Kwa uzandiki aliofanya January Makamba kwa Hayati Magufuli hakupaswa kuteuliwa kuwa waziri. Uzandiki dhidi ya Rais ni kosa kubwa sana

Kwa uzandiki aliofanya January Makamba kwa Hayati Magufuli hakupaswa kuteuliwa kuwa waziri. Uzandiki dhidi ya Rais ni kosa kubwa sana

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Japokuwa uteuzi huwa ni bakshishi za kisiasa kwa watu wa karibu wa mwenye mamlaka lakini teuzi lazima zizingatie maadili,utii na sifa njema.

Urais ni taasisi na sio mtu mmoja tu. Kama January alionyesha uzandiki na hila kwa rais aliyepita na kisha akanaswa akimsengenya kimajungu mkuu wa nchi, huyu anafaa kurudi kwenye kabineti tena?

Maana ilidhihirika wazi kuwa hakuwa na utii kwa rais. Na ndio maana alidiliki kupika majungu.

Clip zilirushwa wazi na akaomba msamaha. Sasa leo ofisi ya rais imeona vipi kuwa anafaa? Japokuwa ni mzandiki?
 
Inategemea kama ni Uongozi wa Kifalme ambapo tunaamini kiongozi ni mtukufu au Uongozi ni Position tu ya muda ambayo binadamu anaweza kuishika..., Na since ni binadamu mwenye mapungufu itakuwa ni upotovu kama watu wakikaa kimya na kunyamaza pale wanapoona anakosea...

Story ya the Emperor has no Clothes ilitungwa ili kuepusha mambo kama haya....
 
Mafisiem mnasagiana kunguni, sukuma gang wote wataondolewa ni muda tu
 
Ndani ya chama unaendaje kupitishwa ugombee urais huku team jk ikiwa nje?

Unaendaje kuiba kura ingali wataalam wa ICT umewaacha nje?

January tumeamchukua siyo kwa utendaji wizarani ila kwa kazi maalum 2025 iwe rahisi kwa mana
 
Back
Top Bottom