Uchaguzi 2020 Kwa umati uliofurika leo Viwanja vya Matogoro Mjini Tandahimba, ni wazi hakuna wa kumzuia Tundu Lissu kuwa Rais

Wakazi wa mji wa Tandahimba na vitongoji vyake walikusanyika kwa wingi kwenye viwanja vya shule ya msingi Matogoro ili kumpokea mgombea urais anayeiwakilisha CHADEMA Mh. Tundu Lissu.

Kwa hakika umati ulikuwa mkubwa haijapata kutokea. Hamasa ilikuwa juu sana.

Huku watu wakiendelea kumiminika, ikaletwa taarifa kwamba Tundu Lissu hatafika kwenye hadhara hiyo kwani hana kibali cha kufanya mkutano wa kampeni katika jimbo la Tandahimba.

Kwa taarifa hiyo wananchi walitakiwa kutawanyika mara moja kurejea makwao. Ila ilichukua muda wa nusu saa watu kuondoka toka viwanjani hapo kwani wengi wao walisikika wakiilaani serikali ya CCM na wengi wao waliapa kumchagua Lissu kwa kishindo kikuu ifikapo tarehe 28 Oktoba mwaka huu.

Nadiriki kusema kwa umati ulioshuhudiwa viwanjani hapo leo, hakuna wa kumzuia Lissu kuingia Ikulu ya Chamwino.

Credit: kwa rafiki yangu aliyeko Tandahimba, kwa taarifa.
Cha kushukuru Mungu ni kuwa hata jeshi la wananchi sasa wameanza kuunga mkono wananchi!
 
Haki uhuru, haki na maendeleo vimeeleweka.

Kipindi kilichobaki tuwekeze kwenye kutafuta na kuweka mikakati kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki.

Haki na uhuru unaozaa amani ni vyetu hatuna wa kumwekea rehani.
 
Sijaona mgombea wa kumshinda Magufuli.

Wapinzani wajiandae kwa kipigo October 28th

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
nani akubali chama kimfie mikononi? watahakikisha wanashinda kwa namna yeyote ile
 
Back
Top Bottom