Kwa USA, Ruto anachukuwa nafasi ya Ramaphosa?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
William Ruto wa Kenya kachukuwa nafasi ya Cyril Ramaphosa wa South Africa baada ya South Africa kujiunga na Urusi na China kwenye Bricks. Hii imetoa mwanja kwa Marekani kuangalia kiongozi mwingine. Marekani imeangalia kiongozi mwingine kwa vigezo ambavyo Tanzania haina kikubwa demokrasia na katiba nzuri.

Pamoja na Mama kujitahidi sana bila katiba mpya na mabadiliko makubwa kwenye sheria na demokrasia sisi Tanzania tutakuwa wafukuza mwenge na sio waongozaji. Maana majirani zetu wamaamua udikteta kama Rwanda na Uganda na wengine demokrasia kama Kenya, Zambia na Malawi. Tanzania haieleweki eleweki na ndiyo maana mpaka leo hatuko strategic na nchi yeyote kubwa zaidi ya hawa waarabu ambao wanacholeta hatujui ni nini maana hawaleti ulinzi, teknologia wala mtaji wa maana. Mbugani hakuna wekezaji wowote wa wale waarabu, ardhi waliopewa hatujui ni ya nini, bandari mkataba wa siri!. ..

Kwa wale waliokuwa hawajui faida ya katiba mpya ni hii sasa. Katiba mpya inaleta uongozi bora na uaminifu wa mfumo ambao unaleta uwekezaji na ushirikiano na nchi kama USA na hii inaleta kazi na maendeleo. Mfano wa ushirikiano wenye mafanikio wa Marekani ni kuanzia 1945 ni Ujerumani, Japan na South Korea. Angalieni hii mifumo ilivyo wapaisha. Mama unapendeza lakini ukitaka heshima kubwa katiba haikwepeki
1716755536841.png
 
BRICS ni kifupisho cha nchi tano BRAZIL, RUSSIA, INDIA, CHINA NA SOUTH AFRICA.
 
Umewahi kuishi Kenya hata wiki moja!?,katiba mpya imewasaidia nini raia wa Kenya!?,mara nyingi sisi watu weusi huwa tunatafuta visingizio maishani vya kufeli kwetu, Kuna watu mmewamezesha huu upumbavu wa katiba mpya, mtu anamaliza chuo anakosa ajira naye anaingia kwenye mlolongo wa kulaumu katiba. Shida yetu sio katiba mpya, hata iletwe katiba gani bila watu kuacha u selfish wa kujilimbikizia mali hatutakaa tupige hatua. Huyo Ruto mwenyewe kajilimbikizia mali vibaya mno. Machoni ni kama watu ila moyoni hawana utu hata aslimia 1.
 
View attachment 3000260
Mama alipendeza sana hapa. Ni uzinduz wa albam ya mmakonde?
 
Sisi ni taifa huru. Madollar makubwa hayawezi kutuchagulia mtu wakushilikiananae. CYRIL RAMAPHOSA.
 
Nadhani wengi wenu mlikuwa wadogo kwenye miaka kabla ya 80s!
Nasema hivyo kwa sababu kabla ya wakati huo Kenya ilikuwa kibaraka mkubwa wa mabeberu/wakoloni. Wakati sisi tunapambana nchi za kusini mwa Africa zipate uhuru (Mozambique, Angola, Namibia, na SA), Kenya walikuwa wasaliti wetu wakuu kwenye ukanda huu wa central and Southern Africa! Wao ndio walikuwa marafiki wakubwa wa wakoloni, na hawakujihusisha kabisa kusaidia hizo nchi zipate uhuru. Kwetu sisi wa zamani kidogo, hatushangai Kenya kurudia nafasi yao ambayo ilififia kidogo kuanzia 90s mpaka hivi karibuni.
Tusishangae kuona tena Kenya wanatumiwa na huyo beberu kuhujumu na kupinga kujitanua kwa mataifa mengine ktk ukanda huu, hasa yale ambayo hayatakubali kuwa vibaraka wa USA/UK hegemony!
 
Umewahi kuishi Kenya hata wiki moja!?,katiba mpya imewasaidia nini raia wa Kenya!?,mara nyingi sisi watu weusi huwa tunatafuta visingizio maishani vya kufeli kwetu, Kuna watu mmewamezesha huu upumbavu wa katiba mpya, mtu anamaliza chuo anakosa ajira naye anaingia kwenye mlolongo wa kulaumu katiba. Shida yetu sio katiba mpya, hata iletwe katiba gani bila watu kuacha u selfish wa kujilimbikizia mali hatutakaa tupige hatua. Huyo Ruto mwenyewe kajilimbikizia mali vibaya mno. Machoni ni kama watu ila moyoni hawana utu hata aslimia 1.
Hatushindani na kenya hapa. Hatu model katiba yetu ifanane na kenya au kuwaiga kenya. Tuna model kufiti mahitaji yetu ya karne hii.
Katiba yeti ina madhaifu mengi hatupo kwenye 70s and 80s anymore, tupo 21st century
 
Back
Top Bottom