Kwa utitiri huu wa watu, je, kweli tuna hifadhi hapa Ngorongoro?

Kwa utitiri huu wa watu, je, kweli tuna hifadhi hapa Ngorongoro?

°Nimekuwa nikijiuliza, masai wote hawa ni wakazi wa ngorongoro au wamewaita wenzao kutoka Kenya?
°Kwa wingi huu, je tuna urithi wa kujivunia pale ngorongoro?
°Tuweke siasa pembeni, twende na usalama wa urithi Wetu kwanza!
°Je baada ya miaka 20 tutakuwa na ngorongoro yetu?
-TUTAFAKARI KWA PAMOJA TUAMUE KWA PAMOJA!
[ ] pic fail.
Wamasai wamekuwepo hapo Ngorongoro kabla wewe hujazaliwa na hakuna uharibifu wamefanya. Wewe kule kwenu kuna hifadhi gani mmeweza kutunza kuliko hao Wamasai?
 
Wamasai wamekuwepo hapo Ngorongoro kabla wewe hujazaliwa na hakuna uharibifu wamefanya. Wewe kule kwenu kuna hifadhi gani mmeweza kutunza kuliko hao Wamasai?
Reserves has been overpopulated, masai ni wengi kuliko wanyama, OK, wacha tupate mji wa ngorongoro!
 
° Nimekuwa nikijiuliza, Masai wote hawa ni wakazi wa ngorongoro au wamewaita wenzao kutoka Kenya?

° Kwa wingi huu, je tuna urithi wa kujivunia pale ngorongoro?

° Tuweke siasa pembeni, twende na usalama wa urithi Wetu kwanza!

° Je, baada ya miaka 20 tutakuwa na ngorongoro yetu?

-TUTAFAKARI KWA PAMOJA TUAMUE KWA PAMOJA!
Ngorongoro ni Conservation area iliyoruhusiwa pia kuwa na wakaazi hasa Wamasai na Wahadzabe na Wadatooga
Bila kufikiria miaka kadhaa mbele maisha yatakuwaje kuhusu ongozeko la wakazi.
Lakini hivi karibuni, idadi ya wakaazi imeongezeka, na inasemekana kutokana na Wamasai wa Kenya kuvamia maeneo baada ya kufurushwa kwao kutokana na suala la ardhi huko ni mali ya watu binafsi.
Hii idadi imekuwa ya kubwa ya ajabu kwa kipindi kifupi, na jitihada za kuwahamisha zilianza tokea wakati wa Kikwete
 
We umeangalia watu waliojikusanya ndani ya eneo la uwanja kama wa basketball halafu ulinganishe na eneo kama Dar mara 10?

Halafu kuuza Hifadhi kwa waarabu ndio kulinda urithi?
 
Waacheni wamasai na Ngorongoro yao

Wapo toka enzi na enzi leo ndio mje kusema mna wasiwasi na hifadhi

EBU WAACHENI BWANA
 
° Nimekuwa nikijiuliza, Masai wote hawa ni wakazi wa ngorongoro au wamewaita wenzao kutoka Kenya?

° Kwa wingi huu, je tuna urithi wa kujivunia pale ngorongoro?

° Tuweke siasa pembeni, twende na usalama wa urithi Wetu kwanza!

° Je, baada ya miaka 20 tutakuwa na ngorongoro yetu?

-TUTAFAKARI KWA PAMOJA TUAMUE KWA PAMOJA!

content://com.android.chrome.FileProvider/images/screenshot/1724393575048571690834.jpg
BADO TUNAIHITAJI NGORONGORO? ndio liwe swali la kila mtu. ngorongoro ni ya kwetu, tunaweza kuamua kuiteketeza au kuihifadhi.

wakati tunapata uhuru walikuwa 10,000 sasaivi wapo zaidi ya laki mbili (200,000) wanaishi na wanyama humohumo, hawana makaburi, na wakati mwingine vyoo ni shida. wafu wanawazika wapi au wanawapa fisi wale? wagonjwa wanatelekezwa kwa fisi n.k, au watuonyeshe makaburi yapo wapi?

wanaoa wake wengi sana wanazaa bila uzazi wa mpango, kufikia miaka 10 ijayo wataweza kufika 400,000 hivi tukiwa na akili timamu, bila ushabiki, hapo ngorongoro itakuwepo au tumeamua kuteketeza ngorongoro ili watu waishi? bado tunaihitaji ngorongoro? ndio liwe swali la kila mtu. kama jibu ni ndio, hatuwezi kukaa na wananchi zaidi ya laki ndani ya ngorongoro wakati mikoa mingine watu wameshafukuzwa kwenye mbuga. mtu anayekuja leo na kusema ile ni ardhi ya wamasai, hajui kama ardhi yote ni ya umma ipo chini ya rais? au kama vipi serikali itafute pesa, wawape fidia wawaondoshe tubaki na mbuga.;msomela wamejengewa na nyumba lakini bado tu hawataki,wanachotaka ni kuteketeza mbuga ya ngorongoro. huu ndio ukweli mchungu ambao wengi hawataki kuusema. hata hapa mimi nitatukanwa kwasababu tu ya kueleza hivi.
 
