GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.
Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.
Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.
Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.
Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.
Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.
Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!