Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Siasa ni gharama kwa hiyo ili chama cha siasa kiweze kufanikisha malengo yake lazima wanachama na wafuasi wake wajitolee kwa hali na mali.
Kwenye uchaguzi mkuu kama huu ambao chama kinahitaji kupata madiwani, wabunge na urais lazima kwa kila ngazi kiweke wakala. Wakala wa chama ndio mlinzi wa kura, kuweka wakala panahitaji gharam maana lazima umlipe posho, umpatie pesa ya chakula na ikiwezekana usafiri mana shughuli ya kuhesabu kura huwa inamalizika usiku wa manane.
Je, kwa ukata wa CHADEMA ambayo hata kuchapa mabango ya mgombea urais imekuwa ni tatizo,je kitaweza kuweka mawakala kama inavyohitajika? Maana kama jimbo lina vituo 60, hapo lazima kila chama kiwe na mawakala 60 ambao kwa gharama ndogo lazima uwape elfu 30.
Je, Chadema huu mziki watauweza? Hapa ndio msemo wa wahenga unakamilika kuwa ngoma usiyoiweza kuicheza usiingie kucheza.
N:B Kuna kiongozi alikwapua michango ndio maana Chadema ina ukata.