Kwa ulimwengu wa leo inafaa mtu masikini kuwa kiongozi?

Kwa ulimwengu wa leo inafaa mtu masikini kuwa kiongozi?

Mishenyi

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2019
Posts
463
Reaction score
750
Binafsi sipendelei mtu aliyeshindwa kujipambanua mwenyewe katika uchumi wake kuwa kiongozi wa watu japo anaweza kuwa na sifa kadhaa kama uadilifu nk.

Lakini kiongozi anatakiwa kuwaongoza watu kutoka hali duni kwenda hali nafuu au ikiwezekana kuwa matajiri hapa inabidi yeye mwenyewe awe ameshapambana na kufika ngazi ya juu ya kipato,atajua kuoanisha mbinu alizotumia kufanikiwa na kuzi apply kwenye ulingo wa uongozi wake hivyo kufanikisha njia mbadala za wananchi kijikwamua

Maskini ni mtu aliyeganda kimawazo japo anaweza kuwa mwadilifu hivyo kushindwa kuona fursa wa wananchi wake kujikwamua hapa atakutana na watoto wa mjini watamwingiza kingi nae kwa kuwa haoni mbali anatoa maamuzi ya ajabu huku wahuni wakinufaika na maamuzi hayo!!!


Kuna watu husema ukipewa nafasi kuchagua kiongozi na ukamchagua maskini unakuwa umejifungamanisha na umaskini wake.

Jipambanue kwanza binafsi alafu ndo utushawishi tukuchague tukiwa na imani kwamba unaona mbali maana ulikwaisha pambana ukafanikiwa.
 
Maskini hapaswi kupewa madaraka makubwa..
 
Nimesoma heading tu, jibu hapana
 
Back
Top Bottom