Endapo kama unaakili timamu kichwani, huwezi kukubali wingi ule wa masai uendelee kuishi mahala pale, aidha wapunguzwe, kibaya zoezi hili lilishachelewa mno, hivyo wakati ni sasa, waondoke kwenye ardhi ya wanyama pori!
Sidhani kuwa wingi wa Masai ndio sababu ya kuwahamisha kutoka Ngorongoro; sababu kubwa ni Samia kutaka kuwa gawia ndugu zake waarabu maeneo ya Ngorongoro!
Angalizo kwa viongozi wa Masai kuhusu kuonana na Samia. Msikubali kuwachagua viongozi wenu kutoka vijijini kwenda kwenye huo mkutano na Samia kwani nia yao ni kutaka kuwa jua viongozi wenu toka kila kijiji ili waweze kuwathibiti!!
Malalamiko ya Masai yanajulikana hivyo sio lazima kila kijijini kipeleke muwakilishi kwenye huo mkutano na Samia. Viongozi wachache wanaweza kuwasilisha malalamiko ya Masai kama kweli Samia na serikali yake watakuwa na nia ya kuridhiana na Masai!
Je Samia na nduguze wangehamishwa toka Kizimkazi kwenda Mpanda kwa nguvu kupisha uwekezaji wa ma hotel ya kıtalıi je wangekubali?
 
Wapelekwe lindi mapori ni mengi sana huko.
Lindi ni kame. Hakuna maji hivyo nyasi ni shida. Labda huelewi lindi. Ukitoka mpakani wa mkoa wa pwani na lindi yaani marendego mpaka mtwara kule mto Ruvuma uneona nyasi na msitu wapi unaofanana na ngorongoro au serengeti? Sana upande wa iringa, songeam mbeya, katavi, sumbawanga na baadhi ya maeneo ya tabora.
 
Hao ndo wapiga kula babu yangu alinambia kipindi anakuja mjini upanga kulikuwa na Simba sasa hivi kuna magorofa
 
Wanyama wewe wengi kuliko masai, au masai wawe wengi kuliko wanyama? 😀
Hao Masai wengi kwenye picha ni wangapi na eneo husika lina ukubwa gani?

Usifanye “generalization” na kutumia hisia zaidi.

Weka data hapa.
 
We umeangalia watu waliojikusanya ndani ya eneo la uwanja kama wa basketball halafu ulinganishe na eneo kama Dar mara 10?

Halafu kuuza Hifadhi kwa waarabu ndio kulinda urithi?
Leta hapa ushahidi wa mwarabu
Mimi naleta huu
 
Hivi serikali inashindwa nini kuwaamisha kwa nguvu hao masai, mbona sehemu zipo nnyingi za kuwapekeka. Serikali iache kuwabembeleza hao masai eti wahame kwa hiari ni kupoteza muda na pesa. Wanatumia muda mwingi kuwahamisha kwa kuwabembeleza huku wanaobaki nyuma wanazidi kuzaana hivyo idadi ya wanaobaki inaendelea kuwa ile ile. Kwa pamoja tuokoe hifadhi ya Ngorongoro. Ningeomba ukuu wa wilaya ya Ngorongoro niwaamishe kwa kuwachapa viboko.
 
Unahamisha masai unaleta waarabu ni akili hiyo au Ninini hiki?
Mi nakubaliana na wewe. Wanasai na wanyama hawawezi kukaa pamoja tukitilia maanani population ya wamasai inaongezeka. Idada ya wamasai Ngorongoro imeingezeka toka 8000 (1959) mpaka 100,000 (1923),First group of Maasai families leave Ngorongoro Game Reserve | Africanews. achilia mbali na ongezeko la mifugo. Hivyo ni wazi kuwa haitawezekana wamasai waendelee kuishi na wanyama hapo porini. Ni rahisi kuwahamisha wamasai ila si rahisi kuwahamisha wanyama.
 
Back
Top Bottom