Kwa ulimbukeni wa usajili wa Yanga na Simba, vijana wetu watatoboa?

Kwa ulimbukeni wa usajili wa Yanga na Simba, vijana wetu watatoboa?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Club za Simba na Yanga wameshindwa kabisa kubalance usajili wao na kujikita zaidi kupata first eleven ya wageni. Najiuliza aina hii ya usajili itawasaidiaje vijana wa Tanzania wanaopanga kutoka kimaisha kwa fani ya mpira? Lini wataonekana na kutoka?
 
Kama kuna wachezaji bora watanzania bado watacheza tu katika timu hizo hizo, wasipocheza basi ujue wamezidiwa uwezo na hao wa nchi so hakuna wa kumlaumu, nikupe mfano mmoja mwaka fulani simba walishawahi kuwa na golikipa mmoja nakumbuka jina kama sikosei Angban yule kipa ata uyu Kakolanya alikuwa alikua bora ila kulingana na hali ya kiuchumi ilibid tu acheze kama ingekua miaka hii ata bench asingekaa ninachotaka kusema ni kwamba sio tu hizi timu zinasajil nje ila pia wanatafuta wachezaj bora kuliko hawa wote kwaiyo apo ni jukumu lao wachezaji wazawa kujielewa maana kwa hawa wachezaji wetu ata tukisema wasajiliwe wageni wanne bado timu zetu zitakua mbovu kuanzia vilabu mpaka taifa uko mwanzo waliruhusiwa watano wa nje je wazawa tulifanya nin ,nazan hii changamoto itawasaidia zaid wazawa maana tukimpata mzawa akacheza simba yanga au azam bas atakua na kiwango bora kwel kwel so ata timu ya taifa itaisaidia
 
Vijana wanaocheza timu ndogo wajitume na wawe na Malengo,waziangalie Simba na Yanga kama sehemu za kupita kwa ajili ya kwenda timu kubwa za Misri, Morocco na Tunisia au South Africa na baadaye waende Ulaya, tatizo lao wakifika Simba au Yanga wanabweteka mfano Mkude na Ajibu

.Ajibu ana kipaji Sana ,kama angekubali kwenda Mazembe leo hii angekuwa mbali.

Simba na Yanga sasa hivi zitavutia sana wachezaji wa nje maana wanaziona kama fursa ya kutokea.

Waige mifano ya Luis na Chama Hawa walikuwa wanacheza kwa juhudi kubwa na ndiyo maana wakaonekana,hata Hawa wageni waliosajiliwa Sasa hivi Simba wenye umri mdogo mwakani wanaweza wakaondoka.

Kwa kifupi hizi nafasi 4 za kimataifa zinaweza kuwanufaisha zaidi wageni kuliko wazawa ni wakati wa wazawa wajitume,wamwage jasho uwanjani ili waonekane kimataifa.
 
Vijana wanaocheza timu ndogo wajitume na wawe na Malengo,waziangalie Simba na Yanga kama sehemu za kupita kwa ajili ya kwenda timu kubwa za Misri, Morocco na Tunisia au South Africa na baadaye waende Ulaya, tatizo lao wakifika Simba au Yanga wanabweteka mfano Mkude na Ajibu.Ajibu ana kipaji Sana ,kama angekubali kwenda Mazembe leo hii angekuwa mbali.
Simba na Yanga sasa hivi zitavutia sanna wachezaji wa nje maana wanaziona kama fursa ya kutokea.
Waige mifano ya Luis na Chama Hawa walikuwa wanacheza kwa juhudi kubwa na ndiyo maana wakaobekana,hata Hawa wageni wanaosajiliwa Sasa hivi Simba wenye umri mdogo mwakani wanaweza wakaondoka.
Kwa kifupi hizi nafasi 4 za kimataofa zinaweza kuwanufaisha zaidi wageni kuliko wazawa ni wakati wa wazawa wajitume,wamwage jasho uwanjani ili waonekane kimataifa.
Ajib alikosea alipotoka Simba mara ya kwanza asingeenda yanga angeenda nje ila kurudi kucheza yanga akawa anarudi nyuma hatua milioni moja
 
Club za Simba na Yanga wameshindwa kabisa kubalance usajili wao na kujikita zaidi kupata first eleven ya wageni. Najiuliza aina hii ya usajili itawasaidiaje vijana wa Tanzania wanaopanga kutoka kimaisha kwa fani ya mpira? Lini wataonekana na kutoka?
Unapokuwa kwenye biashara huwa hakuna tena kuangaliana kwa jicho la kijamaa au huruma huruma. Hapo timu inasajili ili ifanye biashara maana hata wachezaji nao wanazikamua fedha klabu kweli kweli. Ukisema wafanye kubalance, maana yake waache kwa makusudi wachezaji wazuri wa nje ya nchi ambao wamo ndani ya uwezo wao, ili eti wawafikirie wachezaji wa ndani! Mpira wa zamani klabu zilikuwa haziingii gharama sana, watu walisajiliwa kwa kupewa kitanda, lakini sasa bila 100M haumsainishi Aishi Manula, sasa unadhani fedha zitatoka wapi? Inabidi klabu ziingie gharama zaidi kupata wachezaji watakaowauza tena kwa gharama kubwa zaidi
 
Vijana wanatakiwa wakakuzwe kwenye timu km mtibwa, costal union, mbeya city na timu nyingine ndogondogo ili wajitume kufika Simba na Yanga. Sio Simba na Yanga ikakuze vipaji vya vijana, Mpira umebadilika hata Barcelona walishaachana na hizo fikra
 
Kibu Denisi
Yusuf Mhilu
Ni muda wenu wa kujituma na kuongeza thamani zenu.
Muweze kuonekana mkapige pesa nje ya nchi.

