Kwa ulichomfanyia mdogo wangu, tutakutafuta tu ewe mwanamke

Kwa ulichomfanyia mdogo wangu, tutakutafuta tu ewe mwanamke

Ewe mwanamke Agnes kwa nini umeyafanya haya? Yani nimekukaribisha na kuwasululisha vizuri maugomvi yetu alafu nilipoondoka ukafanya haya? Uliomba msamaha wa nini sasa kama bado ulikuwa na kinyongo?

Ni hivi huyu mwanamke ni mpenzi wa mdogo wangu kwa muda wa mwaka mmoja lakini waligombana na kuachana kwa muda wa mwezi mmoja kwa sababu walikuwa na ugomvi, sasa juzi nikaitwa kwenda kuwasikiliza na kila mmoja akafunguka kivyake na mwisho wa siku ikaamuliwa yameisha na kila mmoja asahau yaliyopita, mwanamke akaandaa ugali tukala na mimi nikaendelea na shughuli zangu.

Cha ajabu leo nimepigiwa simu niende nimekuta mwanamke amebeba kilicho chake na kutoroka kusiko julikana na simu zake hazipatikani huku ameacha amejisaidia haja kubwa ya kutosha kwenye mabegi ya nguo za mdogo wangu, amekojolea kwenye unga, sukari, na amepaka mavi kitanda kizima!

Yaani mlango wote umepakwa kinyesi ukiingia tu unakanyaga kinyesi, diaba la maji kinaelea kinyesi! Yaani amekishusha hasa sijui alikula nini tu!

Wana jamiiforums tunaomba mawazo yenu tukimkamata huyu tumfanye nini?

Hapa tupo tunafua nguo, inasikitisha sana kwa umri na busara zangu nilizonazo kufua kinyesi cha mwanamke fulani tu ambaye nilimuheshimu kama shemeji!


Mdogo wako is not Man enough, kama umeamua kumsaidia ungemtunza huyo Mwanamke mwenyewe.
 
Kisa kinachekesha sana hiki, anyway, hapo huyo mwanamke kaamua kumkomoa tu huyo jamaa ila ole wake huyo mwanamke kama angefanya hivyo kwa msela mwingine katili angejichwa vibaya sana. Hawa ndio wale wanawake wanaouawa kinyama kwa majamaa zao. Duh! Huyo msela hata asihangaike kumtafuta mwanamke huyo mshenzi yasije yakamkuta mabaya zaidi akaishia jela na huyo mwanamke akaishia kaburini
 
Back
Top Bottom