Kwa viwanja vizuri Goba, Madale, Salasala, Mbezi beach, Makongo hakikisha unawasiliana nasi

Kwa viwanja vizuri Goba, Madale, Salasala, Mbezi beach, Makongo hakikisha unawasiliana nasi

Joined
Sep 11, 2024
Posts
33
Reaction score
46
Habari za wakati huu...
Natumai wote ni wazima wa afya..
Wale ambao afya inashida kidogo Inshaallah mwenyezi atafanya wepesi tutakuwa sawa...

Leo nataka tukumbushane kuhusu kununua eneo au mali ambayo ni ya marehemu(mirathi)

AWALI YA YOTE NIENDELEE KUWAKUMBUSHA KUHUSIANA NA BIASHARA YA KULENGA VIWANJA NA MAENEO MAKUBWA..
BIASHARA HII NI YAUHAKIKA NA INALIPA SANA..
KAMA UZI ULIKUPITA BASI PITIA KWENYE AKAUNTI YANGU HII KUPATA KUIJUA ZAIDI BIASHARA HII...

TWENDE SAWA...

Leo nahitaji kukumbushana kuhusu kununua eneo ambalo mmiliki wake amefariki,
Je ni kipi na kipi cha kuzingatia wakati wa manunuzi hayo..?

Mara nyingi baada ya mmiliki wa mali kufa huwa kunamchakato wa kupata msimamizi wa mirathi wa mali zilizoachwa na marehemu...

Hapa ndio tatizo maranyingi huanzi..
Warithi wa mali kisheria huchagua msimamizi mmoja wa mali za marehemu..
Kazi ya msimamizi ni kugawanya mali za marehemu kwa warithi halali wa mali za marehemu...
Anaweza kuwa mmoja wa familia mtoto/mke/ndugu nk lakini pia anaweza kuwa rafiki au mwanasheria au yeyote yule ambae atachaguliwa na warithi halali wa mali za marehemu...

KOSA LINAANZIAGA HAPA...
Unaenda kununua mali ya marehemu unauziwa na masimamizi wa mirathi ukiamini ndio mmiliki wa mali zile kwasababu anautambulisho wa mahakama kama msimamizi wa mirathi..
Hili ni kosa kubwa sana..
Endapo atakuwa hajakubaliana na wana familia kuuza mali hiyo labda shamba/kiwanja au nyumba baada ya muda wamiliki halali wa mali za marehemu wakitambua wakaweka pingamizi utapaswa umtafute msimamizi wa mirathi akurudishie pesa zako...
Ndio akurudishie pesa zako kwasababu yeye sio mmiliki yeye ni msimamizi hata kama ndio mtoto mkubwa wa marehemu...

Kwahivyo wakati wa kununua unatakiwa kuhakikisha hati ya mahakama ya usimamizi wa mirathi inakuwa na majina yoye ya wamiliki halali wa mali za marehemu pamoja na mali zote zilizoachwa na marehemu...

Hivyo hakikisha kama waliotajwa kama warithi wa mali zote za marehemu unapata saini zao kwenye hati ya mauziano...
Kama wapo 10 hakikisha unapata sine za watu wote 10 sio uambiwe wapo 9 mmoja yupo mbali hizo ni janja janja..
Maana huyo mmoja siku akianzisha kesi mahakamani hapo huna mali tena kama utapata haki yako basi utasumbuka sanaa...

KWA VIWANJA VIZURI GOBA,MADALE,SALASALA,MBEZI BEACH,MAKONGO HAKIKISHA UNAWASILIANA NASI
☎️ +255 699 255 530
KARIBU SANA

IMG_2255.jpeg
 
20 x 20 bei gan
20 X 20 ni SQM 400
Kwa sasa Goba unapata kwa milioni 25
Kipo kiwanja cha SQM 500 kinauzwa milioni 27
Kipo mita 10 X 10 milioni 8 kipo sehemu nzuri sana unaweza kujenga nyumba ya viwili sebule jiko na choo safi kabisa kipo eneo zuri sana..
Kipo kiwanja cha SQM 700 kinauzwa milioni 38
Kipo kiwanja cha SQM 1400 MILIONI 130 lakini hiki sasa kimezungukwa na washua haswaa kwahyo mnunuzi nae ajipange kujenga ghorofa 😅
Kuna kiwanja kina SQM 400 kipo Half london GOBA mtaa huu ndio kila nyumba ni ghorofa elewa kila nyumba Boss
Unaweza kuingilia Diz Pub kama unapafahamu inahitajika milioni 50 tuu...
pia kipo kiwanja kina SQM 1100 kinauzwa milioni 65 tu kipo barabara kubwa kabisa ya mtaa kipo tambarare kabisa na kina barabara mbili mbele na nyuma
☎️ +255 699 255 530
Vipo viwanja vya milioni 200,150 nk
Karibu sana
 
Kazi nzuri mkuu, kikubwa kusiwe na janjajanja za kujeruhi wateja.
 
Back
Top Bottom