Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Matukio ya jana jimboni Gaza na kauli kutoka Marekani na Israel ni wazi kuwa mbabe mkubwa amekubali kistaarabu ili yaishe.
Shinikizo la kuondoa askari Gaza si la Benjamin Netanyahu kwa ridhaa yake bali limetokana na ukweli aina tofauti katika uwanja wa vita.
Ukweli wa mwanzo ni kuwa hali ya uchumi wa Israel imekuwa mbaya na tishio la Marekani kuzuia misaada liko wazi sana kutokana na majukumu yaliyolielemea taifa hilo,ikichangiwa na jeuri ya Netanyahu kupingana na kujibizana na raisi Biden.
Ukweli wa pili ni kuwa Israel imeona kuwa malengo yake hayana dalili ya kutimia, ambayo yalikuwa ni kuokoa mateka na kuwasambaratisha Hamas na wenzao ili wasiweze tena kutawala jimboni humo.
Na mwisho kama ilivyoelezwa na washirika hao ni kuwa wanajeshi wamechoka kupigana bila kuona matokeo mbali na kuua watu ovyo na wengi kutaka wapumzike.Katika hali kama hiyo kuwalazimisha kupigana na kuendelea kubaki mbali na familia zao ni hatari zaidi na mwishowe wanaweza kuasi kwa mpigo jambo ambalo limeshaanza kwa hatua za awali.
Kauli kwamba brigedia moja imeachwa kuangalia watu wasirudi kaskazini ni kauli ya kujitoa kimaso maso kwani hiyo hiyo jana mamia ya watu wamerudi makwao na bila vikwazo.Kwa upande mwengine si rahisi kwa askari waliobaki kumudu wimbi la watu kutaka kurudi majumbani mwao wakati ambapo waliweza kupenya hata kabla ya tukio hili la kuondoshwa brigedia zilizokuwa zikipiga kwa nguvu.
Baada ya yote hayo suala muhimu, ni je kuna umuhimu wa Israel baada ya uovu wao huo ihurumiwe na wapinzao wao kama vile Houth na Hezbollah.
Je, Hamas wawaachie mateka warudi makwao na Hizbullah iache kurusha makombora kaskazini ya Israel ili waisrael wanaoishi kwenye mahoteli ya kulipiwa nao warudi makwao.
Na je, Houth waache kushambulia meli na kurusha maroketi kusini ya Israel. Mara baada ya tangazo la Israel kurudisha nyuma askari tayari bei ya mafuta duniani imeshuka kidogo.