Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari za asubuhi wana JF wenzangu.
Ndugu zang baada ya kufuatilia kwa makini utendaji wa kazi unaofanywa na jeshi la polisi, pamoja na mbinu mbalimbali zinazotumiwa na makanda wa jeshi hilo katika jitihada za kupambana na uhalifu nchini, hasa kwa mkoa wenye uhalifu mwingi kama Dar es Salaam.
Kwa kweli nilikuwa nashauri kwamba ikitokea IGP Simon Sirro amemaliza muda wake wa utumishi katika jeshi hilo kwa mujibu wa sheria, basi ikimpendeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mama Samia Suluhu Hassan amteuwe kamanda Jummane Muliro kuwa IGP mpya wa jeshi hilo, ili kushika nafasi itakayoachwa na Sirro.
Huyu kamanda amekuwa akipambana na uhalifu kwa njia zote za kijeshi, na mapambano yake huwa yanaleta ahueni kwa wananchi. Kamanda Muliro ni mwiba mkali kwa wahalifu wa aina zote nchini, na kamwe hajawahi kushindwa na wahalifu.
Nawasilisha mawazo huru.