Uchaguzi 2020 Kwa ustawi endelevu wa taifa: Tume iongezewe kazi ya kuhakiki na kurekebisha mapungufu kwa kushirikiana na wagombea

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Uchaguzi ni suala nyeti.

Lazima Tume ihakikishe yenyewe inawashauri wanaokosea kurekebisha.

Kwa Lugha nyingine udhaifu wa form usiwe kosa la Mgombea bali TUME.

Hivi inguwaje kama nchi ingemkosa JPM na LISSU kwenye uchaguzi kisa eti wino, au Picha au sahihi au muandiko kwa mfano.

Tusibobee kwenye asilimia 20 inayoweza kuleta madhara 80%. Itashangaza sana mwaka 1995 Wagombea waliweza kujaza bila kukatwa hivi, Leo dunia ya kisiasa zaidi 2020 eti watu hawawezi kujaza form. Taarifa hii ikiifikia dunia ni aibu kwa taifa.

Sisemi hii kwa Sababu ya Wapinzani. Bali zaidi kama ingethibitika JPM alikosea kujaza form hivyo akakatwa ujumbe huu ungeliabisha taifa pakubwa, na leo wanatushangaa.

NEC hata kama mnatuhumiwa kwa kutokuwa huru, ila hili la kujaza form mlifanyie marekebisho hata baada ya Uchaguzi huu.
 
Umeongea jambo la msingi, dhumuni la uchaguzi ni watu kupata wawakilishi wao na si kuoneshana umahiri wa kujaza makaratasi.

Kama katiba imeweka moja ya kigezo cha mbunge/diwani ni kujua kusoma na kuandika, ni jambo la ajabu sana kuwaengua wagombea hao hao kwa kukosea kujaza fomu tu.

Kwa upande mwingine sio kosa mtu kusaidiwa kujaza fomu, yaani uwanyime watu haki ya kupata muwakilishi wa maana kisa yule mwingine kajaziwa fomu vizuri?
 
Nafikiri pia ni kudai jiwe ajiuzulu manake ameleta ushenzi mkubwa nchini.
 
Jaji mwenye akili na maadili High Court alishaamua ni kinyume cha sheria, taratibu, na maadili kwa wakurugenzi kusimamia uchaguzi na sababu za kisheria zikatolewa. Rufaa ikakatwa, serikali "ikashinda"; matokeo yake ndio kama hivyo.
 
Hapa hadi watu waje waamke usingizini, wapiganie haki zao, watoane damu ndo mabadiliko yatawezekana!

Huko Zanzibar huweza kikanuka wakati wowote. Chuki iliyopandishwa ni zaidi ya mbwa na ngedere.
 
Kwa kadiri chama tawala (chama cha demokrasia bandia) kinavyokuwa na kundi kubwa la viongozi wenye shahada za uzamivu, ndivyo ambavyo wanakuwa na maamuzi ya hovyo kuwahi kutokea. Hili kundi la "elites" ndani ya chama ni watu waliokuwa ni wanafiki wasio kuwa na kipimo cha kuwaelezea.

Misimami ya wengi wao walipokuwa wahadhiri wa vyuo tofauti, na tena kupitia ktk "thesis, periodicals, journals & articles" zao walizoandika wenyewe ama kwa kushirikiana na wanataaluma wengine, huwezi kuamini ndiyo watu walewale ambao wapo upande wa watawala dhalimu, na wakiyatenda kwa umahiri mkubwa yaleyale maovu ambayo walituaminisha kuwa wanayapinga kwa hali zote.

Ni ajabu na kweli kuwa na Rais wa nchi kutoka ktk kundi hili, na tena akiwa na Katibu Mkuu wa chama chake naye akitokea kundi hili, wote kwa pamoja wakishikwa na woga ktk kukabiliana na wapinzani. Wanaona ni faraja kutoa maelezo ya hovyo kabisa ili kuwaengua wagombea kutoka vya upinzani, kwa nia ya kupata ubwete wa ushindi.
 
Ingelikuwa ni tume ya Taifa ushauri wako ungepewa nafasi na tija yake ingekuwa tunu kwa taifa lakini si kwa tume hii...
Mkubwa mmoja alijikurupua dakika za mwisho na kusema "...walioenguliwa wameenguliwa kwa makosa warudishwe!!!" Ilishakuwa too late na hakuna kemeo wala karipio lililofuata!!
Tunajenga nchi ya haki huku tukizikanyaga haki za wengine!!
 
Naamini hata CCM wamekosea sana tu ila kwao kombe linafunikwa!

Uchaguzi umegeuka wa kutafuta bingwa wa kujaza fomu badala ya mwakilishi wa wananchi!

Nadhani forms are just tools to assist in consolidating personal informations... Sidhani kama wagombea wanalazimika kufanya written exams au matriculations ndo waruhusiwe kushiriki uchaguzi...
Huu ni utapeli kama utapeli mwingine...
Wananchi wanataka viongozi kupitia kwenye mchakato rasmi unaowapa fursa ya kufanya maamuzi yao...!
Ijulikane kuwa hao waliopita ama kupitwa bila ridhaa ya wapigakura ni ishara ya muendelezo wa dharau kwa wananchi...!!
 
Mkuu nakupata vyema.
Ni haki kisheria mwenye Sifa kupata kitambulisho cha uraia.

Hadi ukipate NIDA watahakikisha hukosei au hupati kwa makosa.
Ni haki kwa mwenye Sifa kugombea. Ilibidi uwe KAZI ya tume kuhakikisha mwenye Sifa anagombea .

Yaani hii ilipaswa kuwa KPI ya NEC.
 
Ni sawa na kumzuia mtoto kula ubwabwa kwa sababu anatumia uma badala ya kumpa kijiko ili aendelee na zoezi lake jema LA kuujenga mwili
 
Wengi fomu zimejazwa vizuri ila wasimamizi wa tume polisi na takukuru wakuu wa wilaya wamebadilisha fomu hizo na kuwaengua wengine hawakuzipokea. Kabisa na wengine walisema picha zimewekwa vibaya au hazikukabidhiwa. Magufuli ni mtu hatari sana kwausalama wa nchi ana roho mbaya sana
 
wengi walijaza vizuri bali tume ya mashetani wameamua kuungana na ccm kuwaangamiza chadema
 

Upo sahihi mkuu, ingefaa kabla ya uteuzi wa wagombea tume iwe na siku kadhaa za kupitia na kuhakiki taarifa zao na pale penye mapungufu aitwe mgombea afanye marekebisho ili kumpatia haki yake ya kuchaguliwa pale alipokidhi masharti yote yaliyoainishwa na tume kwa mujibu wa sheria.

Hii ya sasa ni uhuni mtupu, kwanza wameweka sheria nyingi ambazo ukizitizama zimelenga kuweka mitego ili wagombea 'fulani' kuenguliwa.

It's something next to miracles kwamba wagombea wa ccm pekee (tena hawa tunao wafahamu) eti wamekidhi vigezo tena kwa awamu hii ya 5 tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…