Kwa urefu huu nawashauri Zitto, Lissu na wengineo msitie mguu

Sasa Amiri jeshi mkuu anatangaza vita dhidi ya watu wake mwenyewe au?

Maana kama unadhani majeshi yatamlinda kwenye ajenda yake ya kutoheshimu katiba na sheria basi unamdanganya
 
..yalikuwa maandamano ya ile taasisi ya kutetea haki za binadamu Tz.

..nimeshakupa hint sasa na wewe unapaswa kujiongeza.
Dr Slaa aliwahi kuandamana ili kupigania haki ya chama na raia, kilichomkuta hakikuwa siri kila mtu alijua au anajua. Prof Lipumba pia aliwahi kuandamana kwa sababu zinazofanana na za kina Dr Slaa kilichomkuta na yeye kila mtu alijua au anajua kuwa alivonjwa mpaka mkono. Sasa inawezekana vipi mtu aina ya Lisu aandamane bila kujua kilichomkuta! Anyway mkuu naheshimu ulichoandika lkn sikubaliani na ww.
 
Siku akienda Mzena urudi tena kutupa taarifa
 
Haya Mambo hayajaanza leo mwendazake alikuwa nayo na akaenda zake .

Hata Huyo nae ataendazake yeye sio wa kwanza .


Nachoona anajiribu kuonesha umwamba wake tu .


Muda utakuwa muamuzi mzuri
 
Sasa Amiri jeshi mkuu anatangaza vita dhidi ya watu wake mwenyewe au?

Maana kama unadhani majeshi yatamlinda kwenye ajenda yake ya kutoheshimu katiba na sheria basi unamdanganya
Wanaotangaza vita ni wale waliosema watamnyoa kwa wembe wakati hawana hata hela ya kununulia huo wembe. Lkn kingine hauwezi kuamua kufanya mkusanyiko wa watu bila kufuata utaratibu wa kisheria kama vile kuwa na kibali nk.
 

..kwasababu hakujeruhiwa na polisi siku ya maandamano ndio inakufanya uamini hayakufanyika?

..hivi umetafuta hizo clip ukazikosa, au unaogopa kuzitafuta kwasababu zitakuwa kinyume na ulichoaminishwa?

..na kama unawataja Dr.Slaa na Prof.Lipumba kwa kupigwa na polisi hata Lissu alipigwa na Polisi wa Tarime kipindi cha JK. Tukio hilo lilitokea wakati akiwatetea wachimbaji wadogo wadogo waliokuwa wakiteswa na kudhulumiwa na serikali.

..Na wakati wa kampeni za 2020 msafara wake ulishambuliwa na Polisi maeneo ya Nyamongo Tarime.
 
Ok mkuu nimekupata.
 
Kwanza jiulize kwa nini Zitto yuko kimyaaa! Zitto huwa anasumbuliwa na mambo ya dini. Uwepo wa Samia yeye anaona naye yuko madarakani. Ndo maana hawezi hata kusema juu ya makato ya miamala wakati siku zote alikimbilia mitandaoni kupata majibu ya kiuchumi, ili ajidai ni mchumi.
 

Ngoja mungu aje na 3rd version tuone urefu wa kina
 
Ngoja mungu aje na 3rd version tuone urefu wa kina
Mbona mungu tayar ashaanza kumsogelea mwenyekiti. Juzi kati kaanza na kaka yake, mwenyekiti akakataa watu wasikusanyike msibani. Hii inaonesha kuwa mtoa roho ashasogea karibu na familia ya mwenyekiti. Kuna msemo unasema "ukiona mwenzio ananyolewa na ww tia maji".
 
Wewe ni Mr Dudumizi hasa.
Tanzania itafaidika ukibaki huko huko kwenye uDudumizi wako, vinginevyo unatias hasara tu kwenye nchi hii.

Hata hivyo, muwepo madudumizi au la, hakuna kitakachozuia mabadiliko yatokee nchi hii. Wakati umefika sasa mabadiliko hayo kuwepo.

Mnapenda sana kuvitanguliza vyombo vya usalama na ulinzi wa wananchi kama ndivyo vyombo vya kuendelea kuwabakisha nyinyi kwenye madaraka kwa nguvu.
Hivi vyombo ni vya wananchi, hatimaye wenye vyombo vyao wataamua viwafanyie kazi wao na siyo kuwalinda nyini wakandamizaji wa wananchi hao.
 
Unamaanisha Mh.naye ni dictator kama CCM wenzake?Hivi hicho kina cha Maji alikitengeneza huyo anayetukataza tusikipime.Hivi CCM na serikali yake inapambana na Raia wake wanaodai Haki zao?Wanafikiria nani atakuwa mshindi mwisho wa Siku?
Historia inatufundisha kuwa Nguvu ya Umma/Wananchi haijawahi kushindwa na watawala.
Tunachohitaji ni Katiba ya Wananchi na hilo siyo hisani.
 
Hata mwenyekiti wenu ametumia red brigedia ya chama chake kuilinda katiba aliyoitengeneza mwenyewe ili asitoke madarakani. Nchi hii ina mamb mengi ya msingi yanayohitajika kufanyiwa wananchi, achana na hiyo katiba ambayo wafaidika wakubwa ni wanasiasa wa hovyo wenye lengo la kujaza matumbo yao kupitia hela watazolipwa kweny vikao vya katiba. Watanzania wa miaka ya leo wengi ni wajanja na wenye uelewa wa hali ya juu japo wapo wale bendera fuata upepo na misukule kadhaa inayotumiwa kama ngazi na wanasiasa ili kufikia malengo yao.
 
KIONGOZI WA KUNDI LA MORON
 
Nilitaka kukueleza kuwa kawaida yangu si kujibishana na watu kama wewe, lakini itanibidi nikujibu tena kwa mara nyingine kwa haya uliyoandika hapo juu.

Unachosema hapa ni kwamba katiba iliyopo inawanufaisha CCM kuendelea kuhodhi madaraka hata kama wananchi hawataki.
Kwa hiyo kwa maoni yako hilo ni bora zaidi, kwa vile CCM wananufaika na katiba hiyo.

Haya ni mawazo ya kiDudumizi hasa!

Sina muda wa kuendelea na wewe.
 
Serikali inakunyima haki ipi mkuu? Ushawahi kuzuiwa kutoka nje ya nyumba yako? ushawahi kuzuiwa kwenda hospital ukapate tiba yako? ushawahi kukatazwa usipande basi au kutembea na gari yako? Ushawahi kukatazwa kula chakula chako? I mean hiyo haki unayozungumzia hapa inahusu zaidi masilahi ya wanasiasa katika harakati zao za kutafuta kupiga hela kupitia vikao vya katiba kama ilivyotokea kwa ile katiba ya mwanzo. Ww kama mwananchi wa kawaida unatumiwa tu kama daraja na wanasiasa hao ili wafikie malengo yao. Ila swala la kunyimwa haki raia kama raia halina mashiko.
 
Wananchi gani unaowazungumzia hapa? Labda unamaanisha wananchi ambao ni chadema. Na hao nchini hawafiki hata milioni 5 katika nchi yenye raia milioni 65.
 
Bi Mdashi aingie tu naye kwenye orodha ya wauaji, chinjilia mbali huyo MBOWE na wenzake isionekane hata mifupa Kama ilivyotokea kwa Ben Saanane.
Hamna atakaye kuuliza
Angalia hili jinga kwa hali hii tz. Bado sana majinga kama haya sizani kama yatakuja kutoweka??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…