Kwa ujinga huu, sitamuamini mtu hasa vijana

Kiukweli wakuu tunahitaji kazi na tuna shida ya kazi kama tunavyo post,

Lakini kwenye wengi tunatofautiana wengine ndo lengo ni kuiba, utapeli n.k

Tatizo linalo tuangisha ni uaminifu narudia kusema watz hatuna uaminifu

Mtu kama huyo nauli haifiki umetumiwa, then unaleta sababu za kuporwa kwa dunia hii ya sasa utaonekana mshenzi, na mwizi wa kizamani.....


Mnapopokea wageni waje na vitambulisho vya NIDA bila kucheka na barua za wadhamini wake ikiwezekana zipite kwa mwanasheria na nyaraka muhimu watu wamekuwa wezi wa hovyo

Mimi kwa kuniambia kaibiwa hata angefika dar angetafutiwa kitu kingne

Pole sana bruh
 
hii so chai ndugu,ymenikuta
Hiyo picha ni yake kweli? I mean ulipomuona ndie huyo huyo wa kwenye picha? kama ndiye basi Sambaza picha yake ukiambatanisha na RB kwenye mitandao yote kuanzia JF, FB, IG, X, Tiktok ndani ya masaa mawili tu ushapata full details, watafute wale watu wenye followers wengi wape kitu kidogo wampost, MUHIMU ambatanisha na RB yake.
 
N
 
Huyu kijana ni tapeli kweli, nilimpigia simu akaja nikamwona tukapanga nimpe kazi , baada nilipotaka kuongea na wazazi na kuonana anayeishi nae akaingia mitini.

nipigie tuongee , nikueleze zaidi yaliyonitokea na mimi kwa huyu kijana cause twaweza kumkamata tukishirikiana.
 

Attachments

  • Screenshot_20250125_143502.jpg
    111.7 KB · Views: 3
Mimi huwa nawashangaa watu eti unakuta mtu anaomba connection humu,yani nikupe connection kabisa mtu nisiyekufahamu?huku mtaani sina watu ninaowafahamu mpaka nikupe wewe wa mtandaoni?
 
Wewe jamaa mgeni hapa jf? Mbona matukio ya namna hii yanaripotiwa kila siku ulikuwa unayaona? au umejizima data? Ona sasa umepigwa kizembe! Wewe unakutaka na mtu mtandaoni unadhani ni mtu? Hapo mtaani ulikosa mtu? Sehemu unakohabudia umekosa mtu? Jamaa ndugu je? Heri nusu shari kuliko shari kamili! Zimwi likujualo halikuli likakwisha! Inamaana unayemjua hadi kwao au ndugu hatakama atakupiga, atakubakishia akiogopa ataenda wapi! Pole sana! Kama huna mke oa ukamfungulie hiyo biashara uue ndege wawili kwa jiwe moja (mbususu na kukuongezea kipato huku akikupa familia)
 
.
 

Attachments

  • downloadfile-322.jpg
    73.4 KB · Views: 3
Huyo jamaa anaitwa nani na anatumia ID gani humu?
 
Pole sana mkuu.
Kuna kitu ulishindwa kukisoma tangia mwanzo kabisa wa stori hii.

Ni mara chache sana jambo hilo kufanyika duniani ingawa lipo, yaani kutokea janga muda ule ule ama siku hiyo hiyo ya appointment.

Likitokea, jiulize mara mbili mbili, yawezakuwa ni dalili za mikosi ama unapewa ishara ya tahadhari kutoka 'juu', hata kama kwa sura jambo hilo ni jema yakupasa uachane nalo'!

Hiyo kwako ilikuwa ni ishara tosha kuanza kumfuatilia kwa ufasaha 'where abouts zake', kuna njia za kufuata kumwelewa kinagaubaga mtu 'kabila' hiyo.

Ujinga sampuli hiyo hufanywa pia na wanawake malaya, akihisi unamshobokea.

Utatuma na ya kutolea, lakini haji ana kublock ama anafunga na simu kabisa, akila zikiisha anakuibukia tena na statements kama za huyo mwizi wako.

Huyo mhalifu asiwaharibie vijana wahangaikaji wa ukweli ama wewe akakukatisha tamaa, maana wapo vijana watafutaji na waaminifu sana.

Katika kuweka vijana kwenye miradi yako, usidake mtu barabarani na kumuweka kama ulivyofanya.

Tumia mbinu wanazotumia wamiliki wa vyombo vya moto, gari ama pikipiki anapompa mtu kuendesha kwa mkataba wa kibiashara.

Mbinu hizo humbana anayesaini mkataba, hata kama ni mwizi lakini atajiheshimu kwenye mkataba unaombana moja kwa moja yeye na mdhamini wake.

Usimwamini mtu kwa muonekano ama pye pye pye za maneno matamu kutoka kinywani mwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…