Kwa uzalendo alionao, James Mbatia anastahili kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungebi

Kwa uzalendo alionao, James Mbatia anastahili kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungebi

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Kwa uzalendo alionao kiongozi wa NCCR Mageuzi ni dhahiri kuwa anastahili kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.
Huyu jamaa kwenye masuala yanayohusu manufaa ya taifa letu hana utengano kama wale jamaa wanaotumiwa na mabeberu. Maana duniani pote nchi inapokuwa kwenye vita lazima raia wote muwe na umoja na kushirikiana.

Kama sasa taifa letu lipo kwenye majanga alafu wafuasi na Wanachama wa Chadema pamoja na viongozi wao ni kuhamasisha watu wasiwe na umoja na kuongeza hofu kwa wananchi,hii inaonyesha ni namna gani hiki chama hakifai kabisa hata kuwepo.

Wanachama na viongozi wa Chadema muda wote wamekuwa wakitaka mifarakano tu hata kama taifa lipo katika janga ambalo linahitaji umoja ili kulidhibiti. Wanasambaza habari ambazo zinatia hofu wananchi na kuleta hali ya taharuki.

Lakini James Mbatia na chama chake chenye slogan nzuri ya Udugu hana mambo kama haya ambayo hayastahili kabisa kufanywa na watu wenye akili timamu hasa kwenye kipindi kama hichi. Na kwa mantiki hii huyu jamaa huu ndio muda muafaka kujipanga ili aje kuchukua hii nafasi maana uzalendo kipimo kikubwa cha kuweza kumwamini mwanasiasa makini.
 
Mbatia ni kiongozi mwenye akili kubwa

kuna KUB moja kawafungia wabunge wake Ndani [emoji3]
 
Mbatia na Kabwe, viongozi makini sana wa upinzani.
Mungu awape maisha marefu.
 
Paw paw unganisheni huu uzi!
Back to topic,anayepata wabunge wengi ndio anaunda kambi rasmi ya upinzani bungeni!Na muamuzi wa hayo yote ni sanduku la kura kwa maana ya wananchi na si wewe wala Jiwe!
 
CCM huwa inakumbatia wapinzani dhaifu ili kiendelee kutawala!Ukiangalia sasa Mbatia,Cheyo,Mrema na Lipumba ndio aina ya watu CCM inaowapigia chapuo!
 
Paw paw unganisheni huu uzi!
Back to topic,anayepata wabunge wengi ndio anaunda kambi rasmi ya upinzani bungeni!Na muamuzi wa hayo yote ni sanduku la kura kwa maana ya wananchi na si wewe wala Jiwe!
Hausiani na huko. Acha wivu wako weee
 
Ukiona mtu anasifiwa sifiwa na Maguli basi ujue ameshafikia bei.

Hutamsikia jamaa akimsifia Mbowe hata iweje








kush and Wisdom
 
Mmechelewa Chadema ni kitu kimesha ingia damuni kwa wananchi nisawa Simba na Yanga hivyo maneno yenu ni kama ilivyo sifiwa Panafrika
 
CDM ni kambi ya jeshi isiyo rasmi maana uendeshwaji wake hauna tofauti na jeshi
 
Kwanini asiwe kiongizi huko CCM maana hata rmwenyekiti wetu mh JPM anajua hill ndio anawatumbua na kuwateua mawaziri walewale.pamja kuwa na mamia ya wabunge wa CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tume huru ndiyo dawa yenu...uhuni uhuni 2020 hatutaki!!
 
Back
Top Bottom