Kwa umri wa miaka 65+ pesa haitakiwi tena kuwa kipaumbele katika maisha yako

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Kuna umri ukishafikisha pesa haitakiwi tena kuwa kipaumbele chako. Kwa sababu, kula yako inakuwa ni ya kawaida (kulinda mwili uwe na afya), usafiri ni wakawaida (miguu ipate mazoezi), pakulala pa kawaida (inawezekana hutoweza kupanda ngazi gorofani), matibabu ni ya kawaida(dawa zisizo na makemikali) n.k.

Mfano una miaka 65+, unatafuta pesa nyingi ya nini; kama una uhakika wa kupata elfu 30 kwa siku, we rizika na hicho kipato, kwa sababu ni umri wa lala salama. Tusitafute pesa nyingi kwenye umri huo, wakati hatutoweza kuzitumia.

Tujifunze kutosheka kutokana na umri tulionao.​
 
Unajua katika umri huo pesa ndiyo itakayo kupa sauti kwenye vikao vya ukoo?

Unajua kwanini baadhi ya wazee wa umri huo huitwa wachawi au wazee wa hovyo?

Kuna utofauti kati ya kufanya mazoezi na kutaabika.!

Umri huo unatakiwa uwe na gari kali yenye shock absorbers imara ili usiumie mgongo.
 
Ukifika miaka 55 tafuta shamba kimanzichana jenga nyumba ya kawaida upate upepo wa kawaida usife kwa presha za katikati ya jiji na mbigwa mbigwa za dunia
 
Ulishawahi kujiuliza swali, kwanini wazee wengi vijijini wanaishi miaka mingi?
 
So Samia yupo age ya lala salam
 
Upo sahihi kwa minajili ya maisha ni kula na kulala

But at that age you need more money kuiona dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…