyewe nilipolazimika kukopa pale airport ili kumlipia bi mkubwa shs 171,000/= wamenitoka kabisa hawa.. Unless kama ninalipiwa na office.. ntakuwa ninapanda mabaci mie..
 

nilijirudia mie na basi la elfu 38,000 /mie natafuta hela kwa tabu then niwape tu alafu huko ndani wanakutembezea vibiscuti ununue tena ,na juice kabox kadigooo 8000/=hahahah nikawaambia mark my face sintapanda hii fast jet tena mimi.bora ndege nyingine ni ghali ila tamu tamu unapewa .jamani kama kuna mtu aliyewahi kupanda hiyo ndege kwa 32+vat isizidi 50,000/= aje atuambie hapa maana nimkwenda mwanza 190,000/=

VIPI sosoLISO HERI YA MWAKA MPYA RAFIKI YANGU MPENDWA.NIPITE HAPO OFICINI KWAKO KARIBU NA TWB UNIPE HATA 50 NISUKUME MWISHO WA MWEZI.
 
Last edited by a moderator:
- Fare differences apply per passenger and flight.
-Your new fare will be at least the fare you originally booked or may be more.
-You cannot change to a lower fare.

Mtoa mada ukisoma vipengele hivi kwenye booking yako utaona hawakukosea kukupandishia nauli. Wakati mwingine tuwe tunasoma haya mambo na kujiandaa kisaikolojia kwa yatakayotukuta baadaye. Hawa ni wahuni, lakini wamejihami kwenye taarifa zao za kwenye booking.
 
Du pole sana mpaka kufikia hapo sina hamu nao hata songea wasije kabisa nitapanda basi au tren YA TAZARA.
 
Tuheshimiane hapo kwenye blue, kama ni upoyoyo ni wewe acha ku-generalize
 
Labda mwenzetu unajuwa mengi, kwa upeo wangu mdogo ukimis Flight nijuavyo unatakiwa ulipe 25% kwa ajili ya next Flight, sasa hawa wenzetu wanatumia sheria ipi kwamba ukimis Flight basi imekula kwako na unakuta reporting time hukuandikiwa sahihi?
 
Sawa Mzee wa kwembe kati, hebu fafanua nini maana ya online booking?, mbona mashirika mengine hayana uhuni huo? kauli yangu haitabadilika hawa ni Fastjocke aka ni wahuni. Nimeshafanya hivyo kwenye Precision Airway na hawana tatizo kabisa
 
Poleni sana nyote mliojeruhiwa, kwa kweli inasikitisha sana na ukiona hivyo ujue WENYE NJAA WAMEINGIA.
Kinaniudhi sana kile kikasuku chao na maneno kama ya mtu asiye na meno, "FasterJet Smart Travel"

Iwe hivi FasterJet "Worst Travel"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…