Kwa uzoefu wangu, mashamba mengi makubwa ya bangi huwa ni ya viongozi wakubwa

Kwa uzoefu wangu, mashamba mengi makubwa ya bangi huwa ni ya viongozi wakubwa

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Ukibisha bisha tu lakini kiuhalisia ndio iko hivyo.

Pwani wilaya ya Kisarawe maeneo ya mto Ruvu nikiwa huko kulikuwa na mashamba makubwa tu bangi ya vigogo na yana wafanyakazi kama sisi tulivyo na wafanyakazi kwenye kilimo cha nyanya.

Vile napenda kuzurura nikaenda Morogoro tena hukohuko mto Ruvu yani ng'ambo ya Pwani ukivuka mto Ruvu kulikuwa na heka na heka za bangi.

Kuthibitisha hilo kuwa mashamba hayo ni ya viongozi wakubwa.

Kuna mtu aliliwa na mamba manusura baadhi ya viungo kama kichwa nk vikaonekana hivyo waliitwa police.

Bahati nzuri lile shamba la bangi lilikuwa limelimwa ng'ambo tu ya mto ule. Hivyo hata polisi walipokuja bangi waliikuta kama ilivyo nilishangaa sana na ikaachwa kama ilivyo.

Sasa ikitokea wewe ukalima basi itakupasa utoe japo 50k kama kiingilio usajiliwe uwe unalima kwa amani pasina shaka yoyote.Hii hata kwenye Pombe aina ya gongo hufanyika.

Iwapo utakaidi ukalima hata kama mashamba yenu yanapakana na aliyetoa hela utakamatwa wewe!

Hii ndo nchi yetu na mambo haya hata kwenu yapo. Kuna sehemu pia nimeona Kuna shamba ya jamaa wa mabaka kaaajiri warundi.

Habari njema ni kwamba kumbe koboko bana anakula bangi vibaya mno hadi analewa!

Mwisho.

FB_IMG_1774802644609.jpg
 
Back
Top Bottom