Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Hakuna haja ya kujipiga kifua, kujidanganya na kuhadaa umma eti chadema hakuna mgawanyiko wala mafarakano na vita ya chini kwa chini miongoni mwa viongozi wake wa andaminizi, hasa kambi ya mwenyekiti taifa na makamu mwenyekiti wa Chadema taifa.
Ukweli usemwe ndrugu zango kwenye changamoto za wazi kabisa. Kama mtaalamu na mbobevu katika siasa, utawala na dipolomasia, mawaidha yangu ni mafupi tu.
Chadema mketi chini pamoja, zungumzeni yale yanayowafanya kuonekana mko tofauti na mmegawanyika, ridhianeni kwa amani katika meza ya mazungumzo, na hatimae mtoke na maazimio ya pamoja, kwa sauti moja na uelekeo moja kuelekea mbele.
Kinyume na hapo, vita hii baridi ya maneno inayoendelea, ikibadilika na kua vita ya vitendo, inaweza kuleta hatari kubwa zaidi na hata kuhatarisha maisha na uhai wa watu, kwasababu tu ya uchu, uroho na tamaa ya mali za chama na madaraka ndani ya chadema.🐒
Mungu Ibarki Tanzania.