Cletus Chama na
Miquissone
Ni mfano mzuri kwenu kujifunza namna ya bora ya kucheza kwa bidii uwanjani.

Kazi kwenu.
Na Wazawa wengine pia
 
Club za Simba na Yanga wameshindwa kabisa kubalance usajili wao na kujikita zaidi kupata first eleven ya wageni. Najiuliza aina hii ya usajili itawasaidiaje vijana wa Tanzania wanaopanga kutoka kimaisha kwa fani ya mpira? Lini wataonekana na kutoka?
Mbona Fei Toto anawapiga gap sana Wachezaji wa Kigeni. Wajitume tu ndio salama yao.
 
Mbona Fei Toto anawapiga gap sana Wachezaji wa Kigeni. Wajitume tu ndio salama yao.
Sema kitu kingine ni wachezaji wazawa wanakosa watu wenye mipango nyuma yao, nikimaanisha Managers wazuri, just imagine yule manager wa Faris Mussa na Metacha Mnata anaitwa jemedari said, daah it is very Unprofessional
 
Club za Simba na Yanga wameshindwa kabisa kubalance usajili wao na kujikita zaidi kupata first eleven ya wageni. Najiuliza aina hii ya usajili itawasaidiaje vijana wa Tanzania wanaopanga kutoka kimaisha kwa fani ya mpira? Lini wataonekana na kutoka?
Sasa hapo kosa ni la Yanga na Simba! Au ni la Wallace Karia na Bodi yake ya Ligi kuruhusu wachezaji 12!!

By the way, hao vijana wenyewe unao wapigania ni hawa akina Ibrahimu Ajib na Jonas Mkude wasio jitambua, au kuna vijana wengine?
 
Club za Simba na Yanga wameshindwa kabisa kubalance usajili wao na kujikita zaidi kupata first eleven ya wageni. Najiuliza aina hii ya usajili itawasaidiaje vijana wa Tanzania wanaopanga kutoka kimaisha kwa fani ya mpira? Lini wataonekana na kutoka?

hebu tuone hao wazawa wanapitia wapi katika safar ya soka

1. anaonekana kwenye ndondo au anajileta mwenywe kwenye yale majaribio ya usajili wa under 20. team inamchumkua hapo yuko around 18/20..

2. akiwa vizur anakaa team B miaka miwili nitatu anaingia team ya wakubwa. anaanza kucheza league anashindana na wachezaj wa team kama
za ndanda, singida, mbao.. team zinazoendeshwa kwa kuunga unga.. katika league ambayo Bingwa anachukua 80m au kusiwe na zawad kabisa. katika league ya viwanja vibovu.. katika league team hazina structure ya kuvumbua vipaji achilia mbali viwanja vyao wenyewe

then umuingize huyu Mashindano ya CAF utegemee akupeleke walau makundi au robo? angalia case za wazir junior, Nchimbi, Ajib na wengineo

Inabid uchague moja.. mnataka League yenu iendelee kuwa league ya ridhaa ama mhamie kwenye professional league

ili ligi yenu itambulike ni professional, inabid muwe na viwanja bora, wachezaji bora, management bora za club na vyama vya soka bora team za vijana bora na miundo mbinu yote kwa ujumla

sasa ili tufike huko ni lazima tuwekeze.. lakin hatuwez kuanza kuweka fedha kwneye viwanja na academy bora bila walau kuwa na jinsi ya kurudisha nusu hasara.. tukiweka fedha huko.
huku tunategemea wachezaj wa ndan tutasubir miaka mingi..

jiulize Azam kweka pesa ndefu leo kwenye league na huko yanga, je sababu ni mzalendo sana au? jibu hapana team zimejiuza na kujiuza huko ni kuwa na wachezaji wa kimataifa

sasa hapa ni kuanza na kuchukua wachezja bora kutengeneza jina la club zetu nje . waje tuwauzie fedha tunayopata tuigawe ingine iende kwenye miundo mbinu hiyo niliosema hapo juu ingine tunawekeza kwenye wachezj wengine bora..

namna hiyo taratibu tutaanza kupanda .. miaka
kadhaa baadae tutakuwa na viwanja na miundo
mbinu bora na wafadhili wa ligi wataweka fedha kubwa zaid sababu tushajiuza.

then mwisho tutasema sasa tuanze kutengeneza kina messi wetu maana hapo tayar tuna uwezo na facilities pia hatutegemei kumuona mchezaj kwenyw ndondo au aje kwenye majaribio ya jumuia ndo tumsajir wala hana ethics za kuwa proffesional player.. kashakauka hawez kukunjika labda mmoja katika kumi

vinginevyo mng'ang'anie kubak na wazawa mtegemee fluke za vikos vya dhahabu vinavyokuja baada ya miaka 20 kama kile cha simba 93, na cha Yanga enz za kina lunyamila
 
Back
Top Bottom