Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HahahahahaaDraft raha sana...
Kuna kopi ukicheza hufungwi
1-Samba
2-Bana Mbili
3-Sumu ya pandu
4-Mnara mrefu
Rest in peace juma mchafuMangwelele ana hatari yake
Ye ndo mwalim wa marehem mchafu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Haya na wewe panda kitandani.
Hapo unamwambia mtu aliyekua anaonyesha kete akiwa nje sasa zamu yake ya kuingia imefika
Haya na wewe panda kitandani.
Hapo unamwambia mtu aliyekua anaonyesha kete akiwa nje sasa zamu yake ya kuingia imefika
Sio kweli draft kila sehem nayoenda hapa tanzania naikuta... Moshi niliikuta, mwanza kigoma ,dar , tabora, mbeya n.k... Drft ni kila kitu kwanguSehemu za kucheza draft zimejaa wachawi wazee wapwani
Wenyewe wanasema unafuata vyumba tu... 😂😂Hahahahahaa
chupi upande
banana chop
Samba INA pati one na two
Alafu kuna samba kompyuta
Kata Mara mbili
Aise kuna as tunawekaweka ila kuna watu wanacheza
mnifundishe hizo styleHahahahahaa
chupi upande
banana chop
Samba INA pati one na two
Alafu kuna samba kompyuta
Kata Mara mbili
Aise kuna as tunawekaweka ila kuna watu wanacheza
[emoji8][emoji8]Mida Fulani ya jioni hivi baada ya kutoka kwenye Mishemishe zetu ama shughuli za hapa na pale zinazotupa mapene na kufanya pochi zetu ziwe nene
Huwa hatuna kilevi kingine zaidi ya Drafti likisaidiwa na kikombe cha kahawa au tangawizi bila kusahau kashata na karanga mbichi
Kama kawaidi kwa vijiwe vilivyoendelea wale ma B ama mapopoma wanakuwa na drafti lao na wale watabe tuna kuwa na la kwetu
Raha ya Drafti maneno bhana! maneno haswa tena Yale ya kumchefua mtu nyongo
Baadhi ya maneno ya karaha niliyowahi kuyasikia ni haya hapa japo si mengi!
"Ukiona tajiri anaanza kukumbusha madeni yake ujue maji yameshamfika shingoni"
hapa unamwambia mtu uliyemfunga kama bado anakukumbusha magoli aliyokufunga juzi au Jana
"Ukiona mgonjwa mpaka maji anataka yalainishwe anzeni kuandaa ratiba ya mazishi"
Hapa anaambiwa mtu aliyebanwa mpaka anaanza kutema kete ovyo
"Kisa mkeo Malaya basi na wewe umeamua kuwa shoga ili nae akipita wamsemee",
Haya unayasema baada ya kumbana mpinzani wako
"Huyu bwana ana mapenzi ya papa,mpaka maji yatikisika"
Hapa unamwambia shabiki wa mpinzani wako
"Haya chukua ringi lako ukaendeshe",
Baada ya kumfunga mtu hapo
"Kashaanza mikwara ya mlevi!mlevi kakimbizwa kwanzia kariakoo mpaka tazara kufika mlangoni, mlevi:nyoko wee! Mme wangu vipi?
mlevi:si huyu hapa!"
Hapa anaambiwa mtu aliyetoa sare kwa bahati
"Cheza pimbi wewe! aliyekwambia radio call ina screen touch Nani?"
"Tangu lini shimo La panya linazibwa na mkate bhana"
Hapa anaambiwa mtu aliyefungia kingi kwa kete
"Umejibanabana mwenyewe! kazini umeenda kwa miguu!Leo umekufa siku ya mshahara"
Hapa mtu kafa mchezo wa mwisho
"Bando langu unanichagulia cha kuposti?
Hapa unamwambia yule bingwa wa kuelekeza michezo akiwa nje
"Utaweza kushikiria bomba hapa na morogoro?"
Unamwambia mtu anayetaka kuzuia sare
"We ungekuwa mchawi ungeroga mpaka kuku"
hapa anaambiwa mtu aliyeonyesha kete Kali
"Hapa timu moja haijafika" au "Hapa nacheza peke yangu,"
Haya unayasema kama unacheza na popoma
"Huu kama uchi wa mtoto! utaishia kuutazama tu"
Haya wadau tupieni na nyie ya kwenu
lolote mliowahi kuyasikia
Katiffah Dangote?!!
Apo unakuta unajibiwa ulipewa mke lkn chongoNilishapewaga mke kwa ajili ya hili dudu (DRAFT) sema alinishinda matumizi tu
Hapa unaongea ukiwa ushamuwahi mwenzako king