tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Mengi amefariki akiwa na miaka 75 na alikuwa akisaka pesa kuliko kawaida.Kuna umri ukishafikisha pesa haitakiwi tena kuwa kipaumbele chako. Kwa sababu, kula yako inakuwa ni ya kawaida (kulinda mwili uwe na afya), usafiri ni wakawaida (miguu ipate mazoezi), pakulala pa kawaida (inawezekana hutoweza kupanda ngazi gorofani), matibabu ni ya kawaida(dawa zisizo na makemikali) n.k.
Mfano una miaka 65+, unatafuta pesa nyingi ya nini; kama una uhakika wa kupata elfu 30 kwa siku, we rizika na hicho kipato, kwa sababu ni umri wa lala salama. Tusitafute pesa nyingi kwenye umri huo, wakati hatutoweza kuzitumia.
Tujifunze kutosheka kutokana na umri tulionao.
Tafuta pesa mkuu; pesa hazina mwisho. Hata ukifa leo utawaachia urithi watoto au wajukuu.